Ulinzi Condoms: Jeshi la Uganda lazindua kondomu za kutumiwa na wanajeshi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Uganda limezindua nembo mpya ya mipira ya kondomu ambayo inalenga kutumiwa na wanajeshi nchini humo.

Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi.

Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali, Population Services International (PSI) - Uganda na Pace Uganda.

Kwenye pakiti za kondomu hizo, pameandikwa 'Usiende Nyama kwa Nyama', kuwahamasisha wanajeshi kutumia kinga wanaposhiriki tendo la ndoa.

Mkuu wa majeshi ya ardhini Uganda Brigedia Leopold Kyanda ndiye aliyeongoza uzinduzi wa kondomu hizo ambapo alitoa wito kwa wanajeshi kuhakikisha wanajilinda na kujikinga. Ni kwa njia hiyo pekee, alisema, ndipo wanaweza kulilinda taifa.

"Iwapo mwanajeshi binafsi hatahakikisha kwamba yuko salama, basi hawezi kuilinda nchi yake na ndio maana kama jeshi tumechukua njia hii, kuhakikisha kwamba mko salama kisha muweze kuilinda nchi," alisema Brigedia Kyanda.

Mwakilishi wa Pace Uganda alisema ni kawaida kwa wanajeshi wakiwa kazini kukutana na kufanya tendo la ndoa na wanawake, na hivyo akasisitiza kwamba ni muhimu kuwalinda wake zao wanaporejea nyumbani.

Mkurugenzi wa PSI nchini Uganda Dkt Dorothy Baraba alisema kwa sasa kondomu hizo ni za wanaume pekee lakini karibuni watawashirikisha wanawake.

Alisema mpango huo umetokana na agizo la afisi ya rais na kwamba wanautekeleza kama washirika wa UPDF.

2.jpg
 
Dah...na huku tunasubiri za... Bunge...JF....CCM...CDM...tuchangamkie fursa wakati wa majaribio :p:p:p
 
Jeshi la Uganda limezindua nembo mpya ya kondomu zitakazotumiwa na wanajeshi nchini humo. Kondomu hizo zinaitwa Ulinzi, na zitasaidia kupunguza kuenea kwa Virusi vya UKIMWI. Pakiti za kondomu hizo zimeandikwa, 'Usiende Nyama kwa Nyama' zikiwahamasisha wanajeshi kutumia kinga. Swahili Times on Twitter

IMG_20181004_184141.jpeg
 
Back
Top Bottom