Tupeane mbinu, mnapambanaje na Ndugu wenye tabia hii?

NJOGHOMILE

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
657
1,868
Mtu yupo kwenye utumishi wa umma kwa miaka 13, wenzake walioingia kwenye utumishi pamoja naye, tayari wana maisha yao. Huyu ndugu hamna alilolifanya, yaani hamna jambo lolote la maendeleo. Sijui salary anapelekaga wapi hata kama anaishi mjini, wenzio nao wanaishi humo mjini kama yeye ila wao wana nyumba, usafiri, familia(ingawa na huyu ndugu naye ana Familia lakini kwa 99% ni mke tu ndio kama Baba wa Familia)

Jamaa sasa hivi anakimbizana na namba(yrs) kuelekea 40 kwenye umri ambao huwa tunaambiwa ndio umri unatakiwa uwe ushaanza maisha!

Tabia yake inayokera ni kuomba pesa(sio kukopa, ni kuomba labda tuseme Chawa, maana Chawa ananyonya, huku anamuacha aliyemnyonya akiathirika) kutoka kwa ndugu, asipopewa anakasirika na kuzua ugomvi anaona ndugu hawamtendei haki, huyu ni mtu mzima ndio yuko hivi.

Ana mambo mengi ya hovyo kabisa ambayo hayafai kuwa kwa mtu mzima kama yeye, ila anasikitisha.

Kwa mtu wa namna hii mnadili naye vipi...
 
Kuna uzi humu ulishawahi kuwekwa jamaa kaajiriwa anapokea milioni 2 kasoro ila mshahara ukiingia, wote unachukuliwa na mwanamke aliekuwa anaishi nae, yeye anapewa laki 1 tu ya matumizi mpaka akaanza kuishi maisha yaliyostua ndugu zake, mwanamke alikuwa kamkamata akili mpaka ndugu zake waliona hio sio hali ya kawaida ikabidi wajiongeze kuvunja hio minyororo isiyoonekana

Lakini pia

Namjua mmama ni jirani anafanya kazi Tra lakini hana hata gari.

Ndugu zake wengi wanamtegemea, yeye ndie mkombozi wa ukoo wao.

Usihitimishe mambo haraka.
 
Bongo hatari.
Yawezekana huyo mama ndiyo muadilifu katika utumishi wa umma ila wananchi mnamwona pimbi.
Namjua mmama ni jirani anafanya kazi Tra lakini hana hata gari.

Ndugu zake wengi wanamtegemea, yeye ndie mkombozi wa ukoo wao.

Usihitimishe mambo haraka.
 
Naomba nikujibu hivi....
Kuwa na maendeleao ni akili ya mtu na mtu....

Hujawahi kuona makazini huko.. kuna mtu/watu wana mishahara mikubwa kukuzidi...wana Safari kila leo....ndani na nje ya nchi..

Ila ukiwaangalia hakuna wanachokuzidi...Na inawezekana umewazidi mbali sana.
 
Namjua mmama ni jirani anafanya kazi Tra lakini hana hata gari.

Ndugu zake wengi wanamtegemea, yeye ndie mkombozi wa ukoo wao.

Usihitimishe mambo haraka.
Huyu jamaa ninayemsema yeye ndio anataka kutegemea ndugu zake, yaani hana plan zozote za maisha zaidi ya starehe, hata familia yake, ni mke ndio anapambana pekee yake.

Sasa imefikia wakati ndugu wamechoka na hiyo tabia yake maana mara nyingine anapiga matukio kama kutapeli halafu msala unawaangua ndugu zake endapo atafikishwa korokoroni, hili lishawahi kutokea
 
Ikiwa hujui undani wake usipende kuhukumu.

Hakuna faraja katika umaskini na hakuna binadamu anaependa dhiki na kudhalilika kwa kuomba omba.

Ikiwa sio mlevi wa kujulikana au muasherati basi weka akiba ya hukumu yako kwake.

Hakuna anaependa bughudha ya daladala, kila mtu anapenda kuwa na usafiri wake, hakuna anaeona raha kupigizana kelele na mwenye nyumba, kila mtu anapenda kuishi kwake. Ila ikifikia kuona mtu anapanga na kupanda daladala ujue kuna sababu zilizokwamisha umiliki.

Kuwa na kipato hakumaanishi ndio kuweza kumudu kila majukumu. Kuna kipindi majukumu huelemea kipato.
 
Nyie ndio aina ya ndugu ambao hua mbawapangia kakazenu hadi mke anaepaswa kumuoa.
Alafu kwani akinywea pombe pesa yake yote wewe unapungukiwa nini??
Hajakatazwa kunywea pombe, ila anywee jasho lake na sio kuomba majasho ya watu wanaojinyima ili wafanye mambo maana. Linalokera ni hili.

