sumbai
JF-Expert Member
- Jun 16, 2014
- 20,890
- 47,611
Mzeee hizi mbinu hatari ssaaana. Yani ulicheza mission atari.Mwaka 2015 nilipata simu ambayo namba ilikuwa ngeni kwangu. Niliipokea, lakini kumbe mpigaji mwenye sauti nyororo mno yanye kuvutia masikioni alikuwa kakosea namba. Basi aliniomba msamaha lakini ikabidi nilazimishe kuendeleza mazungumzo kidogo. Aliniambia kuwa ni mwanafunzi katika chuo cha sheria Lushoto.
Mara moja moja tuliendelea kuwasiliana kwa simu na kwenye WhatsApp. Kama kawaida ya hawa viumbe wa kike alikuwa haishi kuomba pesa kwaajili ya hiki na kile. Nilijitahidi kadiri niwezavyo kumsaidia. Mawasiliano haya yalidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kipindi chote hicho hatukuwahi kuonana. Mwaka 2016 nilipata safari ya kikazi Tanga. Niliona hii ndio fursa ya kuonana na huyu mrembo mwenye sauti nyororo kama ya Double E wa enzi zile za Radio Free Africa.
Nilifika Tanga siku ya Ijumaa mchana na tulikuwa tumekubaliana na huyo dada aje Tanga Jumamosi. Alifika kweli Jmosi mchana, alikuwa ni demu mzuri na hakika sauti yake ilikuwa nyororo mno. Tulipata mlo wa mchana na kisha tukaenda kupata vinywaji sehemu nyingine. Mida ya saa moja hivi aliniambia kuwa alikuja na mwenzake toka chuo lakini alikuwa kaenda kumsalimia dada yake, hivyo akaomba amuite aje. Nikampa ruksa amuite! Bahati mbaya simu ya huyu demu iliisha charge hivyo akaomba simu yangu ili ampigie. Nilimpatia akawasiliana na huyo rafiki yake alipomaliza alinirudishia lakini alisahau kufuta namba!! Baada ya nusu saa hivi huyo demu alifika.....mapigo yangu ya moyo yalienda kasi! Alikuwa ni mrembo mno kumzidi rafiki yake. Alinichangamkia kama vile ananijua sana (inaonekana yule mwenzake alikuwa akimuhadithia uhusiano wetu)!
Vinywaji na vitafunwa viliendelea mpaka mida ya saa tano usiku hivi. Wakati huo wote nilianza kuchati na huyo demu mwingine akalielewa somo. Basi mida hiyo ya saa tano, yule demu mwingine akajifanya kama anaaga arudi kwa dada yake. Nikajifanya kumuomba yule demu wangu wa mwanzo amshawishi tukalale wote hotelini, tumchukulie chumba (nilisha muomba wakati tunachati na akakubali)! Mwisho wa siku alikubali. Nikapiga simu hotelini na chumba kikapatina.
Nilimpigia mshikaji wangu mmoja tuliyekuja naye kikazi aje pale tulipo na alipofika nilimtambulisha kwao kisha nikawaomba wale wadada watangulie hotelini kwani tuna mazungumzo ya kikazi na huyu mwenzangu. Niliwaitia tax hawa mabinti ikawapeleka hotelini. Nilizuga zuga kwa nusu saa huku nikiwasiliana na yule rafiki wa demu wangu. Nilienda hotelini nikafikia kwa room ya ya huyo rafiki wa demu wangu. Hakika alikuwa ni mzuri sio tu kwa sura bali hata kitandani. Nilikaa hadi saa tisa usiku kisha ndio nikaenda kwa demu wangu. Nilimkuta kalala fofoo kutokana na ulevi hivyo sikumsumbua. Nilijipigia Morning Glory tu!
Legendi
