Japo sikupenda sana ulivyo m discibe mleta mada...ila Nimependa maelezo yako!! Natarajia masomo zaidi ya solar !!!
Swali: je kabla ya kupaata battery na nimesha size panel yangu...nitajua vipi mahitaji yangu ya umeme mfano nna redio...tv..pasi...friji....ntajuaje vinahitaji power gani ili nikanunue battery stahiki???
Je panel gani ni nzuri na battery gani zinadumu???
Zipo solar pv panels za aina nyingi lakini common na zenye ufanisi mzuri ni mbili tuu
1:monocrystalline solar pv
2
😛olycrystalline solar pv
Ukianza na hii monocrystalline hii huwa ina efficiency ya 15-20%
Pia hii panel inakuwa na umbo dogo kwa watts sawa sawa na ile itakayoundwa kwa mtindo wa polycrystalline hivyo hii panel tunasema inahitaji eneo dogo tuu kwaajili ya installation.
Kuitambua hii panel inakuwa na vipande vya silicon (silicon cells) zilizo katika umbo kama la octagonal in shape pia inakuwa na rangi moja tuu kama ni nyeusi ni nyeusi kote kama ni blue basi ni blue kote .
Pia life span ya monocrystalline ni 25 years.
Ukija hii solar panel aina ya polycrystalline utaona hii efficiency yake inarange 13.5-17%.
Pia inakuwa na umbo kubwa kuliko monocrystalline for the same amount of power.
Kuitambua hii panel utaijua kwakuangalia cells zake huwa na umbo la rectangular au square pia zinakuwana rangi tofauti tofauti unapoitizama yani inakuwa kama spectrum fulani hivi.
So ukija ukicheki ishu ya price, mono zinauzwa bei kubwa kulipo poly kwa mfano unaweza kuya poly ya 100watts ni 250k wakati kwa power hiyo hiyo utaipata mono kwa 350k so nazani hapo nimejaribu kukuchambulia kuhusu solar panel ipi ni bora.
Nije kwenye issue ya battery
Zipo aina tatu tuu za battery
1:FLA
2:GEL
3:AGM
Nizielezee kwa ufupi sana nikianza na hiyo ya kwanza FLA- flooded lead acid battery hii ndio battery common sana inayotumika katika shughuli nyingi.
Pia inauwezo wa kuishi muda mrefu na bei yake ni ndogo sana ukilinganisha na GEL.
Mapungufu yake ni kwamba itakuhitaji uwe unalifanyia checkups mara kwa mara maana maji ya battery hupungua kadiri linavyo chajiwa.
Aina ya pili GEL- Gelled electrolyte sealed lead acid battery.
Sifa kuu ya hili battery linahitaji voltage kidogo tuu ukilinganisha na other types of lead acid battery so ukilitumia hili hata kama jua sio kali unauhakika lita jaa maadamu unatumia solar panel nzuri kati ya zile nilizoainisha hapo juu.
Swala lako lingine umeuliza utajuaje loads zako na ukatoa mfano wa vifaa ulivyo navyo na ukauliza utajuaje size ya battery linalokufaa kuendesha hivyo vifaa vyako.
Jibu ni kwamba kila kifaa cha umeme unacho nunua kimeandikwa power yake kwenye name plate yake so unachotakiwa ni kusoma power za kila kifaa halafu jumlisha upate total yake labda tuseme wewe umepata total ni 800watts, baada ya hapo unatakiwa ujue wewe unataka battery lakuweza kuendesha hizo 800watts kwa masaa mangapi? Kwa mfano tuseme wewe unataka masaa matatu (3hours) sasa hapa nitakufundisha njia rahisi ya kufanya assumptions ambayo nahisi ndio rahisi na pia ipo accurate so assume wewe umechagua battery la 100Ah/12V, hili battery inabidi utafute power yake na formula ya power inasema ni voltage times current so chukua 100Ah×12V=1200Wh then hili jibu ulolipata gawanya kwa total loads zako ambazo tume assume kuwa ni 800watts so ukichukua 1200Wh÷800W=1.5hours lakini sisi tulitaka buckup tym ya masaa matatu(3hours) lakini kwa battery moja la 100Ah limetupa 1.5hours kwa load yetu ya 800watts je utafunga battery ngapi kuweza kupata backup tym ya 3hrs? So chukua 3hrs÷1.5hrs=2 nahili jibu la mbili ni kwamba zitahitajika battery 2 za 100Ah na zitafungwa in parallel kutengeneza 200Ah so kumbe ukichukua 200Ah×12V=2400Wh then ukichukua hii 2400Wh÷800W=3hrs ambayo ndio required backup tym tuliokuwa tunaitaka kwa loads zetu za 800watts
Nazani nimejaribu kukujibu kwa kifupi unaweza pata kitu kidogo ukifuatilia na pia soma majibu ya wadau wengine watakao jaribu kukujibu pia.