Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Hata akipewa brigade nzima hawezi pata amani. Amani ya kweli hutoka moyoni. Na hupatikana kutokana na matendo yako mema kwa jamii inayokuzunguka. Ajirudi tu ili apate amani ya kweli. Afanye kazi kwa weledi na kanuni bila kuongozwa na maagizo kutoka juu.
 
wana wasiwasi sana mbona watu hawana time nae, wanataka kusema ina maana hakutani na wenzako wakabadilishana mawazo, hamna mtu mwenye time nae, awe na amani tu
 
Naibu Spika wa bunge, dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa dk Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.. Nukuu jambo leo.

Suali wale waliohoji sababu wako sahihi? Na hofu ya nini ilhali yeye sio aliyewasilisha bajeti hiyo.

Karibu mdau
Adui wa ccm ni mwanaccm , ccm hawaachiani hata maji ya kunywa mezani - Jakaya Kikwete .
 
Nawashangaa UKAWA wanaposubiri mkono udondoke... Kwamba Magu atampiga chini huyu dada...
 
Wamlinde pia during the last safar to pagak maana mungu ndo mlinzi kwa viumbe wake sisi binadamu ni mbwembwe tu mungu akipanga uende utaenda tu ila sio mbaya maana lengo ni kuminya people's will.
 
Ulinzi pekee unaoweza kuutoa kwa binadamu wako dhidi ya binadamu wengine ni kitu kinaitwa HAKI. Ukitenda haki, utatembea ukiwa huru kabisa, jiulize majambazi wanaweza kuvamia kituo cha polisi wakaua polisi zaidi ya ya saba, na kuchukua silaha zaidi ya kumi. Jiulize pia majambazi wanaweza kuingia benki na mabomu ya kurusha kwa mkono, silaha za kivita, redio za polisi, wakafunga mtaa kwa muda mwisho wa siku wakajikuta wamechukua milion 50 tu na effort zote hizo.

Ndo maana duniani kuna dini, tukiamin kuna MUNGU anayeogopwa, na pia kuna siasa zinazoshape mind za watu, (japokuwa za kwetu ziko kichuki zaidi) nachotaka kusema ni kwamba huwezi kumzuia binadamu mwenye nia flani, unachoweza kufanya ni kutenda HAKI, na onesha kuwa unatenda HAKI.
 
Ngoja ZZK aende Kigoma akaongee na wazee wake tuone kama hao walinzi watasaidia teh teh
Unanikumbusha maneno kwenye ile speech ya mbagala kama umeiskiliza anasema alishindwa mwalim,yeye ataweza ? watu:"hawezi" ,zitto:Hatoweza. Haya mambo ndo yananichelewesha kuingia kwenye siasa. Na ww kaseme hivi uone invisible powers zitakavyo operate on you while alone. Hii kwenye surface inaonekana mivutano ya kawaida underground inaweza ikawa zaidi,hasa hili la posho.
 
Chadema........., Geita........, pale Dodoma gari ajali ileeee, kwa ufupi chadema ni wazoefu. Maana hata juzi tumeshuhudia chadema wakiungana na kushirikiana na yule mhalifu aliyemtusi rais na yeye mwenyewe kukiri na hatimaye kuhukumiwa na mahakama. Ila I hope siku zao zinahesabika maana mbinu zao zinazidi kujidhihirisha kila kukicha!! Ila kwenye maandamano sasa serikali imewadhibiti, maana nako walikuwa wanahadaa wananchi ili akiuawa mwananchi wanasema demokrasia imeminywa, ila kwa sasa wamebinywa mbinyo wa mjusi mlangoni.
 
Unanikumbusha maneno kwenye ile speech ya mbagala kama umeiskiliza anasema alishindwa mwalim,yeye ataweza ? watu:"hawezi" ,zitto:Hatoweza. Haya mambo ndo yananichelewesha kuingia kwenye siasa. Na ww kaseme hivi uone invisible powers zitakavyo operate on you while alone. Hii kwenye surface inaonekana mivutano ya kawaida underground inaweza ikawa zaidi,hasa hili la posho.
Uchawi wa huyo mnafiki hauna nafasi ktk maisha ya mwanadamu, serikali huwa hailogwi. Ingekuwa hivyo walimu vyuoni wangerogwa sana. Pia unajua gharama ya kumchukiza amri jeshi mkuu wa nchi??? Just wait..., mtaja ona matokeo ya wale wote wanaobeza mamlaka ya Mungu!!
 
Ngoja ZZK aende Kigoma akaongee na wazee wake tuone kama hao walinzi watasaidia teh teh
Atakufa yeye, maana sasa kinchofanya kazi ktk anga la Tz siyo uchawi, bali Mungu karuhusu nguvu zake zitumike kuliongoza taifa.
 
Unanikumbusha maneno kwenye ile speech ya mbagala kama umeiskiliza anasema alishindwa mwalim,yeye ataweza ? watu:"hawezi" ,zitto:Hatoweza. Haya mambo ndo yananichelewesha kuingia kwenye siasa. Na ww kaseme hivi uone invisible powers zitakavyo operate on you while alone. Hii kwenye surface inaonekana mivutano ya kawaida underground inaweza ikawa zaidi,hasa hili la posho.
teh teh teh teh kilichomtokea Mwl Kigoma anakijua mwenyewe... Wasiombe ZZK aende kushtaki kwa babu zake Kigoma..
 
Back
Top Bottom