SoC03 Mfumo wa Upigaji Kura Kidigitali na Kielectroniki

Stories of Change - 2023 Competition

Tibaiwa

Member
Sep 8, 2021
50
38
(MFUMO WA KIDOLE GUMBA)

Kidole gumba ni wazo la kuanzisha mfumo wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya kidigitali na kupiga kura kielektroniki kwa kutumia alama ya kidole gumba. Wazo hili linahitaji ushirikiano wa pande mbili, yaani tume ya Taifa ya uchaguzi NEC pamoja tume ya Taifa ya vitambulisho vya uraia NIDA.

Kupitia tume ya vitambulisho vya taifa, taarifa za upigaji kura ziongezwe na kuamishiwa kwenye mfumo wa kidole gumba ambao utakuja kuwa chini ya Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC kwani kitambusho cha utaifa kina taarifa zenye kuonyesha umri sahihi wa mwananchi ambapo kila mwananchi mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na minane ni haki yake ya msingi kupiga kura katika kumchagua kiongozi anayempenda kuwa kama mwakilishi wake au msimamizi wa jambo fulani.

UMUHIMU WA MFUMO HUU WA UPIGAJI KURA KIDIGITALI “KIGORE GUMBA”
Baada ya kuanzisha mfumo huu wa kielektroniki wa kupiga kura “ Kidole gumba” kutasaidia sana Taifa la Tanzania kutoka kwenye mfumo wa analojia yaani “kura za kupiga na kuhesabu kwa kutumia karatasi” na kutumia mfumo wa kisasa kwa kutumia vishimwambi au vifaa vinavyotumika sasa hivi katika kasajilia namba za simu kwa kutumia alama za vidole baada ya mwananchi kuingiza kitambulisho chake cha utaifa kwenye chombo hiki na kukiamrisha kwenye programu ya kupiga kura.

Mfumo huu wa “kidole gumba” utarahisisha zoezi la kupiga kura kwa kutumia muda mfupi, pamoja na zoezi la kuhesabu kura kwani kila chama kitakachoshiriki kwenye uchaguzi kitakuwa kinamtuma wakala wake kwenye “kituo kikuu cha kupokea taarifa za uchaguzi” na kuhesabu moja kwa moja kura zinazopigwa na hii itapunguza hali ya foleni na kukuza mwitikio wa wananchi kupiga kura.

Mfumo wa kidole gumba utaondoa wasiwasi juu ya wizi wa kura kama vile masanduku kukutwa na kura ambazo zimeishapigwa tiyari kabla ya zoezi zima kuanza kwani kadi hii ya “kitambulisho cha utaifa” kitakuwa kinasoma na kufanya kazi mara moja na hii ni baada ya mhusika kuweka alama yake ya kidole kwenye kifaa husika na hii iwe ndani ya muda yaani dakika zisizozidi tatu au tano.

Kupitia mfumo huu wa “kidole gumba” Tanzania litakuwa taifa la kwanza ndani ya bara la Afrika kama sio dunia kwa kuanzisha mfumo wa kupiga kura unaoendana sayansi na teknolojia kuliko kura ya karatasi.

Kidole Gumba utakuwa mfumo wa kuzuia matumizi ya wino wa kuchovya na kidole cha mwisho ili kuzuia mtu mmoja kupiga za kujirudia ambapo wino unaotumiwa sio salama kwa ngozi ya binadamu kwani mfumo huu utatambua kitambulisho cha mtu amabacho tiyari kimeisha husika kwenye kupiga kura kwani utakuwa na uwezo wa kuzuia alama ya kidole gumba kupiga kura kwa hawamu ya pili.

Mfumo wa kidole gumba utasaidia sana kupunguza gharama za uendeshaji wa zoezi la kupiga kura kutokana na urahisi utakao kuwepo. Mfumo huu utasaidia sana kwenye elimu yetu ya Tanzania kwani utaitaji zaidi kuandaa mazingira, wanafunzi na wananchi katika kuwaweka kwenye utayari wa kumakinika na somo la “TEHAMA” na utafanya elimu hii iwe yenye tija kwa kumtoa mtanzania kwenye mifumo ya “kizamani” analojia na kujikita zaidi kwenye teknolojia.

Mfumo huu utachochea upatikanaji wa huduma zingine kwa wananchi, kama vile umeme kwani uendeshaji wake utaitaji nishati ya umeme hivyo utailazimu serikali kuhakikisha inaendelea kusambaza huduma ya umeme kwenye maeneo yanayokosa huduma hii.

Mfumo huu unaweza kuzalisha ajira hata nje ya nchi kwani ukileta mafanikio makubwa utakuwa mwanzo wa kuunadi hata nje ya nchi na kuombwa vijana wanaoweza kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya kuuendesha.

Mfumo huu utakuwa na kurasa au vyumba maalumu vyenye picha ya wagombea na vyama vyao vya siasa na kumhitaji mpiga kura aweke ala ya tiki au kidole gumba kwenye picha ya mgombea anayemtaka.

Haki ya kupiga ni kwa mtu yeyote aliye na umri wa kuanzia miaka kumi na nane (18) hivyo kama ni mtanzania utamwondolea vigezo kandamizi kama vile kumtaka kurudi sehemu aliyojiandikisha au mpaka hawe ameisha jiandikisha kwenye daftari boreshwa la mpiga kura kwani atakuwa na uhuru wa kupiga kura mahali popote lakini kwa mara moja tu.

Mfumo huu hauna haja kubwa ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kuwasajili wapiga kura wapya kila mara, yaani wale wanaofikisha umri wa miaka kumi na minane ndani au kabla ya uchaguzi husika kufika kwani raia kila atakapo weka kadi yake ya kitambulisho cha utaifa kama hajafikisha umri huu mfumo huu utamkatalia hatua ya kufikia kipengele cha kupiga kura.

“Siasa ni mchezo” na uwanja wa kumpata mshindi harali wa mchezo ni zoezi la kupiga kura, hivyo mfumo wa kidole gumba utakuwa kama VAR yaani video assistance refarii kwenye zoezi la upigaji kura na kuratibu zoezi zima lilivyoenda na kuurudia pale itakapohitajika kuondoa dosari au utata baada ya matokeo kutangazwa kwani hakutakuwepo na vitendo vya kusubiri ushaidi wa kurudia kuhesabu karatasi.
 
Back
Top Bottom