Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.. Nukuu jambo leo.

Suali_wale waliohoji sababu ya ulinzi wako sahihi..!?

Karibu mdau.!
 
Leo katika kipindi cha magazetini Star TV nimesikia serikali imemuongezea ulinzi naibu spika hadi kufikia walinzi watano!

Kuna hatari gani dhidi yake?
 
Inaweza kuwa minyapara, mafisadi waliyopo CCM wakishirikiana na wale wa CHADEMA inamnyemeleaa
 
Naibu Spika anaweza kupewa Ulinzi wa ziada kwa muda kama atakuwa ametoa malalamiko Polisi. Zaidi ya hayo hakuna Taasisi isipokuwa Rais inayoweza kumwongezea ulinzi(kwa utashi) bila malalamiko au viashiria vya hatari kwa Usalama wake.
Kama jambo hili limefanywa kwa utashi tu basi ujue kuna mambo yanapangwa kufanywa ambayo yanalenga kuwakandamiza kwa makusudi watu fulani..
 
Labda itakuwa ni maandalizi tu ya kuwa full Spika baada ya kuhitimu mafunzo akiwa NS.
 
Kapewa makomandoo au wavaa kaunda suti?
Hawezi kupewa Wavaa Kaunda Suti kwani kiutaratibu yeye hayuko katika kundi la Viongozi Wakuu wa Nchi ambao wanalindwa na watu wa Usalama wa Viongozi Wakuu.. Sana sana atapewa Walinzi kutoka Kitengo cha Ulinzi cha Bunge au Walinzi wa Viongozi Mashuhuri(VIP) kutoka Idara ya Upelelezi(CID)..
 
Back
Top Bottom