Ulinisaliti Juliet

Ulinisaliti Juliet

SEHEMU YA 20

Sikuongea kitu chochote kile, kila ndugu aliongea lake kama unilaumu. Juliet alikuwa amefika mahali hapo na kuwajaza sana ujinga kwamba nilikuwa mbaya, nilimtesa maishani mwake na hakukuwa na siku iliyomfanya kuwa na furaha, hakuifurahia ndoa hata mara moja.

Ilinishangaza sana, huo haukuwa ukweli kabisa, Juliet aliamua kuwadanganya na kunifanya nionekane mbaya kwa kila mtu. Mpaka kufika muda huo, sikuwa nimeongea neno lolote lile, nilijichukulia kama fala kitu kilichowafanya wanicharukie zaidi.

Waliotaka kunipanda kichwani walinipanda, ndugu waliotaka kunipiga masingi na kunizomea kwa upuuzi waliokuwa wakidanganywa, niliwaacha wafanye hivyo.

Kila aliyeongea, alikuwa akinilaumu, walimwamini Juliet kwa maneno yote aliyokuwa amewaambia kwamba mimi ndiye nilikuwa korofi.

“Naomba anisamehe,” niliwaambia.
Juliet akashusha pumzi, nilikuwa mpole kupita kawaida. Nadhani hata yeye mwenyewe hakuamini kwani alitegemea kwamba ningewaonyesha hata zile picha kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo.

Nilikuwa mnyenyekevu kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa siri pekee ya kumshinda adui. Baada yakikao hicho na kuomba msamaha, nikaomba niondoke na mke wangukurudi Dar es Salaam.

“Sitaki kurudi,” alisema Juliet maneno yaliyomchanganya kila mtu.
“Kwa nini?” bi Lilian aliuliza.
“Sitaki tu,” alisema Juliet.
Kila mtu akamshangaa.

****
Nahisi Juliet alihisi kwamba ningeweza kumfanyia kitu kibaya na wakati mawazo yangu hayakuwa hivyo kabisa. Alikuwa mke wangu hivyo kurudi nyumbani lilikuwa ni jukumu lake.

Kila ndugu yake aliniona mbaya lakini endapo ningewahadithia kile kilichokuwa kimetokea na kuwaonyeshea ushahidi, nadhani wangenisifia kwa ujasiri mkubwa niliokuwa nao.

Sikutaka kuwaambia kilichotokea kwani ugomvi wa ndani ya ndoa ulikuwa ni wa wanandoa tu na hivyo sikutaka kumshirikisha mtu yeyote wala kumwambia ubaya niliokuwa nikifanyiwa na mke wangu.

Kwa kuwa ndugu waliniona kama mimi kuwa mkosaji, wakata nimuombe msamaha Juliet kitu ambacho kwangu wala hakikuwa kigumu. Nikapiga magoti na kuanza kumuomba msamaha huku nikimtaka arudi nyumbani tuendelee na maisha kama kawaida.
 
SEHEMU YA 21

Pamoja na kufanya hayo yoooote, Juliet alikataa katikata kurudi nyumbani jambo liliwafanya ndugu zake kuniona mbaya kwa kuhisi kwamba vitu nilivyokuwa nimemfanyia Juliet vilikuwa vikubwa visivyosameheka.

Nilichokifanya, nikawaomba niende na mke wangu pembeni kidogo tuweze kuongea, wakaniruhusu hivyo kwenda na Juliet pembeni.

“Juliet, turudi nyumbani,” nilimwambia.
“Siwezi kurudi nyumbani Steven.”
“Kwa nini?”
“Nahofia utaniua.”

“Nikuue! Ili iweje? Kama ningetaka kukuua si ningekuua pale hotelini, hebu acha utoto, turudi nyumbani,” nilimwambia.
“Siwezi kurudi.”

“Basi sawa. Ngoja niwaonyeshee uovu wako ili wajue ni kitu gani kilitokea,” nilimwambia na kutishia kuondoka, akanivuta mkono.

“Nakuomba usifanye hivyo Steven,” aliniambia huku akianza kupiga magoti, nikamzuia.

“Kama unataka nisifanye hivi, turudi nyumbani.”
“Sawa. Nimekubali.”

Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, mimi ni mwanaume mwenye akili sana na nina hekima nahisi zaidi yako. Nilijua kwamba Juliet aliniumiza sana lakini hiyo haikuwa sababu ya kumuacha.

Moyo wangu uliumia sana na nilichokuwa nikikifikiria kwa wakati huo ni kulipa kisasi tu.
Nilitaka Juliet aumie kama nilivyoumia, nilitaka akose raha kama nilivyokosa kipindi cha nyuma.

Nisingeweza kumuumiza kama angeendelea kuwa nyumbani kwao, ili aumie, ilikuwa ni lazima arudi nyumbani na kuendelea kuishi na mimi.
“Nimekubali kurudi nyumbani,” alisema Juliet, ndugu wote wakapiga makofi.