Hivi mtu mwenye plan za maendeleo atanyimwa support kweli?
 
Naomba nikujibu hivi....
Kuwa na maendeleao ni akili ya mtu na mtu....

Hujawahi kuona makazini huko.. kuna mtu/watu wana mishahara mikubwa kukuzidi...wana Safari kila leo....ndani na nje ya nchi..

Ila ukiwaangalia hakuna wanachokuzidi...Na inawezekana umewazidi mbali sana.
Ni sahihi usemacho lakini ukianza kuwa tegemezi ilihali ulipaswa kutegemewa unakuwa mzigo. Yaani mtu ana kipato/mshahara halafu anaenda kuomba wengine wanaohustle kivyao, haileti sense
 
Ikiwa hujui undani wake usipende kuhukumu.

Hakuna faraja katika umaskini na hakuna binadamu anaependa dhiki na kudhalilika kwa kuomba omba...
Sikupingi ulichokisema lakini laiti ungeweza kupata nafasi ya kudadisi kuhusu huyu ninayemsema, hii comment yako ungekuja kuibadilisha.

Wapo wa namna hiyo unaowasema, na wa namna kama huyu pia wapo
 
Sikupingi ulichokisema lakini laiti ungeweza kupata nafasi ya kudadisi kuhusu huyu ninayemsema, hii comment yako ungekuja kuibadilisha.

Wapo wa namna hiyo unaowasema wapo, na wa namna kama huyu pia wapo
Na ndio maana nikasema 'ikiwa hujui undani wake'.

Ila kama kuna la zaidi unalijua basi puuzia comment yangu mkuu.
 
Hajakatazwa kunywea pombe, ila anywee jasho lake na sio kuomba majasho ya watu wanaojinyima ili wafanye mambo maana. Linalokera ni hili.

Hivi mtu mwenye plan za maendeleo atanyimwa support kweli?
Kwani hua anawalazimisha ama anawashikia visu hadi mumpe pesa...??
 
Mtu yupo kwenye utumishi wa umma kwa miaka 13, wenzake walioingia kwenye utumishi pamoja naye, tayari wana maisha yao. Huyu ndugu hamna alilolifanya, yaani hamna jambo lolote la maendeleo. Sijui salary anapelekaga wapi hata kama anaishi mjini, wenzio nao wanaishi humo mjini kama yeye ila wao wana nyumba, usafiri, familia(ingawa na huyu ndugu naye ana Familia lakini kwa 99% ni mke tu ndio kama Baba wa Familia)

Jamaa sasa hivi anakimbizana na namba(yrs) kuelekea 40 kwenye umri ambao huwa tunaambiwa ndio umri unatakiwa uwe ushaanza maisha!

Tabia yake inayokera ni kuomba pesa(sio kukopa, ni kuomba labda tuseme Chawa, maana Chawa ananyonya, huku anamuacha aliyemnyonya akiathirika) kutoka kwa ndugu, asipopewa anakasirika na kuzua ugomvi anaona ndugu hawamtendei haki, huyu ni mtu mzima ndio yuko hivi.

Ana mambo mengi ya hovyo kabisa ambayo hayafai kuwa kwa mtu mzima kama yeye, ila anasikitisha.

Kwa mtu wa namna hii mnadili naye vipi...
Kama ni mwalimu msimlaumu muulizeni Mpwayungu Village
 
Ni mlevi? Tuanzie hapo.
 
Ndio, anakunywa pombe
Mara nyingi, watu wanaokunywa pombe kupita kiasi, wanakuwa hawana maendeleo. Hii inatokana na ukweli kuwa, mtu akilewa, hawezi kujiongoza (control himself/herself).

Akifikia hatua hiyo (ya kulewa), atatumia hela hovyo, hata kwa matumizi yasiyohitajika; ikiwa ni pamoja na kuwanunulia watu pombe bila staha, kutongoza wanawake, kula bila mpangilio (kuchoma nyama), nk.

Tumia njia yoyote unayoona inafaa, kumfanya apunguze au aache kabisa kunywa pombe. Waone wataamu wa saikolojia, wampe ushauri nasaha juu ya suala zima la yeye (muhusika) kujitambua kuwa yeye ndiye kichwa cha familia.

Ikiwa mbinu hii ya ushauri nasaha imeshindikana, basi, itumike njia ya kumsaidia kudhibiti kipato chake kwa kulazimisha, kama mdau mmoja alivyosema hapo awali; yaani kipato chake kipitie kwa mkewe au mtu mwingine, na mhusika apewe kidogo kwa matumizi yake.

