Hatua nne za kufuata ikiwa kondomu itapasuka wakati wa kushiriki tendo la ndoa

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Uzi muhimu Sana huu. Wengi Wanachukulia poa suala hili.

1. Ukisikia imepasuka acha Mara Moja tendo, Kuwa mtulivu na Uitafuta kondomu hiyo Iliopasuka.

Mara nyengine vipande vya mpira huo wa kondomu vinaweza salia ndani ya uke, Ingiza vidole vyako ndani yake ishike na kuitoa nje.

Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya Uke vinaweza kusababisha Saratani ya mlango wa kizazi hapo badae, hivyo basi ni muhimu kuangalia na kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.

2. Tumia Dawa za Dharula za Kuzuia Kushika Mimba iwapo hamjakubaliana Kupata Mtoto kwa wakati huo.

Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72. Zinapatikana katika maduka ya dawa.

NB: Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga uzazi.

3. Kupimwa Magonjwa ya Zinaa hususan HIV iwapo hujui hali ya Mwenzako.

Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliyo tokea.

Pia unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.

PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi vya UKIMWI ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.

NB: Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa. Unashauriwa kufanyiwa vipimo zaidi vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi 1 na baada ya miezi 6 ili kujua hali yako.

4. Chunguza Kilichotokea.

Wapenzi wengi huruka hatua hii-hayo ni makosa makubwa, kwa sababu ni hadi utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndiposa unaweza kujiweka katika tahadhari nyengine.

JIULIZE MASWALI YAFUATAYO KUPATA MAJIBU SAHIHI

1. Je, Mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu wakati wake ulikuwa umekwisha?

Iwapo hilo ni kweli unaweza kutupa paketi ulio nayo na kununua pakiti nyengine. Ziweke mbali na joto ama hata kwenye mwanga na usizibebe katika kipochi chako na usizifungue kwa kutumia mkasi ama meno.

2. Je, Mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu ulivaliwa vibaya?

Finya eneo la mbele la mpira huo ili kutoa upepo Ukishavaa kondomu hiyo wacha nafasi mbele ya mpira huo ambayo itaweka shahawa.

3. Je, Mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa kuwa ulikuwa mdogo sana?

Pima ukubwa wa uume wako wakati unaposimama, Halafu uangalie chapisho la kondomu hiyo inaukubwa gani wa kondomu unaopaswa kutumia.

4. Je, Mpira huo wa kondomu ulipasuka baada ya kuupaka mafuta?

Utumizi wa mafuta kama vile ya Olive ama mafuta ya nazi unaweza kuwa hatari kwasababu yanaweza kufanya kondomu kupasuka.

NB: Kumbuka kwamba ajali za kondomu zinaweza kumtokea mtu yeyote.
 
Umezungumzia upande wa mwanamke tu, mbona hata kwa mwanaume kuna changamoto za matumizi ya kondom, unakuta ni kubwa mno kiasi cha kuvulika na kubaki ndani ya uke wakati tendo likiendelea
 
Back
Top Bottom