FEBRUARI 10
Maisha yalikuwa kama zamani, nilijifanya kumpenda mno mke wangu Juliet, japokuwa kila siku alikuwa akiniomba msamaha, nilimwambia kwamba nimemsamehe lakini ukweli ni kwamba sikuwa nimemsamehe hata kidogo.

Nilijitahidi sana anione tofauti, aone kwamba kila kitu kilikuwa kimepita na maisha mapya ndiyo yaliyokuwa yameanza. Nilipokuwa nikienda kazini, nilikuwa nikimletea zawadi mbalimbali na mara kwa mara kutoka naye mitoko ya usiku kwa ajili ya kula chakula.

Juliet akaanza kujisahau kwa kuona kwamba nilikuwa nimekwishaanza kusahau kile kilichokuwa kimetokea lakini ukweli ni kwamba nilikumbuka mno, tena nilikumbuka zaidi ya alivyokuwa akikumbuka.

“Nataka twende Zanzibar mpenzi,” nilimwambia Juliet.
“Nitafurahi laaziz, twende na Magreth?”
 
SEHEMU YA 22

“Hapana. Mtoto acha abaki.”
Siku iliyofuata tukachukua ndege mpaka Zanzibar, alionekana kuwa mwenye furaha mno na tulipofika kule, tukakaa kwenye hoteli ya gharama, huko tulifanya yetu na tulikaa kwa muda wa wiki nzima na ndipo tukarudi nyumbani.

Maisha yakaonekana kubadilika, upendo wa kinafiki niliokuwa nao moyoni ulikuwa zaidi ya kile kipindi cha kwanza.

MARCH 2
“Nahitaji mtoto wa pili kipenzi,” aliniambia kwa sauti ya upole.
“Usijali kipenzi, atatafutwa tu,” nilimwambia.

Kazi haikuwa ndogo, usiku mzima tulishinda tukimtafuta mdogo wake na Magreth. Kwa kipindi hicho nilijifanya kuwa mjinga bila kujua kwamba nilikuwa na akili zangu timamu.

Usiogope kuzaa na malaya, unachotakiwa ni kuwa na mtoto wako tu bila kujali ni mwanamke gani uliyezaa naye. Unaweza ukategemea kuwa na mke aliyetulia ili uzae naye mtoto lakini matokeo yake ukaambiwa kwamba mwanamke huyo hana kizazi.

Kwangu mimi, kuzaa na Juliet ilikuwa kawaida sana, alikuwa mke wangu japokuwa nilikubaliana na ukweli kwamba alikuwa kahaba mstaafu.
Siku ziliendelea kukatika, ilipofika Julai ya tarehe 21 ndipo nilipoanza kubadilika.

Kitu cha kwanza nikaanza kuchelewa kurudi nyumbani, kila alipokuwa akiniuliza, jibu langu lilikuwa ni kwa sababu nilikuwa na kazi nyingi mno ofisini.
Kiukweli ni kwamba nikaamua tu kutembea na wanawake wengine.

Nina fedha, nina kampuni so kuhusu wasichana walikuwa wakinipapatikia sana. Kuna siku nyingine sikuwa nikilala nyumbani na kila nilipoulizwa, kama kawaida yangu kisingizio changu kikaanza kuwa kilekile, kazi zilikuwa nyingi.

Juliet aliumia sana, aliniamini kwa asilimia mia moja, alinipenda kwa mapenzi yote, kitendo cha kumwambia kwamba nilikuwa bize tena huku akiwa mjauzito, aliumia kupita kawaida.

Hilo ndilo nililokuwa nikilitaka, nilitamani aendelee kuumia maisha yake yote, sikutaka kumuonea huruma kwa sababu hata mimi nilipokuwa nikiumia, hakunipa nafasi ya kunionea huruma.

“Baby, naomba leo uwahi nyumbani,” aliniambia simuni.
“Nahisi nitawahi, kazi si nyingi ofisini,” nilimwambia.
“Sawa. Mpenzi, nimekumisi mume wangu.”
 
Yaan huyo kanisababisha mpaka siweki avatar za watu tena kuna kipindi nilikuwa naweka avatar ya mdada flani hivi irene yule mwanamke wa diamond

Kheee mwisho wa siku nakuta kaniandikia thread eti natumia avatar ya mwanamke wake
 
Muda wote Christopher alikuwa akilia, hakuamini kama ningeweza kufanya kitu kama kile Nikachukua simu yangu kutoka kwa mke wangu na kuondoka zangu huku nikiwaambia kwamba wangeweza kuendelea.

Yaani hata hukukoga, sii dudu lilikuwa na nyie...
 
Yaan huyo kanisababisha mpaka siweki avatar za watu tena kuna kipindi nilikuwa naweka avatar ya mdada flani hivi irene yule mwanamke wa diamond

Kheee mwisho wa siku nakuta kaniandikia thread eti natumia avatar ya mwanamke wake
he! Jf kuna makubwa ana lake jambo mama achana naye
 
Back
Top Bottom