SoC03 Uliwengu wa kidigitali katika kuongeza ufanisi wa kiutendaji(Sensa & Kupiga kura)

Stories of Change - 2023 Competition

Ndundame

Member
Jul 8, 2023
60
72
MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIGITALI KATIKA UCHAGUZI & SENSA YA WATU NA MAKAZI.
Miongoni mwa mambo mazito katika utekelezaji ususani kwa nchi zinazoendelea ni maswala mazima ya kuendesha na kusimamia zoezi la uchaguzi pamoja na sensa za watu na makazi.

Gharama nyingi sana utumika kusaidia uendeshaji wa zoezi hili, hali inayopelekea mataifa mengi yanayoendelea kutegemea ufadhili kutoka njee ili kuwezesha haya yaweze kufanyika kwa weredi.
Lakini tukitazama kwa kina uzito au sehemu kubwa ya gharama zinazofunika mambo haya muhimu ya sensa na upigaji kura (uchaguzi) ni zile ambazo sio za lazima pia zinaepukika ukizingatia maendeleo ya teknolojia tuliyonayo zama hizi.

BAADHI YA CHANGAMOTO ZA MIFUMO YA SASA YA UCHAGUZI & SENSA
Ebu tujiulize kama tumeweza kuedesha mifumo mikubwa kama mfano utumishi( Ajira portal) ambayo inatumika katika usaili wa watu wengi kabisa nchi nzima kuna ulazima gani kufanya yafuatayo;

1.Kuweka bajeti kubwa kwaajili ya semina za mafunzo ya makarani wa kusimamia uchaguzi na kusimamia zoezi la sensa?

2. Kutenga bajeti kubwa kuwalipa rasilimali watu safu nzima(wasimamizi wa vituo, makarani, walinzi n.k) wanaosimamia mazoeazi hayo?

3.Kutumia muda mwingi, gharama na nguvu nyingi kuanza kuhesabu vituo vyote nchini, kujaza taarifa na kuanza kuzikusanya pamoja ili kupata matokeo ya jumla?

4.Kusimamisha watu kwenye foleni kutwa nzima wasimamishe shughuli zao za uzalishaji mali ambazo zingeweza kupelekea kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja & taifa kwa ujumla?

5.Kupita nyumba hadi nyumba kwaajili ya kukusanya taarifa za kila kaya Tanzania nzima kwaajili ya zoezi zima la sensa.

6.Kutokana na umuhimu wa kuwa na taarifa za watu na makazi sensa haikuwa ya kupangwa ifanyike mara moja kwa interval ya miaka kumi ila ufinyu wa bajeti na ukubwa wa gharama za kufanikisha zoezi hili ndo maana ukapangwa muda wa miaka kumi, badala yake kama tutaweza kufanya zoezi hili kwa gharama za chini tunaweza punguza hata huo muda kwaajili ya kuweza kupata taarifa sahihi kwa wakati ili kuweza kupanga mikakati ya kimaendeleo kwajili ya taifa.

7.Kura zinazo haribika, kura zinazozidi idadi ya wapiga kura walioandikishwa, tuhuma za kuletwa masanduku yenye kura katika vituo mbalimbali hali ambayo imashusha imani ya wapiga kura kuhusu matokeo ya uchaguzi kutokana na dosali zinazoonekana katika usimamizi wa uchaguzi.(malalamiko ya kuibiwa kura kil uchaguzi)


MTAZAMO
NB:
Kwanini basi tusingetumia watu wetu wa ndani watuundie mfano wa mifumo au app kama tulizo nazo au wakaunda kutoka kwa mifumo ya nchi zilizoendelea wanayotumia katika kutekeleza mambo kama haya yetu ambapo wataalam wetu wangeweza wakaboresha tukawa tunafanya haya kidigitali hali ambayo ingeweza ikaleta tija na faida kama zifuatazo.

FAIDA ZA KUTUMIA MFUMO WA KIDIGITALI
1
. Kutunza muda(Time saving) muda wa kusimama foleni kutwa nzima katika uchaguzi(kupiga kura kituoni) au kupita nyumba hadi nyumba kwenye sensa ya watu na makazi huu muda tungetumia katika mambo mengine ya msingi,

Mfano mtu unalog-in kwa kutumia namba zake za kadi ya mpiga kura, unaona orodha ya wagombea unachagua baada ya hapo punde unapata ujumbe kuwa kura yako imetumwa kikamilifu na kupokelewa(mfano wa jumbe tunazopata tukituma maombi ya ajira), pia ukishatuma huwezi kupiga tena kura.

