Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Leo katika kipindi cha magazetini Star TV nimesikia serikali imemuongezea ulinzi naibu spika hadi kufikia walinzi watano!

Kuna hatari gani dhidi yake?
Atakuwa katishiwa maisha tu,tunajua hulka ya nyumbu hata kwa Makinda aliwahi kutukanwa na kutishiwa maisha
 
Nawashangaa UKAWA wanaposubiri mkono udondoke... Kwamba Magu atampiga chini huyu dada...

Yule jamaa aliyejibu swali bungeni huku akiwa bwiii/tilalila mlisema hivi hivi, alipotumbuliwa mkakimbia humu wootee...wanaohangaika sasa kumtetea (ingawa maji yameshamwagwa) ni madiwani wake...
 
Hawezi kupewa Wavaa Kaunda Suti kwani kiutaratibu yeye hayuko katika kundi la Viongozi Wakuu wa Nchi ambao wanalindwa na watu wa Usalama wa Viongozi Wakuu.. Sana sana atapewa Walinzi kutoka Kitengo cha Ulinzi cha Bunge au Walinzi wa Viongozi Mashuhuri(VIP) kutoka Idara ya Upelelezi(CID)..
Mkuu ni suala la amri tu,hata wewe unaweza kupewa wavaa kaunda suti ikithibitika una umuhimu huo
 
Ngoja ZZK aende Kigoma akaongee na wazee wake tuone kama hao walinzi watasaidia teh teh
Mkuu nakumbuka wakati wa Karamagi alivyoenda kwao tuliona jambo na moshi mweupe ulifuka..
 
Chadema........., Geita........, pale Dodoma gari ajali ileeee, kwa ufupi chadema ni wazoefu. Maana hata juzi tumeshuhudia chadema wakiungana na kushirikiana na yule mhalifu aliyemtusi rais na yeye mwenyewe kukiri na hatimaye kuhukumiwa na mahakama. Ila I hope siku zao zinahesabika maana mbinu zao zinazidi kujidhihirisha kila kukicha!! Ila kwenye maandamano sasa serikali imewadhibiti, maana nako walikuwa wanahadaa wananchi ili akiuawa mwananchi wanasema demokrasia imeminywa, ila kwa sasa wamebinywa mbinyo wa mjusi mlangoni.
IQ yko ndogo mno
 
Uchawi wa huyo mnafiki hauna nafasi ktk maisha ya mwanadamu, serikali huwa hailogwi. Ingekuwa hivyo walimu vyuoni wangerogwa sana. Pia unajua gharama ya kumchukiza amri jeshi mkuu wa nchi??? Just wait..., mtaja ona matokeo ya wale wote wanaobeza mamlaka ya Mungu!!

mawazo ya maskini Wa fikra
 
Katika nchi inayojinadi kuwa ya amani inapotokea Naibu Spika analindwa kama spika wa Afganistani ni jambo la kujiuliza sana. Na kwa nini awe naibu spika pekee anayepewa ulinzi wa aina hiyo? Ana maadui gani hasa kiongozi huyu wa chombo cha wananchi?
Kwa maana halisi ya kazi yake adui yake alipaswa kuwa serikali na sio wananchi maana anaongoza chombo kinachoisinamia serikali. Jee serikali inamuwinda wakati ndiyo iliyomuweka nafasi hiyo? Hapana.
Hii ni mara ya kwanza kiongozi wa bunge kuwa adui wa wabunge na wananchi, ndio tunapoona madhara ya kuwa na spika au naibu wake mteule wa Rais (serikali)
Tayari huo ni uhasama.
 
Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.. Nukuu jambo leo.

Suali wale waliohoji sababu wako sahihi? Na hofu ya nini ilhali yeye sio aliyewasilisha bajeti hiyo.

Karibu mdau

Masuala ya ulinzi waacheni wenyewe professionals, wao ndio wanaojua ni nani apewe ulinzi na wakati gani na ulinzi wa aina gani...tatizo la baadhi yetu sisi watanzania ni kwamba tunajifanya kuwa tunajua each and everything...Masuala ya ulinzi siyo ya mchezo wako watu waliosomea masuala hayo, tuwaache wafanye kazi zao...
 