Kwa njia hii, panaweza kuwepo mabadiliko ya kimaendeleo katika familia husika.

Nina ushuhuda mmoja, unafanana sana na suala hili: Jamaa mmoja, alikuwa anafanya kazi katika moja ya migodi hapa Tanzania. Huyu jamaa naye alikuwa mlevi sana, siku akipata mshahara, haonekani nyumbani; yeye ni pombe, pombe na yeye.

Alikaa na familia yake katika nyumba ya kupanga kwa kipindi kirefu ilihali akiwa na uwezo wa kujenga nyumba yake mwenyewe. Baadae, mke wake akaona huu ni upuuzi, akaamua kulivalia njuga suala hilo.

Bahati nzuri mke wake alikuwa na umbo kubwa. Huyu mama (mkewe), zikifika siku za mwisho wa mwezi, akiona mme wake haonekani nyumbani, anajua yupo baa anakunywa pombe.

Anaanza kusaka baa moja baada ya nyingine, huku akiwasiliana na baadhi ya marafiki zake na kuwauliza endapo wamemuona mme wake kwenye baa yoyote.

Watu watakunyima chakula, lakini umbeya hawakunyimi. Kwa jinsi hii, atapigiwa simu kuwa tumemuona baa fulani. Hapo, atafika haraka kwenye baa hiyo, atamkuta anakunywa, anamyang'anya hela yote na kumgawia kidogo tu kwa yeye kuendelea kunywa pombe (kumbuka huyu mama ana umbo kubwa).

Kumbe huyu mama alikuwa na akili; akaenda akanunua kiwanja, bila kumtaarifu bwana wake. Ikawa kila mwisho wa mwezi, anatumia mbinu zilezile kufahamu anapokunywa pombe mme wake, humvamia na kuchukua hela, na akaanza kujenga nyumba katika kiwanja alichonunua.

Aliendekea kukabana ba mme wake, na kuendeleza ujenzi. Baada ya miezi kadhaa, nyumba ilikamilika, lakini hakumwambia chochote bwana wake kuhusu nyumba hiyo!

Sasa angalia maajabu ya Mungu, baada tu ya nyumba kukamilika, yule bwana alifukuzwa kazini kwa sababu za ulevi. Yule jamaa alilia sana, hasa akikumbuka hana nyumba, na ana mke na watoto. Akajiuliza, je, kodi ya nyumba ikiisha, nitaenda wapi mimi masikini, na mke wangu, na hawa watoto wetu?

Baadaye akafika nyumbani, mke wake kucheki, anamuona mme wake analia. Akamuuliza, baba John (John ni mtoto wao wa kwanza) kulikoni? Mbona hivi leo, kuna nini?

Baba John akamwambia mke wake waingie ndani, na kumueleza kila kitu kilichotokea huku akiwa analia. Akamwambia jinsi alivyochanganyikiwa kwa kufukuzwa kazi katika kipindi ambacho hakuwa na maandalizi yoyote, hasa mahali pa kuishi.

Mke wake (mama John), huku ameshikwa na huruma, ikabidi amueleze kila kitu juu ya nyumba yao mpya. Baba John hakuamini, lakini mke wake akamwambia kuwa kesho wangeenda kuiona.

Siku iliyofuata walienda kuiona nyumba, baba John hakuamini macho yake! Nyumba ni nzuri sana! Akamuuliza mke wake, hela za kujengea nyumba yote hii ulizipata wapi? Mkewe akamjibu ni zile nilizokuwa nakunyang'anya kule baa; kiasi niligawa kwa ajili ya matumizi ya chakula nyumbani, kiasi kingine kidogo nilinunua bidhaa za pale gengeni kwetu, na kiasi kilichobaki ndio nikafanya ujenzi huu!

Baba John alimwangukia miguuni mke wake na kumuomba radhi kwa mapungufu yote aliyofanya. Mke wake akamsamehe. Wakarudi nyumbani, na kujiandaa kwa ajili ya kuhamia nyumba yao mpya.

Sasa hivi Baba John na familia yake, wanaishi katika nyumba yao. Baba John anafanya vibarua vya hapa na pale, wakati huo huo akijitahidi kutafuta kazi katika makampuni mbalimbali, huku Mama John akijishughulisha na biashara ya genge.

Akina mama big up sana sana sana. Sisi wanaume (wengi wetu), hatuangalii kesho yetu, lakini ninyi wake zetu (napenda kuwaita pia ninyi ni mama zetu, maana ninyi ndio mnaoleta watu hapa duniani), mnachuwa jukumu la familia yote, ikiwa ni pamoja na kumuongoza baba wa familia. Asante sana wake zetu, Mungu awe nanyi.
 
Back
Top Bottom