Ulishughulika vipi na kisa cha namna hii?

Ulishughulika vipi na kisa cha namna hii?

Huyu msichana nilisoma nae 'A' level katika shule fulani hapa Dar es salaam. Darasani kwetu hakuna ambae hakumjua maana alikuwa msichana mwenye sura nzuri sana tena kuliko wote darasani. Ila hakuwa social kiviile. Alikuwa na rafiki zake aliowazoea na hakupenda mazoea sana.

Sasa mi nikawa nimempenda. Nikaanza kumtongoza tokea tunaanza form five. Kipindi ambacho mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza kumtongoza pale shuleni lakini alinikataa. Baada ya miezi mitatu nikapiga moyo konde nikamtongoza tena akakataa nikapotezea.

Tukiwa tunafanya mitihani ya mwisho tunaingia form 6 nikasema ngoja nijaribu tena nikamtongoza tena kwa mara ya tatu akakataa. Nikamuomba namba ili tuwe tunawasiliana maana kuna rafiki yangu mmoja 'Kishoro' (bado marafiki mpaka sasa) alinishauri bora niwe naenda nae taratibu niwe nawasiliana nae namuhonga honga vocha, na ukizingatia kilikuwa kipindi cha mitihani tunakaribia kwenda likizo. Nikamuomba namba akaninyima.

Baadae tukiwa likizo nikaitafuta namba yake kwa mtu mwingine. Nikampigia simu akawa ananijibu kwa mkato ili maongezi yaishe nikimtumia meseji hajibu kabisa.

Nikaacha kuongea nae tukaingia form 6. Nikawa najaribu kwenda nae taratibu nikawa nalazimisha urafiki. Akawa ananikwepa kwepa. Hataki story na mimi. (Inauma sana aiseee!). Kuna siku nilimuomba twende Kunduchi beach jumamosi kila kitu nitalipa mimi (baada ya kukopa sana maana mwanafunzi hela unatoa wapi ?). Akakataa nikaja kuskia Jumamos alienda Beach kombo na monitor wetu nilikuja kuambiwa baada ya kumaliza kuwa wakati tunakaribia kumaliza alianza mahusiano na monitor.

Tukiwa tunakaribia kufanya paper ya Form 6 nikataka nimtongoze tena akakataa kuongea namimi. Ila tu nikamwambia "Sawa. Ila hakuna msichana nilikuwa nampenda kama wewe". Hakujibu akaondoka. Tukafanya paper tukamaliza.

Toka tumemaliza form 6 sikuwahi kuonana nae tena. Nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita(degree)
Kazi nnayoifanya ni tofauti na niliyosomea. Sio ya maslahi ila inaniwezesha kuishi Dar. Nilishamsahau maana hatujaonana mda mrefu. Sasa juzi(jumatatu) niko makumbusho nasubiri daladala ya ubungo nikashangaa naguswa bega. Kugeuka ni yeye. Moyo ukapiga paa. Nilishangaa sana maana hakuwahi nianza mazungumzo wala kunisalimia popote.

Akaniambia Danny za siku nyingi nikamwambia safi. Tukaongea sana. Sana, tukakumbushana watu tuliosoma nao, mambo ya shule. Ila Gari la Kunduchi lilipofika akataka kupanda aondoke. Akaniambia "Danny naomba namba yako tuwasiliane." Nikashangaa sana. Nikampa namba.

Nilivofika nyumbani nikawaza sana kwamba kinachotokea ninaota ? Prisca wakuniomba mimi namba ? Mimi ambae miaka kadhaa iliyopita alininyima namba yake nikaitafuta kwa mtu mwingine ?

Ilivyofika saa tano kasoro akanipigia simu nikapokea. Tukaongea stori kibao. Hakusema kwanini amenipigia zaidi ya story za hapa na pale. Akanipa story za UDSM (mimi nilisoma SAUT). Baadae tukaagana nikalala. Ila asubuhi wazo la kwanza lililonijia ni kuwa yawezekana Prisca anataka kunikubali sasa hivi. Maana haiwezekani Prisca anipigie mimi Danny simu hivihivi. Tena Prisca, anipigie mie simu ?