Haki tuu ndio ulikuwa ulinzi wa Tulia na angejikuta anaweza kwenda hata supermarket peke yake kwa raga zake ila tabia zake zimemnyima Uhuru. Unadhani mumewe na wanae wanaposikia hilo wanapata amani? Mwisho ataonba nao walindwe shuleni na nyumbani kwani mwenye kutaka kumtenda baya anaweza kwenda hata kwa hao ili kumuumiza tuu
 
Katika nchi inayojinadi kuwa ya amani inapotokea Naibu Spika analindwa kama spika wa Afganistani ni jambo la kujiuliza sana. Na kwa nini awe naibu spika pekee anayepewa ulinzi wa aina hiyo? Ana maadui gani hasa kiongozi huyu wa chombo cha wananchi?
Kwa maana halisi ya kazi yake adui yake alipaswa kuwa serikali na sio wananchi maana anaongoza chombo kinachoisinamia serikali. Jee serikali inamuwinda wakati ndiyo iliyomuweka nafasi hiyo? Hapana.
Hii ni mara ya kwanza kiongozi wa bunge kuwa adui wa wabunge na wananchi, ndio tunapoona madhara ya kuwa na spika au naibu wake mteule wa Rais (serikali)
Tayari huo ni uhasama.
Mkuu umenena, Kiongozi wa Bunge ambalo ni chombo cha uwakilishi wa wananchi atakuwa na maadui gani kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi bungeni? Ukitenda haki utachukiwa? maana chuki ndiyo huleta adui.
 
Labda itakuwa ni maandalizi tu ya kuwa full Spika baada ya kuhitimu mafunzo akiwa NS.
Lini alijiunga na NS? Na mafunzo kahitimu lini? You seem to have full details eh!!! Tujuze basi JF ni Jukwaa Huru.
 
Mkuu umenena, Kiongozi wa Bunge ambalo ni chombo cha uwakilishi wa wananchi atakuwa na maadui gani kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi bungeni? Ukitenda haki utachukiwa? maana chuki ndiyo huleta adui.
Na wao wanadhani kuonyesha kuwa NS anapewa ulinzi kuelekea kujadili budget ni jambo la sifa kumbe ni kuonyesha wananchi kuwa analindwa ili apate kulazimisha mambo ya serikali yaende bila kukwama. Napata mashaka hata ugonjwa wa Ndugai kuwa kuna namna.
Hili sasa sio bunge la wananchi tena bali la serikali, na wabunge walio wengi (ccm) wametusaliti au wamekuwa kondoo mno na hawatufai kabisa
 
Lini alijiunga na NS? Na mafunzo kahitimu lini? You seem to have full details eh!!! Tujuze basi JF ni Jukwaa Huru.
NS = Naibu Spika kama sikosei kwani wewe unadhani National Security? Soma, tafakari, comment. Thanks Masatujr.
 
NS = Naibu Spika kama sikosei kwani wewe unadhani National Security? Soma, tafakari, comment. Thanks Masatujr.
Thank you niah. Nilipata hamasa ya kuuliza hivi baada ya kuisoma comment nikaona kama issue ya kuhitimu mafunzo imekaa ki NS kwa maana ile nloisema mwanzo. Kumbe ni mafunzo ya Unaibu-Spika tehe teh teh. Kwa kweli reading doesn't necessarily mean comprehending.
 
Hawezi kupewa Wavaa Kaunda Suti kwani kiutaratibu yeye hayuko katika kundi la Viongozi Wakuu wa Nchi ambao wanalindwa na watu wa Usalama wa Viongozi Wakuu.. Sana sana atapewa Walinzi kutoka Kitengo cha Ulinzi cha Bunge au Walinzi wa Viongozi Mashuhuri(VIP) kutoka Idara ya Upelelezi(CID)..
Mh mbona yuko nao kila siku.

Ulinzi unaoongezwa ndio huo wa CID.

Hivi naibu spika ni mwepesi kumbe???
 
Back
Top Bottom