ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,851
Wana JF uliza swali lako lolote kuhusu madini, mafuta na gas, kuanzia njisi yanavyojitengeneza ardhini, kufanyiwa utafiti, kuchibwa hadi kuuzwa nawe utajibiwa na mtaalamu wako hapo.
mkuu kujenga huo mtambo ya kurifine natural gas ikatumika majumbani ni gharama sana. Imagine plant za madimba na songosongo kwa kuprocess gas cost ni almost 2.5Trilion wakati cost ya LNG plant zidisha hiyo cost mara 10Kwanini Gas yetu asilia haiwekwi wazi kwamba twaweza ku i refine na tukapata gesi ya jikoni na bidhaa nyingine? Petroleum?
Ni vitu gani hasa vinasababisha mafuta kujitengeneza huko chini ya ardhi? na ni kwa nini kuna baadhi ya maeneo mafuta yako kwa wingi sana tofauti na pengine? mfano huko uarabuni toka enzi na enzi uchumi wao ni mafuta tu..itatokea hizo reserves ziishe? huku kwetu je kiasi kilichogundulika kinaweza kufikia kiwango walicho nacho? Kuna tofauti ya mafuta yanayopatikana baharini na yale yanayopatikana kwenye maziwa? Inawezekana kupata mafuta au gas eneo la nchi kavu? mfano pale Ruvu naona kuna shughuli inayoendelea nikaambiwa ni utafiti wa mafuta na gas? kuna viashiria gani vinavyoonesha kuwa hapa kuna mafuta na gas?
Kwanini Gas yetu asilia haiwekwi wazi kwamba twaweza ku i refine na tukapata gesi ya jikoni na bidhaa nyingine? Petroleum?
Bilionea Asigwa.Gesi ya helium kwa volume iliyoko hata Tanzania inawezekana kujengewa kiwanda na ikauzwa baada ya kuwa processed au inauzwaga hivyo hivyo ikiwa raw??
Vipi kuhusu dhahabu, kwa nini dhahabu kwenye machimbo madogo huwa inafumuka kwa msimu bila kutumia nguvu yoyote kuichimba, na baadaye kupotea kabisa.??
Hili jambo la dhahabu kufumuka na baadaye kupotea ni la kitaalamu au ni mambo ya kishirikina??
1: Zamani enzi za mababu zetu walikuwa wanaokota dhahabu juu ya ardhi kwanini isiwe sasa au madini yaliyopo juu ya ardhi yaliisha na kama yaliisha ilikuwaje wakae juu ya ardhi kipindi hicho?
2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?
3: Nasikia Mchanga wa Madini una tabia ya kuzaliana na baadae kuwa madini je kuna ukweli juu ya hili na kama ni kweli kwanini?
4:Kuna aina ngapi za Madini duniani na ni madini gani ni ghali kuliko yote.
5:Je hapa duniani kuna (nchi) ukanda ambao hauna madini yeyote yale ?.
6:Je Kuna Mahusiano gani kati ya madini na Miamba?
7: Gesi na Mafuta hutofautiana nini?
8: Kwanini Nchi nyingi za Uarabuni zina Mafuta sana?
9:Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?.
10:Ni dalili zipi za awali huonekana katika ardhi yenye Madini,Mafuta na Gesi kabla ya utafiti kufanyika(huwa kuna dalili zipi).
11:Naomba kujua hii gasi ya kupikia ina tofauti gani na hii gasi iliyopo hapa Nchini (Mtwara).
12: Mafuta ya Ndege Gari na vyombo vingine huwa yanatofautiana nini?
Naweza kujibu kama ifuatavyo Mr Mreno
2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?
Jibu
Mafuta hutengenezwa kutokana na mkusanyiko wa masalia ya viumbe hai na mimea ambavyo kwa pamoja hufukiwa na mchanga (sediments) kwa kipindi kirefu sana (millions of years) hasa katika maeneo ya mabonde, maziwa, bahari (basin area), mgandamizo na joto linalotokana na kinakirefu cha mchanga kilichofukia masalia ya viumbe na mimea ndicho kinachopelekea kuzalishwa kwa mafuta, gesi na makaa yam mawe (fossil fuels).
7.Gesi na Mafuta hutofautiana nini?
Jibu
Gesi na mafuta vyote hutengenezwa katika namna inayofanana kamailivoelezwa katika swali na 2 kinacholeta utofauti ni joto na mkandamizo unaotumika kutengeza,
Mafuta yenyewe hutengezwa katika joto kati ya (65'C na 150'C) joto hili hupatikana kutika kina 2000m mpaka 5500 meter, Joto likizidi 150'C basi hizo organic compounds ambazo zingekuwa mafuta sasa zitakuwa gesi asilia na likizidi 250'C basi izo organic compounds zitabadilika nakuwa graphite. (kumbuka Joto na mgandamizo huongezeka kadiri kina kinavyo ongezeka.
9. Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?
Jibu
Napenda kuelezea kuhusiana na gaharama za gesi na mafuta pekee.
Kwanza gharama zinaanzia katika utafutaji na badae tutaona katika uzalishaji, ntaelezea katika mukitadha wa kitu kinaitwa oil and natural gas life cycle.
1. Gharama za kupata access (gaining Access)
Hizi ni gharama zitakazo husiana na kupata vibali katika mamlaka mbalimbali lakini pia kupata documents au taarifa za awali (data) kuhusiana na eneo amabalo unapanga kufanya utafiki ( gharama hizi zitategemea sana sheria na aina ya mikataba katika nchi husika lakin wastani ni dola za kimarekani 20 million na hutumia kati ya miaka 0 mpaka 2 kukamilisha taratibu katika kipengele hiki.
2. Gharama ya kufanya utafiti (exploration cost)
Gharama hizi zitahusisha tafti mbalimbali za awali utakazo zifanya kama aerial survey, seismic ( ambazo unaweza kuzifanya kwakutumia meli kama ni baharini au tracks kama ni nchi kavu) lakin pia gharama za kuchimba kisima kama tafiti za awali zitaonesha dalili njema za kuwepo mafuta au gesi na gharama za kufanyia analysis sample mbalimbali ambazo utazitoa kwenye kisima (gharama zake zitategemea eneo unalofanyia utafiti kama ni kinakirefu cha bahari au kifupi au nchi kavu) wastani wa gharama za kuchimba kisima kimoja katika nchi kavu (onshore) ni dola za kimarekani million 1 mpaka million 15 kutokana na urefu na complication za mahari kilipo wakati kuchimba kisima kimoja katika kina kirefu cha bahari (offshore) (1000 meta na kuendelea) ni dollar za marekani kuanzia million 100 nakuendelea ,so hapo utajumlisha na gharama nyingne za tafiti za awali ambazo zitategemeana na watoa huduma. Unaweza tumia miaka 4 au zaidi katika kipindi hiki cha exploration.
3. Gharama za kuchimba visima vingne zaidi kwa ajili yakujiridhisha kiasi kilichopo katika eneo (appraisal phase cost)
Katika hatua hii utalazimika kuingia gharama za kuchimba visima vingine kadhaa kama kisima ulicho chimba awali kimeonesha matumaini ya kuwepo mafuta au gesi, katika hatua hii visima vinaweza kuwa vitatu au zaidi kwa gharama zile zile nilizo zioredhesha katika point no 2, umhimu wa hatua hii nkutaka kujua jumla ya kiasi kilichopo katika eneo lako atachoweza kuzalisha, unaweza tumia miaka 2 au zaidi
4. Gharama za kuandaa miundo mbinu ya uzalishaji
Katika hatua hii sasa utakuwa tayari umejua kama kitaru chako kina mafuta au gesi au vyote kwa pamoja hivyo utatikiwa kuandaa mazingira ya uzalishaji kulingana na aina ya product iliyopo.
Kama ni gesi asilia ndo ipo
Itakulazimu kuandaa mazingira ya uzalishaji kutoka na soko lilipo kwanza itabidi kujenga kisima kiwe nahadhi ya uzalishaji na sio utafiti tena, hapa utaweka mabomba ya kuzalishia kuanzia chini ya kisima mpaka kwene well head na kisha utajenga kiwanda cha kuisaficha gesi kwani huwa inazalishwa ikiwa na viambata mbalimbali ambavyo hupunguza efficiency ya gesi lakin pia husababisha ugumu wa kuisafirisha.. gharama zake zitategemeana na wingi wa gesi unayo zalisha lakin pia aina na kiasi cha viambata ambavyo unataka kuvitoa kwani kuniaviambata vingine ambavyo ni complex kuviondoa kama hydrogen sulfide, but Tanzania hatuna gesi yenye sulfur gharama za kujenga plant hii ya kasafisha inaweza kurange kati ya dola million 100-200 million kwa kiwanda chenye uwezo wakuzalisha wastani wa 80-180MMcft per day , harafu utatandaza mabomba kutoka kiwanda cha kuchakata kilipo mpaka kwa wateja wako kama watakuwa hawapo mbali sana ( kama ndani ya nchi au nchi jirani ) gharama zake ni umbali wa kutoka mtwara mpaka somanga fungu, songosongo mpaka somangafungu harafu somanga fungu dsm imecost kama pesa za Tanzania zadi ya 1 tillion.
