Ulinisaliti Juliet

Ulinisaliti Juliet

SEHEMU YA 18

Nilikuwa na hasira, wakati huo nilikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile. Christopher alijitahidi kuniomba msamaha lakini sikujali, nikampa kamera Juliet kwa ajili ya kurekodi kila kitu kilichokuwa kikiendelea baina yangu na Christopher.

Siwashauri watu kufanya kama nilichokifanya usiku wa siku hiyo, hapa ninajaribu kuwahadithia maisha yangu ya nyuma.

Mchezo niliotaka kuufanya siku hiyo ulikuwa mbaya ambao nitakuwa nikiukumbuka katika maisha yangu yote.

Nilitaka Christopher ajute tu. Nilikuwa na uwezo mkubwa wa kuwaua lakini hilo halikuwa lengo langu.

Kwa hapa ngoja niwaambieni kitu fulani. Mtu fulani anapokufanyia kosa kubwa, kumuua si suluhisho, kama aliuumiza moyo wako, basi wewe ufanye moyo wake kuwa na majonzi milele.

Nilichokitaka kukifanya ni kuziharibu akili zao tu, niwafanye wajute katika maisha yao yote, yaani hata siku Christopher akikaa chini na kuanza kukumbuka basi kichwa chake kiwe kinamuuma, asijisikie furaha maisha yake yote.

Kama ningewaua, ilimaanisha kwamba ingekuwa mwisho wa kila kitu, kama nilivyokuwa nimeumia, kama nilivyokuwa sina raha, yote hayo nilitaka hata nao wayapate, wajisikie kama nilivyokuwa nikijisikia kipindi hicho. “Nisamehe sana Steven...” alisema huku akilia kama mtoto.

Kwa wakati huo moyo wangu ulikuwa umebadilika kabisa, sikuwa Steven yule niliyekuwa na huruma, nilikuwa kama mwanajeshi wa Jeshi la NAZI huku nikiongozwa na kiongozi mwenye roho mbaya, Adolf Hitler.

“Kipenzi, njoo uchukue hii simu, huu ni muda wa show time,” nilimwambia Juliet ambaye akaja na kuchukua simu yangu.

“Hakikisha haunichukui usoni, ukinichukua usoni hata kama kwa bahati mbaya, nakuua. Hakikisha unarekodi kama mpiga picha mkuu, yaani uchukue sura yake vizuri, ninapomfanyia kazi na mambo mengine, umesikia?” nilimuuliza Juliet.
“Nim..es..iki..a,” alisema Juliet huku akitetemeka.
Qumanina zao mkule kiboga huyo jamaa na Juliet umle pia
 
SEHEMU YA 17

Niligonga kwa sekunde kadhaa, mlango ukafunguliwa, macho yangu yakagongana na macho ya Christopher, alishtuka sana na kutaka kufunga mlango ila nikauzuia na kumsukumia ndani.

Macho yangu yakatua kwa Juliet, alikuwa mtupu kitandani, aliponiona, alishtuka mno, akajifunika shuka. Hata kabla Christopher hajafanya kitu chochote, nikatoa bastola na kumnyooshea.

“Naomba unisamehe Steven..naomba unisamehe rafiki yangu,” aliniambia Christopher huku akipiga magoti.
“Nisamehe mume wangu,” aliniambia Juliet.

Nikabaki kimya, machozi yalikuwa yakinitoka, hasira zikanipanda, nikauma meno kwa hasira. Nikajisikia kuuaua tu wakati huo. Nikachukua simu yangu na kuwapiga picha mfululizo pale kitandani.

“Nitawasamehe? Naanzaje kuwasamehe? Yaani wewe Chriss ni rafiki yangu wa damu, ulikuwa bestman wangu kwenye harusi yangu, halafu nikusamehe! Nikusamehe kutembea na mke wangu?” niliuliza huku nikionekana kuwa na hasira mno.

