Ulishawahi kuwa na marafiki wa aina hii?

Hii iliwahi kunifikirisha sana....kuna jamaa marafiki zangu kama wawili huwa mpaka wananifokea kama sikjawasaidia kiasi cha hela wanachoomba....sasa nilijaribu kuulizia kuna mchungaji akaniambia hiyo ni baraka aliyokupa Mungu amekuchagua wewe akuwezeshe ili uwasaidie wengine, yaani ridhiki zao zinapitia kwako..na hivyo hautakiwi kulalamika bali unatakiwa kumshukuru Mungu sababu hautakuja kufilisika....endelea kuwasaidia jinsi unavyoweza.....basi nimekuwa mpole....na dili hazikauki kwangu... yaani kadri wanavyoomba na ninavyotoa...miamala inasoma si kitoto...Asante Mungu
 
Mim hakuna Baraka yoyote bana
Labda nikupee namba yake akukope awe anakulalamikia kila saa utapata hizo baraka mim sizitaki
 
Daaah sasa wewe ni binadamu au zombie?
 
Achana nae Dina rafiki wa hivyo anakupenda ukiwa nacho ngoja uishiwe sasa kama utamuona

Mwambie ukweli kama anaweza badilika kama hawezi mwepuke taratibu

Nishamchana ukweli na nimemuambia kwaherii
Alikuwa ananipa stress hakika
Mim sijawah mlilia shida maana najua nae ana shida zake napambana na hali yangu
 
Nishamchana ukweli na nimemuambia kwaherii
Alikuwa ananipa stress hakika
Mim sijawah mlilia shida maana najua nae ana shida zake napambana na hali yangu
Umefanya vizuri sana
Urafiki wa kweli ni kwa shida na raha kwa wote wawili sio wewe pekee uwe tegemezi kwa mwenzio

Bora uwe na rafiki wachache ambao unajua ukipata tatizo hata usiku wa manane wanaamka wapo upande wako
 
Rafiki wa kweli huwa analetwa na mwenyezi Mungu,katika maisha yangu hadi sasa sijawahi kufikisha hata marafiki watano nadhani nimewahi kuwa na marafiki wa tatu tu tena kwa nyakati tofauti lakini wamekuwa zaidi ya ndugu hata mtu nikimwambia mtu yule ni rafiki yangu anakataa nadhani ni ndugu kabisa!
N:B,sivuti bangi,sivuti sigara,situmii kilevi chochote,sitoki out weekend!kama sina issue yeyote sitoki ndani wala sipigi simu ovyo na huwa sibadilishi wanawake ovyo pia ni ngumu sana kumuamini mtu
 
Umefanya vizuri sana
Urafiki wa kweli ni kwa shida na raha kwa wote wawili sio wewe pekee uwe tegemezi kwa mwenzio

Bora uwe na rafiki wachache ambao unajua ukipata tatizo hata usiku wa manane wanaamka wapo upande wako
Nna marafiki wengine hata hatusumbuani kabisa na tunaelewana na wala hawanilalamikii ,pale nilipatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…