Lakin kama wateja wako wapo nchi za mbali lets say Tanzania to china hutoweza kujenga mambomba kwa umbali huo itakulazimu kujenga LNG plant ambapo itakuwezesha kubadilisha gesi yako kutoka kwenye gesi form kwenda katika liquid form hivyo basi mbali nakujenga kiwanda cha kusafisha gesi itakulazimu kujenga pia LNG plant kwa gharama zake zitategemia nakiasi utakacho safirisha kwa mwaka kam itakuwa ni tani million 1 kwa mwaka kiwanda chako kitagarimu takiribani dola za marekani 1.5bilion hii nikwenye plant ya kupabadilishia gesi kwenda kwenye liquid form lakin ikifika sokoni itabidi kujenga plant itakayo badilisha kuirudisha kwenye gesi form kiwanda hiki kitagharimu takribani dola za marekani 1 bilion uwezo wake itakuwa nikubadilisha kiasi cha gesi yenye ujazo wa 1billion cubic feet per day.
Kuhusu gharama za uzalishaji wa mafuta
Hapa itakulazimu kwanza kuchimba kisima cha uzalishaji au kubadilisha kisima kilicho chibwa kwaajili ya utafiti kiwe cha uzalishaji hivyo utaweka mabomba maalum kwa ajili kutoka chini mpaka juu kwenye well head baada ya hapo utaweka mabomba kutoka kwenye well head mpaka kwenye refinery plant ambayo utaijenga kulingana na wing I wa mafuta unayo zalisha, mfano Uganda wanataka kujenga refinery plant yenye uwezo wakuzalisha mapipa 60000 kwa siku kwa bei ya 2.5 billion dollar unawezakupata picha ya gharama zake lakin wakati huo huo kunakiasi cha mafuta kama 200000 ivi watapitisha Tanzania mpaka bandari ya Tanga kupitia kwenye bomba litakalo jengwa kwa gharama za shilingi 4 billion usa dollar so unaweza kuona how this iverstment cost a lot
So issue nkwamba ni ngumu kujua nkipi kinagharama kubwa kuliko kingne kutokana na mazingir za hiyo product ilipo, composition zake na soko lako
Bwana lazaroKuna teacher mmoja alinifundisha wakati nikiwa skuli flani akiniambia medulla yangu INA madini sasa nataka kujua madini hayo ni aina gani na nitayatoaje?
Bwana nzalendo jibu lako linajibiwa vizuri sana na NATURAL GAS UTILIZATION MASTER PLAN 2016-2045. Hii ni plan ya serikali ya Tanzania itakavyotumia gas. unaweza kuisoma hasa ukurasa wa 15 hadi 31. . ila pia kumbuka gas haifanyiwi utafiti na TPDC. Bali ni makampuni binafisi hupewa vitalu na kufanya utafiti na kulingana na sheria serikali inamiliki 20% na hivyo mipango ya uanzaji wa udhalishaji gas na mafuta inategemea mipango ya mabwana wakubwa wanaomiliki hisa kubwa pia pesa za kuendeleza miladi.Kwanini Gas yetu asilia haiwekwi wazi kwamba twaweza ku i refine na tukapata gesi ya jikoni na bidhaa nyingine? Petroleum?
Bwana ginius. nitakujibu kwa kigezo cha kikemia ambacho ndiyo kinafanya zitofautiane hata kimatumizi.Kuna tofauti gan kati ya mafuta na maji
1: Zamani enzi za mababu zetu walikuwa wanaokota dhahabu juu ya ardhi kwanini isiwe sasa au madini yaliyopo juu ya ardhi yaliisha na kama yaliisha ilikuwaje wakae juu ya ardhi kipindi hicho?
2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?
3: Nasikia Mchanga wa Madini una tabia ya kuzaliana na baadae kuwa madini je kuna ukweli juu ya hili na kama ni kweli kwanini?
4:Kuna aina ngapi za Madini duniani na ni madini gani ni ghali kuliko yote
5:Je hapa duniani 5:Je hapa duniani kuna (nchi) ukanda ambao hauna madini yeyote yale ?.
6:Je Kuna Mahusiano gani kati ya madini na Miamba?
7: Gesi na Mafuta hutofautiana nini?
8: Kwanini Nchi nyingi za Uarabuni zina Mafuta sana?
9:Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?.
10:Ni dalili zipi za awali huonekana katika ardhi yenye Madini,Mafuta na Gesi kabla ya utafiti kufanyika(huwa kuna dalili zipi).
11:Naomba kujua hii gasi ya kupikia ina tofauti gani na hii gasi iliyopo hapa Nchini (Mtwara).
12: Mafuta ya Ndege Gari na vyombo vingine huwa yanatofautiana nini?