2.Ingepunguza usumbufu wa kuanza kuhesabu na kujumuisha kura moja moja kwa vituo vyote vya kupiga kura (manually).

3.Uwazi na Haki, haya malalamiko yasingewepo kila uchaguzi kulalamikiwa masanduku yanaingizwa kituoni yenye kura, kura zinazidi idadi ya wapiga kura n.k ( ila pia kuna ulazima wa tume huru ya kusimamia huu mfumo ili haya kuwezekana kwa 100%).

4.Gharama za uendeshaji zingepungua sana tena sana kutokana na wasimamizi wachache kuhitajika maana mfumo unajiendesha wenyew na kutoa jumla kwa haraka.

5.Wakati wa uchaguzi mtu angeweza kupiga kura akiwa mahala popote pasina ulazima wa kuhitajika kurudi katika kituo alichojisajiria kwaajili yabkuoiga kura.

Mfano mtu alijisajiri mtwara vijijini kutokana na pilika za maisha akajikuta anaendesha maish yake musoma, wakati wa uchaguzi kwa sasa atalazimika aache shughuli zake zote, ajigharamie kwa nauli aende hadi alipojiandikisha ndipo akapige kura, hii hainakaa sawa wengi wanapotezaga haki zao za kikatiba za kuchagua viongozi wanao wapenda.

Hivyo kwa mfumo huu ungesaidia sana kuwezesha mtu kutumiahaki yake kumchagua mgombea wake akiwa popote ulimwenguni cha msingi awe alijiandikisha kwaajili ya kupiga kura, akapata kitamburisho, akanisajili kwa kufungua akaunti ya kupiga kura mtandaoni

Angalizo
Sambamba na faida hizi chache ambazo zinajikita katika mitazamo ya kiuzarendo kwa maslai ya taifa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, wale waliokosa uzarendo, mafisadi, wapenda rushwa hawataweza afiki hili maana litazuia upigaji kwa maslai yao binafsi

CHANGAMOTO KUU YA KUTUMIA MFUMO HUU
Licha ya faida hizi najua changamoto itakuja kwa walio vijijini na wasio na uwezo wa kufikia intaneti au simu janja, licha ya kuwa tukiangalia kundi ili ni dogo tena sana ukilinganisha na waliona uwezo wa kutumia na kufikia intaneti kwa zama hizi tulizo nazo,

NAMNA YA KUKABILIANA NA HII CHANGAMOTO
Hilo kundi dogo lingeweza kuwa na wasimamizi wachache katika vituo vya uchaguzi kutoa msaada wa kulog-in katika akaunti zao kupitia namba za kipekee ya kwenye vitamburisho vya mpiga kura husika na kumpa nafasi kumchagua mgombea wake kupitia vishikwambi vya serikali na kulog-out anafata mwengine, kutoka na uchache wao bado isingeathiri utendaji mzima.
Pia katika swala la sensa mtu analog in anajaza au kujibu maswali kwa taarifa zake .

USHAURI KWA SERIKALI
Hivyo basi naishauri serikali, kupitia wizara husika ni muda sasa wa kuleta mabdiliko chanya ya kidigitali katika nchi yetu kwaajili ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa wafadhili na kuingia mikopo mikubwa kuwezesha mambo ambayo yanaweza kutekelezeka kwa gharama ambazo tunaweza kuzimudu na hivyo kuwezesha fedha zingine zitumike katika mambo mengine ya kimaendeleo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

MENGINEYO/ NYONGEZA MUHIMU YA KUHITIMISHA
Sambamba na haya ni ukweli usiopingika kuna kila haja ya kuwa na tume iliyo huru ya uchaguzi ili kuimarisha demokrasia pamoja na kurejesha imani kwa kundi kubwa la watanzania ambao wameanza kujikatia tamaa kwa kutoaminia kuwa kupitia upigaji kura wa mfumo uliopo kuwa utawawezesha kumchagua mgembea wa mahitajio yao.

Wako katika ujenzi wa taifa💥

Mzarendo mpenda amani🤗

Mungu ibariki Tanzania🇹🇿🙏


🇹🇿Tanzania ya kidigitali ni Sasa!🏅🌉⚡
 
Back
Top Bottom