Jumannne hatukuwasiliana ila Jana jumatano alinipigia simu mchana akanilaumu sana kwa sauti ya mapenzi mbona sikumtafuta siku ya Jumanne ? Mi nikamwambia 'sikuwa na vocha' ila sikuwa na sababu ya kumtafuta kusema ukweli. Tukiwa tunaongea na simu hiyo jana akaniuliza vipi wifi mzima ? Nikamwambia sina mwanamke. Akaniambia anataka kuja kunitembelea Jumamosi. Nikamwambia nikipata muda ntakwambia.

Nikakutana na Kishoro kumuomba ushauri. Alichoniambia ndicho kinachonifanya nilete uzi hapa.

Kishoro alisema: "Hakupendi huyo, ila tu anakuja kwako kupooza machungu kwa sababu aliowataka yawezekana kagombana nao. Sasa we jiangalie wewe unampenda ama humpendi?".

Mimi, naweza sema nampenda ila sio sana kama nilivyokuwa nampenda kipindi kile; ni kama alinitoka kiukweli, ila sijiskii vizuri kumpotezea. Nipo single na nataka KUOA(sitaki mahusiano ya kucheza cheza) lakini nafsi yangu inasita kumuoa yeye.

Ila pia maneno ya Kishoro yanajirudia rudia sana kwenye akili yangu "Hakupendi huyo, do for your own risk."

Halafu mimi mwenyewe nashangaa. Alivyokuwa ananitreat kipindi kile, leo hii Prisca ananipigia simu ? Ananiuliza mbona sijamtafuta ? Halafu anataka kuja kunitembelea ? Huyu ni Prisca kweli au naota ndoto za mchana ?

Anyway, Yawezekana humu kuna watu waliwahi kupitia kisa kinachofanana na changu na wangependa kushare uzoefu wao jinsi walivyoshughulika na hivyo visa. Ntafurahi nikipata kuskia kutoka kwenu.

Lakini pia dada zangu mtanisaidia maoni yenu; Je, inawezekana kwa mwanamke ambae alikuwa hakupendi miaka ya nyuma akaja kwako kwa upendo wa dhati ?

NB:Kuna vitu vingi nimevitoa ili kufupisha story, kama bado ndefu mniwie radhi
Mkuu, huyo demu hakupendi, sikiliza maneno ya rafiki yako. Just kula mzigo then move on. Huyo demu anajifanya kukutafuta kipindi hiki kwasababu mapenzi aliyoinvest miaka hiyo yaliishia shimoni. Believe me, atakusumbua sana ukimpa moyo wako.

Kwasasa hana cha kufanya kwasababu hana mtu wa maana anayempenda kwa dhati thats why amekutafuta wewe bwege mtozeni wake. Akipata anayempenda kwa dhati hatofikilia hata kwa dakika kukuacha!

Hayo yalitaka nitokea mie though kwangu mie ni tofauti kidogo. Maana mie alinikubalia, bahati mbaya yeye alifeli na mie nilifaulu. Nimpenda sana and so sikujali ufaulu wake. Niliendelea n advance yeye akaenda veta. Alianza leta usumbufu wa kutopokea simu na kujibu hovyohovyo. Nikaamua kumsahau. Kaja nitafuta nikiwa naingia chuo mwaka wa kwanza, mixer anapiga simu mpka kuniuliza kama nimekula, offcourse moyo ulitaka niendelee naye pale tulipoishia but akili ikakataa.

Nimemaliza chuo ikabidi nimchane live tu kuwa siwezi kuwa naye maana alishapoteza chance yake kipindi kile nipo shule, afterall alishazalishwa na jamaa haeleweki kama atamuoa.

Take care chief.
 
