Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Njia pekee ya kuilinda haki ni kuiacha isimame.
Akiendelea hivi,kuna siku na hao walinzi nao watahitaji walinzi wa kuwalinda.
 
Waongeze tena wafike 10 amechemka na hatumtaki! Kama mnapenda kumlinda mpeni hata kikozi kizima! Lakini pale atoke hatumtaki! Yeye haoni aibu jamani? Anaishi kwa kulindwa na wasi wasi mkubwa! Kisa nini?? Nchi utaiacha tu utaipeleka wapi? Kwa nini ukomalie vitu vitakavyokupa lawama na kuhatarisha maisha yako? Wenzako wanaishi kwa amani na furaha wewe unalindwa kama uko gerezani sasa! Kuna raha gani?? Jiuzulu urudi serikalini......au ukafundishe
 
Ngoja waje waandishi wa gazeti la uhuru watakua na audio na video zenye ushahidi kwa nini ulinzi umeongezwa kwa huyo bibi bomba.
 
Lakini ni sasa kwa huyu mdada kuongezewa ulinzi. Kwani si ndiyo amewekwa pale kitini kama mnyapara anayewakilisha na kuhakikisha serikari inalisimamia bunge badala ya bunge kuisimamia serikali? Acha serikali itumie mamilioni ya fedha kwa ajili ya wakala wake.
 
Mkuu ni suala la amri tu,hata wewe unaweza kupewa wavaa kaunda suti ikithibitika una umuhimu huo
Mkuu hilo siyo sahihi.. Kama unakumbuka wakati Rais Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Rais Mkapa na akapata vitisho, Rais Mkapa aliamuru apewe ulinzi na alipewa walinzi kutoka Polisi(CID) siyo kutoka Ikulu.
 
Kutojiamini tu
Na kutojiamini kwa ukawa ndo kunawafanya wamwogope Naibu spika na kutimua mbio kila anapoingia bungeni. Eti hao nao wanajiita MAKAMANDA alafu wanamwogopa dada Tulia ambaye kwa sifa katulia na kufuata kanuni za bunge. Hongera sana Dkt. Tulia hakika umewatuliza ukawa.
 
Mkuu hilo siyo sahihi.. Kama unakumbuka wakati Rais Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Rais Mkapa na akapata vitisho, Rais Mkapa aliamuru apewe ulinzi na alipewa walinzi kutoka Polisi(CID) siyo kutoka Ikulu.
Waziri yupo chini ya naibu spika kiprotokali,halafu uache kukariri mambo,kuamuru NS alindwe na nani ni amri tu
 
Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.. Nukuu jambo leo.

Suali_wale waliohoji sababu ya ulinzi wako sahihi..!?

Karibu mdau.!
Ukiona mtu anajilinda kiasi hicho ujue ni muovu
 
Leo katika kipindi cha magazetini Star TV nimesikia serikali imemuongezea ulinzi naibu spika hadi kufikia walinzi watano!

Kuna hatari gani dhidi yake?
Kazi aliyopewa ni ngumu ya kuhakikisha upinzani unakufa
 
Back
Top Bottom