Mimi ni mpole na ni mtu wa kukubali yaishe, marafiki wengi wamenidhulumu!

Wrevta

JF-Expert Member
Jan 18, 2023
1,440
1,720
Kazo iendelee! Mimi ni mpole na mkimya toka utoto. Mpaka muda huu ni mtu mpole, naumia mno jamaa au rafiki yangu akipata matatizo. Najiona ni kama mimi ndiye ninayepata matatizo hayo, nashughulika na matatizo ya rafiki na jamaa zangu kama matatizo yangu.

Mara nyingi nimekuwa mtu wa kukopesha ila matatizo yakinikuta hakuna wa kunikopesha wote wanasema hawana. Naishia kukomaa mwenyewe tu kibishi kimya kimya.

Siyo msumbufu wa kudai, mara nyingi ni mpaka mtu akumbuke mwenyewe kunilipa, nakumbusha mara chache sana kuhusu deni langu.

Hali hii mpaka wazazi wanaifahamu na wamenionya mno kuwa walimwengu si kama niwafikiriavyo.

Ninasoma mwaka chuo, kwanza kabisa kuna rafiki yangu aliwahi kunikopa hela nikampa, akiahidi atarejesha baada ya week moja. Yeye alikuwa na mkopo asilimia zote mia, mimi sikuwa na asilimia mia. Nilithamini tatizo lake nikamkopesha.

Leo hii ni mwaka umepita na simu zangu hakupokea wala kujibu meseji, nimesamehe ingawa nilisikitika sana. Urafiki ulivunjika na yeye ndiye aliuvunja kwa hela ndogo namna ile.

Huyu mwingine alinunua viatu vyangu kwa mkopo, mpaka leo ni miaka hajanilipa hata senti. Na hashtuki kwa lolote.

Huyu mwingine pia alikuwa na shida nikamkopesha hela, aliahidi baada ya siku 3 tu. Leo ni mwaka na kitu hajanilipa hata senti. Nilipomtumia meseji hakujibu, nilipopiga simu hakupokea.

Leo hii amepata shida tena ndipo amekumbuka kuanza kunitafuta, na tumewasiliana kwa kama week mbili hivi akanieleza ana tatizo nimkopeshe hela.

Hivi mimi nina matatizo(upole wangu na ukarimu) au hao rafiki zangu ndiyo wana matatizo?

Naumia mno kwa alivyonieleza shida yake na nahisi nitamkopesha tena hela.

Kinachoniuma ni kuwa, marafiki wengi wanaonizunguka ni kama wakinipiga hela wanapotea na naona ni kama wanakuja kwa lengo hilo.

Mimi hata msichana akinililia shida nilikuwa nikimpa kama ninacho bila kutegemea malipo yoyote hasa ngono.

Huenda naonekana lofa kwa wema wangu huu. Nabadilikaje na ndiyo nipo hivi?

Maisha yangu muda mwingi ni ya upweke na nayapenda maisha haya na kutoyapenda kwa wakati mmoja.

JF ndiyo imekuwa kama mama na baba kwangu wakati huu niwapo mbali na familia.

Sijui naonekanaje, wasichana wengi niliowakopesha hawakunilipa hela zangu, najiuliza mbona wengine wanalipwa?

Turudi kwenye suala la mwanzo, nina tatizo au rafiki zangu ndiyo wenye matatizo? Kwa kweli naumia mno kuona mtu wa karibu yangu anateseka, hata akiwa mnyama naumia pia.

Huu ndiyo udhaifu wangu, naogopa kupiga wanyama mno, hata mende kuua naogopa sana achilia mbali panya na mijusi. Nathamini uhai wa kila kiumbe.

Nakuja kwenu baba zangu, kaka zangu na dada zangu mnishauri huenda nikawa mimi ndiye mwenye shida.
 
Komaa kiume hii Dunia ni uwanja wa vita,hukusoma biology o level 'survival for the fittest'

Sasa mtoto wa kiume sijui unaogopa hata kuua Mende? Ukiwa baba wa mji akiingia nyoka kwako utakimbia au? Mtu kashakukopa kakuzulumu anakuja tena kukukopa afu unasema "nahisi ntampa tu, siwezi kumnyima"

Komaa mtoto wa kiume utakuja kuombwa visivyoombeka, shauri yako
 
Kazo iendelee! Mimi ni mpole na mkimya toka utoto. Mpaka muda huu ni mtu mpole, naumia mno jamaa au rafiki yangu akipata matatizo. Najiona ni kama mimi ndiye ninayepata matatizo hayo, nashughulika na matatizo ya rafiki na jamaa zangu kama matatizo yangu.