Changamoto yangu kaka ni Je, tutaishi kwa upendo maana sijui kama kweli kaja kunikubali kwa moyo mkunjufu au la !!!
Kakukubali bahati mbaya..
Maana am sure she wasn't single mlivoonana Makumbusho.
Ila umetokea wa ahueni ya alienae mda huo. Si ajabu pia anapima kwanza kuona ka bado unamshobokea ka mwanzo. Akicomfirm tuu umo basi gwaride litaanza(kukutesa)
 
Form 5, alikuwa bado ana akili za kitoto...na kwa kuwa unataka mke basi mpe nafasi, mkaribishe, mtoke muende sehemu iliyotulia ya wazi (siyo kwako wala lodge) umsikilize, mdadisi na pia ujaribu kuuliza kwa waliosoma udsm tabia zake n.k...sikushauri kumla bila kujua historia yake tangu mlivyomaliza form 6. Sikushauri kabisa kumla kama ataanza kujirahiisha ili umtie siku ya kwanza kukutana.

Kuhusu kuliwa sana hiyo ni kawaida, kwa wanafunzi wa chuo, wakimaliza chuo wanakuwa wamechapika kweli kweli hasa kama alikuwa ni slay queen, ila siyo wote.

Mahusiano ya shule na chuo kwa asilimia kubwa hayana clarity in terms of future, things don't work out, you move on...haina makombo. Ila onyo usimle bila kumfahamu vizuri
 
Wanyooshe vidole wale wote waliooa wanawake ambao waliwakuta bikira au hawajawahi kudate na mtu yoyote, hao pekee ndio wanapaswa kumshauri Danny achape lapa...

Otherwise bwana mdogo Danny, katika kusoma andiko lako hakuna mahali ulipoweka bayana sababu ya wewe kukataliwa na Prisca mkiwa sekondari...

1.Kuna uwezekano binti alikuwa na mtu
2.Kuna uwezekano binti alifundwa vyema na wahenga zake
3.Kuna uwezekano hakuwa amepevuka akili kujua mwanaume anayemuhitaji maishani ni nani

Ushauri:
Anza mahusiano naye lakini pitia hatua zote za kumuelewa Prisca ni nani, na ni kwa nini akuhitaji wakati huuna sio wakati uliopita.

Tuchukulie kwa sasa ukamtosa Prisca, je huyo utayempata mwingine una hudubini ya kuweza kujua habari zake za zamani?
Ushari mzuri
 
Prisca alikuwa sahihi kukukataa akiwa kidato cha tano na sita.
Kwa sasa acha awe rafiki kwanza, kama kuna masahibu yoyote yametokea utajua tu.
Si sahihi kumhukumu mtu mzima kwa makosa aliyofanya akiwa mtoto.

Awe rafiki kwa sasa.

Kama utaona kuna sababu ya kuanzisha mahusiano basi kila la kheri
 
mchunguze kwanza historia yakr ana kazi? sasa hiv ana maon gan kuhusu maisha?
vip amedhoofu labda?
mchek kwanza na ummulize kipind kile ilikuwaje kuwaje.
usichape kabla ya ndoa shaur yako.mchuma janga utakula na wa kwenu
 
Kaka apo 100% ni Jumba Bovu sikushauri kuwa nae...Apo karuka ruka wee kaona mambo sio mambo anae mtaka hamtaki sasa anatafuta atakae mtaka...cha kufia nini si alijitia jeuri funika kombe nasema funika. Nakushauri ivi kwasababu lolote litakalo kuja kutokea uko mbeleni tofauti na matarajio yako ndugu yangu utakuja kulalamika sana na utapata stress mbaya haijawai tokea.


Good thing ni kwamba alisha kutoka japo sio mazina as you said ila fanya mishe zingine mpotezee atakutoka kabisa. Wanawake wapo wengi Kaka songa mbele kama ambulance uku unalia. ukifika utanyamaza
 
Hili suala lipo""" Nami nilishawah kataliwa sana kipindi cha nyuma huko"" 2014 hiv!!! Nilimpenda mno jacky!!!
Nakumbuka niliwah kumbembeleza day 1 hivi""" mchana mpka nilipiga magoti na machoz!! (Stend ya mabas ilikua)

Kisa alikua ki"chuo flan hiv! Afu mi msela wa mtaan!! Yaan sio type yake
Kmmk!!!!!!! Kimaelezo kutoka kwake""

Mkono wangu wa kushoto nilichora jina eruf! Ya kwanz ya Jina lake" kwa kutumia wembe"""" damu iliruka aswaa"" ajabu sasa"" wala akustuka zaid ya kusema nitolee uchuro wako hapa""""

Jack"" huyu alisababisha nionekane fala kwa ndugu zangu wote"" baada ya kugoma kula kwa siku 2 mpka nguvu zikaniisha"""

Mkuu nilipambana mnooooo......
Kusaka life kwa hasira"
Japo sina elimu kubwa...naishukulu serikali iliniona"" nikala shavu upande mmoja hivi;;;;;

Nilikutana nae 2019 hapo Nov""""alinitunuku nilimla na"kumuacha mkuu"" japo analia lia sana kweny social net!!!......to be cont.....
 