“Nisamehe mume wangu....naomba unisamehe...” aliniambia mke wangu Juliet huku akitembea kwa magoti kunifuata, aliponikaribia nikampiga teke moja kali la mbavuni, akaangukia pembeni na kuanza kulia kama mtoto mdogo.

“Wewe malaya hebu nyamaza! Nikisikia unalia, nitakachoacha humu ndani ni ubongo wako kumwagika sakafuni,” nilimwambia Juliet kwa hasira, na kwa jinsi nilivyoonekana muda huo, alijua kabisa nilimaanisha kile nilichokisema.
Christopher hakuzungumza kitu, alikuwa kimya huku akiwa amepiga magoti.

Alinijua ninapokuwa na hasira nakuwaje, ninaweza kufanya jambo lolote lile bila kujali chochote. Kwa jinsi nilivyomuona, alijua kabisa muda wowote ule ningebonyeza kitufe cha bastola na kuwamaliza wote wawili.

“Christopher ni lazima uigize filamu ya ngono na mimi, Juliet utakuwa mpiga picha wetu, tukimaliza, picha nazipeleka magazetini na mitandaoni,” niliwaambia na kufunga mlango, ufunguo nikauweka mfukoni, nikatoa simu yangu na kuwasha kamera.
“Mkikataa, nawaua wote,” niliwaambia huku nikionekana kuwa na hasira.

Huo ndiyo uamuzi ambao niliamua kuuchukua, Christopher aliona raha kutembea na mke wangu, na mimi nilihitaji kumuonyeshea ni madhara gani yanatokea unapokamatwa na huyo mke wa mtu.


Kweli mke wa mtu sumu... jamaa anataka kulipiza...


Cc: mahondaw
 
SHEMU YA 12

“Ninakupenda sana Steven,” aliniambia kipindi alichokuja ofisini mwangu.
“Samahani Upendo niite bosi,” nilimwambia huku sauti yangu ikitoka kwa kumaanisha sana.

Upendo alinisumbua sana lakini nilikuwa na msiamamo mkali, sikutarajia kumsaliti mke wangu maishani mwangu, na kama ingetokea hivyo isingekuwa kwa mfanyakazi wangu, ambaye anaishi kwa fedha zangu, anabadilisha nguo na kununulia magari kwa fedha zangu.
“Siweza kudate nawe,” nilimwambia Upendo.

Hakukoma, aliendelea kunifuatiia zaidi na zaidi lakini msimamo wangu ulikuwa uleule, sikutaka kudate naye.

Siku hiyo nilipoingia ofisini huku nikiwa na majonzi, kwa kuniangalia tu, aligundua kwamba nyumbani kwangu kilikuwa kimenuka, hivyo aliitaka nafasi hiyo kwa kisingizio cha kunipa furaha.

Nilipokaa kitini, akapiga hodi na kuingia, bado sikuonekana kuwa na furaha kabisa. Akapiga hatua na kusogea kule nilipokuwa, akanishika begani.
“Kuna nini bosi?” aliniuliza.
“Hakuna kitu.”

“Hapana. Haiwezekani. Huwa haupo hivyo. Wifi kakukorofisha nini?” aliniuliza huku akionekana kunionea huruma.
“Kawaida tu Upendo. Naombe ukaendelee na kazi.”

“Bosi, nitaendelea vipi na kazi na wakati upo katika hali hii? Siwezi, nakosa amani moyoni kukuona hauna furaha,” aliniambia kwa sauti yake nyembamba.
“Kaendeleea na kazi Upendo,” nilimwambia, kidogo nikatoa sauti yenye ukali.

Akaonekana kuogopa, akaanza kuondoka ofisini mwangu. Kumkataa Upendo ulihitajika moyo wa chuma, alikuwa msichana anayevutia sana, kwa nyuma alikua amejazia halafu siku hiyo sketi yake aliyokuwa ameivaa iliishia magotini huku kukiwa na mpasuo mdogo wa kizushi, nilipouona upaja wake, matemate yakanitoka na kujilaumu kwa kumuumiza mtoto huyu.

Kuna mambo mengi nilijifunza kwamba inawezekana mtu hataki kuchepuka ila kutokana na maisha yanayomzuka nyumbani, anajikuta akiwa amechepuka.

Toka nimuoe Juliet, sikutarajia kama kuna siku ningekuja kuchepuka nje lakini kwa kile kilichokuwa kikiendelea cha kunisaliti, niliona kwamba huo ndiyo ulikuwa muda pekee wa uchepuka.
“Lakini nina mtoto, nitaweza vipi kuchepuka? Kweli nimuumize Juliet? Haiwekani,” nilijiambia.
Dawa ya moto ni moto
 
Mimi sintosahau demu niliyempenda alipewa mimba na mtu mwngne mpk Leo sipendi wanawake
 
SEHEMU YA 23

“Nimekumisi pia, nakuja.”
Siku hiyo sikutaka kurudi nyumbani mapema, nilichokifanya ni kuunganisha mpaka baa ambapo nikaagiza kleti moja ya pombe na kuwaita warembo waje kunywa tani yao huku mziki mkubwa ukisikika.

“Kunyweni mpaka muache, mkichoka, niambieni niwaongezee,” niliwaambia wanawake wale.

“Asante sana, wewe ndiye mtu saa achana na wale wazee wenye mikono ya birika,” aliniambia msichana mmoja na kuanza kunywa, walikuwa kama watano hivi.

Unywaji wao ulikuwa ni wa harakaharaka, kila walipomaliza kreti moja, niliagiza nyingine, nilitaka wanywe tu mpaka wachanganyikiwe.

“Hahah! Kwa hiyo baby tukuite nani sasa manake hii ofa ni funga mwaka,” aliniuliza msichana mmoja kwa sauti ya kilevi, alikuwa amelewa mno.

“Niite Pedeshee Steve au Papaa Steve,” nilimwambia msichana yule.

“Hivi unafanya kazi wapi?” aliuliza msichana mwingine, naye alikuwa amelewa tu.

“Mimi ni Mkurugenzi hapo TRA. Hebu kunyweni kwanza, maswali mengine baadaye,” niliwaambia na kuagiza kreti nyingine.

Usiku huo ilikuwa ni kunywa tu. Sikuwa mlevi wa pombe, nilichokuwa nikinywa ilikuwa ni soda tu. Wanawake wale nisiowajua walikuwa wakipiga kelele kila wakati kiasi kwamba ikaonekana kama fujo pale tulipokuwa tumekaa.

Utulivu wao haukuwa mkubwa kabisa, kila wakati walikuwa wakinishikashika maeneo ya zipu huku wengine wakitaka kuifungua na kuana mchezo wao, nilikuwa makini sana.

Kwa muda mwingi, Juliet alikuwa akinipigia simu lakini sikutaka kupokea kabisa, nilikuwa naiangalia simu na kisha kuichunia.

Hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu na mwisho wa siku kuamua kuipokea. Kitu cha kwanza kabisa kukisikia ilikuwa ni sauti ya wanawake wale, nahisi alichanganyikiwa.

“Upo wapi?” aliniuliza, sauti za wanawake zilikuwa zimemchanganya.
“Nipo kazini.”
“Kazini?”
“Ndiyo.”

“Mbona nasikia kelele za wanawake mpenzi na muziki?” aliniuliza, sikutaka kulijibu swali hilo, nikakata simu.
 
SEHEMU YA 24

Mwanamke, hebu jifikirie, unampigia simu mumeo arudi nyumbani, anakwambia yupo kazini, unapompigia simu saa saba, anakwambia yupo kazini lakini unasikia sauti za wanawake wakicheka, unapomuuliza, anakwambia yupo kazini, ila unapouliza kama ni kweli yupo kazini, anakata simu. Utajisikiaje? Utaweza kuvumilia na wakakati wewe ni mjauzito?

Hakika aliumia, lakini haikuwa na jinsi, alitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba nilikuwa nikilipiza kisasi bila kujua, kama alivyoniumiza, na mimi nilitaka kumuumiza.

Siku hiyo sikurudi nyumbani, nilipotoka hapo baa nikaelekea hotelini na kulala, siku iliyofuata, nikaenda ofisini na kurudi nyumbani.

“Mume wangu! Ulikuwa wapi usiku wa jana?” aliniuliza, alionekana kutia huruma, machozi yalikuwa yakimlenga.
“Nilikuwa kazini mpenzi.”
“Pole sana na kazi, nahisi zilikuwa nyingi sana.

Ila naomba unionee huruma na hali niliyokuwa nayo mpenzi,” aliniambia kwa sauti ya upole. Japokuwa nilitakiwa kumuonea huruma, wakati huo ulikuwa ni kuonyesha sura ya mbuzi tu au kuvaa miwani ya bati.

“Samahani mke wangu.”
Sikutaka kuongea sana, nilichokifanya ni kuvua nguo zangu na kuelekea bafuni kuoga.

Kesho yake, nikajiandaa na kuelekea kazini huku ile nguo niliyokuwa nimeivaa nikiacha pakti tano za kondomu, tena pakti nne zilikuwa zimetumika zote na pakti moja zilikuwa zimebaki mbili tu.
 
SEHEMU YA 25

Niliporudi nyumbani usiku, kondomu zile sikuzikuta na wakati nguo zilikuwa zimefuliwa. Nilipomwangalia, macho yake yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amelia sana.

“Kuna nini mke wangu?” nilimuuliza.
“Hakuna kitu mpenzi. Pumzika tu.”
“Hapana, siwezi kupumzika na wakati upo kwenye hai hii.”
“Naomba upumzike.”
Sawa.”

Wakati yeye akiwa na uchungu wa moyo, kwangu ilikuwa ni furaha tele. Ilipofika saa sita na nusu usiku, simu yangu ikaanza kuita, alikuwa amelala ila kwa sababu nilipanga kuipokea simu hiyo, hivyo sikutaka kulala japokuwa nami nilijifanya kulala.

Alipoisikia simu yangu inaita, akashtuka, nikaipokea na kuanza kuongea. Ilisikika sauti ya mwanamke upande wa pili, alikuwa ni Getrude, msichana aliyekuwa mfanyakazi wangu. Aliongea kwa kulalamika kwamba alikuwa amenimisi na alitaka kuniona, nilichokifanya ni kuinuka na kwenda kuoga.

Wakati nipo huko, meseji ikaingia simuni mwangu, nilisikia mlio huo na nilimpanga kwamba baada ya kuongea naye ilikuwa ni lazima atume meseji ambayo iliandikwa hivi ‘Baby, naomba uje, mwili unaniwasha, nahisi kuna vijidudu vinanitembelea mwilini.

Njoo uupoze moyo wangu kama jana na juzi ulivyonikuna vilivyo. Achana na huyo mjauzito, hawezi kukuridhisha, njoo kwangu nikupe mahaba motomoto mpaka uchanganyikiwe na kuona kwamba watoto wa kitanga tunayajua mapenzi. Kama unanipenda zaidi ya mke wako, njoo, ila kama mke wako ni zaidi yangu, usije’.
Nilipomaliza kuoga, nikarudi chumbani.

Alikuwa akilia sana kwani aliusoma huo ujumbe, nikajifanya kutokujali na wala sikumuuliza kulikuwa na nini, nikavaa na kuondoka zangu huku nikimuacha akilia kama mtoto.
Nilichokuwa nikitaka ni kumuumiza tu.
*
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
Back
Top Bottom