Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

Tulisema Hii dhambi itakusumbua sana Tulia! Ukatili umekuzidi jaribu kuwa mpole na mstaarabu kiburi hata Mungu alikilaani! Ulinzi wa nini sasa?
 
Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.. Nukuu jambo leo.

Suali wale waliohoji sababu wako sahihi? Na hofu ya nini ilhali yeye sio aliyewasilisha bajeti hiyo.

Karibu mdau
Eti serikali imemuongezea ulinzi???,nilijua bunge ni muhimili unaojitegemea...basi Wale wanaosema naibu spika anaongoza bunge kwa maelekezo ya Magogoni wapo sawa.
 
UWANJANI mpirani kulikuwa na Mikidadi Mahmoud,Ahmed Jongo,Swedi Mwinyi.Chaguo la msikilizaji walikuwepo Elycia Isabula,Alicia Maneno.Michezo,Abdallah Majura,Ahmed Kipozi.....
 
Chadema........., Geita........, pale Dodoma gari ajali ileeee, kwa ufupi chadema ni wazoefu. Maana hata juzi tumeshuhudia chadema wakiungana na kushirikiana na yule mhalifu aliyemtusi rais na yeye mwenyewe kukiri na hatimaye kuhukumiwa na mahakama. Ila I hope siku zao zinahesabika maana mbinu zao zinazidi kujidhihirisha kila kukicha!! Ila kwenye maandamano sasa serikali imewadhibiti, maana nako walikuwa wanahadaa wananchi ili akiuawa mwananchi wanasema demokrasia imeminywa, ila kwa sasa wamebinywa mbinyo wa mjusi mlangoni.
Unachoshangilia ni katiba kukanyagwa? Mkuu wa polisi kuzuia mikutano, ya vyama siasa, nchi nzima? Hoja zimeisha mnagemea polisi ivunje katiba?
 
Uchawi wa huyo mnafiki hauna nafasi ktk maisha ya mwanadamu, serikali huwa hailogwi. Ingekuwa hivyo walimu vyuoni wangerogwa sana. Pia unajua gharama ya kumchukiza amri jeshi mkuu wa nchi??? Just wait..., mtaja ona matokeo ya wale wote wanaobeza mamlaka ya Mungu!!
Ndio maana ni washangiliaji wenye bidii
 
Labda itakuwa ni maandalizi tu ya kuwa full Spika baada ya kuhitimu mafunzo akiwa NS.
wachamalizana na hali ya Spika Ndugai ....ambaye wabunge walilazimisha lazima awe spika wakati ....watu wake walitaka toka awali spika awe Tulia ..
Huyu dada kichwa kitamponza sana ....kinakuwa kikubwa na karibu kitapasuka .....wangenge wa upinzani hawawezi kumdhuru .....ccm ndio wanazijua fitna ....zaidi ni ulinzi juu ya wananchi ambao sana sana wanaweza kumpiga mawe barabarani
 
hili la ma-lecturers kurogwa sijui ? Ila nasihi bongo watu wengi ni washirikana, ndo maana utasikia mtu anakuambia huniwezi nmeaga nyumbani, kuhusu kurogwa kwa serikali pia sijui, ila kuna baadhi ya viongozi wamekiri kufanyiwa mambo ya kimila.

Hivi yule mbunge aliyeonekana bungeni akitanya kitu kama unga ilikuwa ni ushirikiana au shambulio la kikemikali?
 
Unajua hawa wakosa posho hawapendi kukaa nje nao wanataka wachangie bunge la bajeti ili waweze kufafanua swala la bajeti hewa. Hawa wakosa posho huwa wanapata taabu sana pale unapofika muda wa kunyanyuka kutoka nje. Kuondokana na hii adha ni kuiteteresha afya ya huyu mwanamke wa shoka. Hivyo hawashindwi kuja na mnywa viroba au kumpenyeza mnywa viroba kama mgeni aliyeenda kujifunza uendeshaji wa bunge ambaye atafanya hila hata kwa kumkanyaga na kuathiri mwili kwa kiwango cha kushindwa kutembea na kukaa kwa muda mrefu. Ikitokea hivyo utakuwa wokovu kwa hawa wakaanje
 
Ulinzi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] najua ulinzi ni kutenda haki tu
 
Leo katika kipindi cha magazetini Star TV nimesikia serikali imemuongezea ulinzi naibu spika hadi kufikia walinzi watano!

Kuna hatari gani dhidi yake?
Serikali kama imefikia hapo maana yake hatendi haki!
 
Back
Top Bottom