Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,688
- 106,829
Binafsi sio mshabiki wa mpira kabisa ila 2022 mwishoni nilianza kuahabikia timu ya Yanga, nikajikuta die hard fan. Kombe la dunia lilipoanza nikawa naangalia maramoja moja, siku moja nikasearch Google ratiba ya mechi nikaangalia, baada ya muda usiku nikaingia FB nikaona Meme inayohusu mpira kutoka kwenye Fan pages za Asians nikaingia kwenye hiyo page kisha nikatoka.
Baada ya muda kidogo nikarudi Facebook nikakuta page kibao pale kwenye suggestions zinazohusu mpira kutoka nchi za asia. Kwakua Memes zilikua zinafurahisha nikawa naingia kwenye page mojamoja naangalia. The rest is history Facebook yangu ikabadirika muonekano ikawa imejaa masula ya mpira tu.
[Meme yenyewe ni hii]
[NB. Fb sipo connected na mtu yoyote I meaan sina rafiki nipo mimi tu, that's why ilibadirika na kua ina mambo ya mpira tu before ilikua ina masuala ya Movie]
Argentina walivyochukua kombe nikasachi account ya Lionel Messi nikaangalia picha alizopost Kisha nikatoka, niiliporudi tena fb nilikuta Pages kibao zinazomuhusu Messi.
Kwakua nafahamu nini kinatokea sikushangazwa na kuyaona hayo.
Kama utakua ni mtumiaji wa Mitandao ya kijamii hasa Youtube, Facebook, Instagram, WhatsApp, Tiktok nk unaweza kua ishawahi kukutokea hili tukio. Kuna wakati unaweza ukawa unafikiria kitu fulani ila ukiingia tu FB au instagram ukakiona kikiwa katika mfumo wa tangazo (Advertisement/Sponsored) pengine hata ukisachi kitu Google kile kitu ukienda Insta au FB unakuta page zinazozungumzia kitu hicho au kukiuza.
Kwa wenzetu huko ambao muda mwingi wapo connected na Internet hua hata wakiwa wanaongelea kuhusu kitu fulani wakiingia tu mitandani kile kitu wanakikuta kinatangazwa. It's like walikua wanasikilizwa na hii ipo zaidi katika vifaa vya vyenye mfumo endeshi wa Android OS.
Hapo ndipo inapoingia suala la algorithm na Machine Learning. "Algorithm" ni mfumo uliowekwa kwa ajili ya kutatua tatizo au hitaji la mtumiaji wa vifaa vya computer na Internet na kufanya mahesabu kadri ya hitaji la mtumiaji (End User).
Algorithm inakua kama mfumo fulani uliotengenezwa ili kufanya kazi fulani hatua kwa hatua kwemye software au hardware. Katika kile seju ambapo Information Technology ipo basi tambua kwamba Algorithm ipo pia.
Machine Language ni algorithm inayotumika kutengeneza (Generating) Algorithm. Kwa waliosoma mada yangu ya Artificial intelligence nilielezea mambo haya kwa urefu zaidi maana Machine Language ipo ndani ya Artificial Intelligence.
Sasa basi mitandao ya kijamia (Nitazungumzia zaidi FB maana situmii Twitter, Insta, Tiktok nk) hasa Facebook mtu anapojiunga hua ana "Accept Company's Privacy Policy" najua wengi hua hatuzisomagi hizo.
Ukizisoma sera/ policies hizo utagundua kwamba pindi unapokubali basi unakua umeruhusu Facebook kuchukua taarafia zako kama Majina yako, Group na Pages utakazojiunga, Tarehe ya kuzaliwa, Watu unaofahamiana nao, pengine hadi namba zako za simu wanazichukua nk na hili hua hatujui maana kwenye kujiungahua tunabonyeza tu Accept bila kujua ndio maana ukienda kwenye Setting>>>Imported Contact utazikuta namba zako zote ulizowahi kutumia toka ujiunge Fb.
Pia Facebook hua inauwezo wa kujua hadi Apps ulizonazo kwenye simu yako, Location yako, Aina ya simu yako, Kama upo kwenye Wi-Fi Facebook inaweza kujua hata watu walioLog In kwenye hiyo WiFi Network.
So kwa njia hizo na zingine kibao inapelekea Fb kukujua vyema ndio maana unaweza hisi kwamba wanatusoma akili zetu lakini si kweli it's just Data Collection.
Algorithm ya mitandao ya kijamii hua inapamgilia machapisho/Posts yaonekane kwako kutokana na mapendeleo yako na sio yale yaliyo mapaya. Kama kitu ni kipya na hakipo kati vile uvipendavyo hutaweza kuviona na kama kitu ni cha zamani ila unakipenda ipo silu utakutana nacho.
Zamani miaka ya 1770s dunia ilipiga hatua kubwa baada ya Industrial Revolution, nchi zilizokua na nguvu ni zile zilizokua na viwanda vingi zaidi hapo ndio Britain ilipozipiga bao nchi zingine za Europe. Baadae miaka ya 1900s dunia ikahamia kwenye Era ya Arms and Ammunition, nchi iliyokua inasiraha nzito nzito ndio iliokopeka zaidi Hapo ndio Germany,USSR, USA zikaibuka.
Sasa tupo Digital World malighafi muhimu kuliko zote kwa sasa kuliko siraha,Chuma au viwanda ni Information. Yaani taarifa muhimu kwa wakati sahihi, Kwakweli makampuni ya Teknolojia kama Google,apple Inc, Disney,Sony, Meta nk wameweza kutuweka kati. Hakuna wasiojua kutuhusu. Pengine wanatufahamu kuliko tunavyojifahamu.
Alamsiki...ningependa kuendelea ila vidole vimechoka😟
~Da'Vinci