Mara nyingi nimekuwa mtu wa kukopesha ila matatizo yakinikuta hakuna wa kunikopesha wote wanasema hawana. Naishia kukomaa mwenyewe tu kibishi kimya kimya.

Siyo msumbufu wa kudai, mara nyingi ni mpaka mtu akumbuke mwenyewe kunilipa, nakumbusha mara chache sana kuhusu deni langu.

Hali hii mpaka wazazi wanaifahamu na wamenionya mno kuwa walimwengu si kama niwafikiriavyo.

Ninasoma mwaka chuo, kwanza kabisa kuna rafiki yangu aliwahi kunikopa hela nikampa, akiahidi atarejesha baada ya week moja. Yeye alikuwa na mkopo asilimia zote mia, mimi sikuwa na asilimia mia. Nilithamini tatizo lake nikamkopesha.

Leo hii ni mwaka umepita na simu zangu hakupokea wala kujibu meseji, nimesamehe ingawa nilisikitika sana. Urafiki ulivunjika na yeye ndiye aliuvunja kwa hela ndogo namna ile.

Huyu mwingine alinunua viatu vyangu kwa mkopo, mpaka leo ni miaka hajanilipa hata senti. Na hashtuki kwa lolote.

Huyu mwingine pia alikuwa na shida nikamkopesha hela, aliahidi baada ya siku 3 tu. Leo ni mwaka na kitu hajanilipa hata senti. Nilipomtumia meseji hakujibu, nilipopiga simu hakupokea.

Leo hii amepata shida tena ndipo amekumbuka kuanza kunitafuta, na tumewasiliana kwa kama week mbili hivi akanieleza ana tatizo nimkopeshe hela.

Hivi mimi nina matatizo(upole wangu na ukarimu) au hao rafiki zangu ndiyo wana matatizo?

Naumia mno kwa alivyonieleza shida yake na nahisi nitamkopesha tena hela.

Kinachoniuma ni kuwa, marafiki wengi wanaonizunguka ni kama wakinipiga hela wanapotea na naona ni kama wanakuja kwa lengo hilo.

Mimi hata msichana akinililia shida nilikuwa nikimpa kama ninacho bila kutegemea malipo yoyote hasa ngono.

Huenda naonekana lofa kwa wema wangu huu. Nabadilikaje na ndiyo nipo hivi?

Maisha yangu muda mwingi ni ya upweke na nayapenda maisha haya na kutoyapenda kwa wakati mmoja.

JF ndiyo imekuwa kama mama na baba kwangu wakati huu niwapo mbali na familia.

Sijui naonekanaje, wasichana wengi niliowakopesha hawakunilipa hela zangu, najiuliza mbona wengine wanalipwa?

Turudi kwenye suala la mwanzo, nina tatizo au rafiki zangu ndiyo wenye matatizo? Kwa kweli naumia mno kuona mtu wa karibu yangu anateseka, hata akiwa mnyama naumia pia.

Huu ndiyo udhaifu wangu, naogopa kupiga wanyama mno, hata mende kuua naogopa sana achilia mbali panya na mijusi. Nathamini uhai wa kila kiumbe.

Nakuja kwenu baba zangu, kaka zangu na dada zangu mnishauri huenda nikawa mimi ndiye mwenye shida.

Kuwa mpole but kuwa na msimamo, dont talk too much ila draw the line linapokuja suala la kutetea maslahi yako
 
Sio kwamba unavinasaba vya usamaria,la hasha,maana usingekumbuka Wala kuumizwa na madeni unayodai.Tatizo ni uboya wako,na hao washkaji washakuona kama pussy flani.Mtafute mmoja mpe vitasa hevi itatoa picha Kwa hao wengine,na hawatarudi kukudhulumu.
N.b mchague unayemmudu
Ahsante. Sijakumbuka kwa kuwa nataka ha zirudi hapana, nilishasamehe. Ila najitathmini nachukuliwaje hasa?
 
Back
Top Bottom