Jamani hii sasa ni Live Updates. Maana asubuhi nilitoka kwenda kipata supu pale Nyuki, nikapokea msg ya bwa shemeji ambaye ndo anamuoa Pendo Jumamosi. Hakua na stori anaulizia tu advance ya mpiga picha tunatakiwa kulipa sh ngapi maana mm ndo nipo kwenye hoyo kamati.
Nikamjibu then nikamwambia anatakiwa arelax so baadae tuonane tupate moja moto moja baridi, kasema poa. So mida ya saa tisa hii naonana na mshkaji mitaa ya Sinza.
Mimi nimeshafika, ni baa moja iko na mandhari poa na private, then ina vyumba vya kulala wenyeji kwa ndani. Sasa shetani kanipa Idea hapa, maana mlango wa kuingia vyumbani ni tofauti na huku garden tutakako kaa na mshikaji, sasa akili inanikataza kabisa kumuita Pendo, ila mwili sasa unanilazimisha. Dah. Ngoja tuone itakavyokua maana hii vita ya mwili na akili sijui nani atashinda.
Ila hapana. Naeza vunja ndoa za watu, bora kulekule home, au sio waungwana?. Hata kama tunakula mtu wake tusimvunjie heshima kihivyo,.
Sent using
Jamii Forums mobile app