Bila shaka yupo wa moyo wako ambaye unamfuatilia kabla hujaonana na 'Prisca' hiyo juzi. Kama kweli yupo basi shikilia na endelea kufuatilia ujiridhishe ukiwa na nafasi na uhuru wa kufanya maamuzi sahihi.

Prisca wa stendi ya Makumbusho siyo yule wa kipindi mko shule. Kumbuka alikukataa wewe pamoja na vitu vingine ni kwamba alishakuwa na uliyemtaja kuwa ni monitor wenu na si kwamba alikukataa kutokana na kuhofia kuharibu 'shule'. Baada ya monitor ni mdosi gani alishikilia chombo hadi sasa apate wazo la ghafla kukukumbuka? Hala hala mti na macho kaka. Na kuna uwezkano mkubwa maamuzi utakayo chukua hivi sasa ambapo hata nafsi yako inagoma si tu kukubaliana na hali halisi unayoiona bali hata kuamini kinachojiri basi maamuzi hayo yanaweza kubeba majuto kwa siku za usoni maana haukujiandaa na hili kipindi hiki. Hujui kabeba nini SIRINI mwake/mwilini mwake ambacho anataka kukitua kwako.

Naamini ingekuwa anakupenda kweli asingesubiri mapenzi hayo ayaoneshe kwa tukio la ghafla hapo stendini bali angefanya namna yoyote kukupata kwani kwa vile nyie mlifahamiana mkiwa shule ni kwamba mna mtandao wa 'classmates' kwa hiyo hata asingeshindwa kupata mawasiliano yako. Je, msingekutana hapo stendini ingekuwaje?

Pamoja na haya yote tunayoyaandika kuchangia kwenye mada yako wewe ndiwe pekee MUAMUZI WA MWISHO. Ila ukumbuke kuwa kosa moja goli.

Asante
 
Kwani wewe mleta mada, ujawahi kuwakataa mademu waliokupenda ila baadae ukagundua wako fire kinyama
 
Hiyo haraka ya Prisca ina walakini mwingi mno.

Nenda naye taratibu inaonesha ana stress sana na mahusiano aliyonayo au aliyowahi kupitia.

Muda unaofikiri upo salama ndiyo huwa wa hatari zaidi.
 
Afate huu ushauri
Wengi wamekushauri eiza uachane nae au uchape usepe. Mimi nitakushauri tofauti kidogo. Hebu kwa sasa mtazame Prisca kama mtu aliyepevuka na anaejitambua. Unakosea kumlaumu mtu wa form 5 kukukataa kimapenzi!!! Huyo alikuwa mtoto jomba. Kweli wewe ulivyokuwa form 5 kiakili ndio ulivyo sasa? Na inaonekana bado unampenda Prisca, acha ligi zisizo na future, kwa sasa wote mmeshapevuka tuliza mpira. Mpe nafasi wala usichukulie maubishani ya form 5. Mpe nafasi, pimeni afya jenga familia kijana. Kweli ulinganishe maisha ya kwenda bichi komba na monita ndio yakunyime future na umpendae?
 
Kwa niaba ya rafiki yangu danny napenda kuwashukuruni nyote kwa ushauri wenu naahidi tutaufanyia kazi na mambo yataenda sawia mi ni kishoro mshikaji wake mtoa maada. Hatuhitaji tena ushauri imetosha. asanteni sana
Asante kwa kumuwakilisha. Yule jamaa (Kishoro) hanaga muda wa mitandao. Anasemaga mitandao inaweza vunja ndoa yake😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom