SEHEMU YA 17
Niligonga kwa sekunde kadhaa, mlango ukafunguliwa, macho yangu yakagongana na macho ya Christopher, alishtuka sana na kutaka kufunga mlango ila nikauzuia na kumsukumia ndani.
Macho yangu yakatua kwa Juliet, alikuwa mtupu kitandani, aliponiona, alishtuka mno, akajifunika shuka. Hata kabla Christopher hajafanya kitu chochote, nikatoa bastola na kumnyooshea.
“Naomba unisamehe Steven..naomba unisamehe rafiki yangu,” aliniambia Christopher huku akipiga magoti.
“Nisamehe mume wangu,” aliniambia Juliet.
Nikabaki kimya, machozi yalikuwa yakinitoka, hasira zikanipanda, nikauma meno kwa hasira. Nikajisikia kuuaua tu wakati huo. Nikachukua simu yangu na kuwapiga picha mfululizo pale kitandani.
“Nitawasamehe? Naanzaje kuwasamehe? Yaani wewe Chriss ni rafiki yangu wa damu, ulikuwa bestman wangu kwenye harusi yangu, halafu nikusamehe! Nikusamehe kutembea na mke wangu?” niliuliza huku nikionekana kuwa na hasira mno.
“Nisamehe mume wangu....naomba unisamehe...” aliniambia mke wangu Juliet huku akitembea kwa magoti kunifuata, aliponikaribia nikampiga teke moja kali la mbavuni, akaangukia pembeni na kuanza kulia kama mtoto mdogo.
“Wewe malaya hebu nyamaza! Nikisikia unalia, nitakachoacha humu ndani ni ubongo wako kumwagika sakafuni,” nilimwambia Juliet kwa hasira, na kwa jinsi nilivyoonekana muda huo, alijua kabisa nilimaanisha kile nilichokisema.
Christopher hakuzungumza kitu, alikuwa kimya huku akiwa amepiga magoti.
Alinijua ninapokuwa na hasira nakuwaje, ninaweza kufanya jambo lolote lile bila kujali chochote. Kwa jinsi nilivyomuona, alijua kabisa muda wowote ule ningebonyeza kitufe cha bastola na kuwamaliza wote wawili.
“Christopher ni lazima uigize filamu ya ngono na mimi, Juliet utakuwa mpiga picha wetu, tukimaliza, picha nazipeleka magazetini na mitandaoni,” niliwaambia na kufunga mlango, ufunguo nikauweka mfukoni, nikatoa simu yangu na kuwasha kamera.
“Mkikataa, nawaua wote,” niliwaambia huku nikionekana kuwa na hasira.
Huo ndiyo uamuzi ambao niliamua kuuchukua, Christopher aliona raha kutembea na mke wangu, na mimi nilihitaji kumuonyeshea ni madhara gani yanatokea unapokamatwa na huyo mke wa mtu.