SEHEMU YA 25
Niliporudi nyumbani usiku, kondomu zile sikuzikuta na wakati nguo zilikuwa zimefuliwa. Nilipomwangalia, macho yake yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amelia sana.
“Kuna nini mke wangu?” nilimuuliza.
“Hakuna kitu mpenzi. Pumzika tu.”
“Hapana, siwezi kupumzika na wakati upo kwenye hai hii.”
“Naomba upumzike.”
Sawa.”
Wakati yeye akiwa na uchungu wa moyo, kwangu ilikuwa ni furaha tele. Ilipofika saa sita na nusu usiku, simu yangu ikaanza kuita, alikuwa amelala ila kwa sababu nilipanga kuipokea simu hiyo, hivyo sikutaka kulala japokuwa nami nilijifanya kulala.
Alipoisikia simu yangu inaita, akashtuka, nikaipokea na kuanza kuongea. Ilisikika sauti ya mwanamke upande wa pili, alikuwa ni Getrude, msichana aliyekuwa mfanyakazi wangu. Aliongea kwa kulalamika kwamba alikuwa amenimisi na alitaka kuniona, nilichokifanya ni kuinuka na kwenda kuoga.
Wakati nipo huko, meseji ikaingia simuni mwangu, nilisikia mlio huo na nilimpanga kwamba baada ya kuongea naye ilikuwa ni lazima atume meseji ambayo iliandikwa hivi ‘Baby, naomba uje, mwili unaniwasha, nahisi kuna vijidudu vinanitembelea mwilini.
Njoo uupoze moyo wangu kama jana na juzi ulivyonikuna vilivyo. Achana na huyo mjauzito, hawezi kukuridhisha, njoo kwangu nikupe mahaba motomoto mpaka uchanganyikiwe na kuona kwamba watoto wa kitanga tunayajua mapenzi. Kama unanipenda zaidi ya mke wako, njoo, ila kama mke wako ni zaidi yangu, usije’.
Nilipomaliza kuoga, nikarudi chumbani.
Alikuwa akilia sana kwani aliusoma huo ujumbe, nikajifanya kutokujali na wala sikumuuliza kulikuwa na nini, nikavaa na kuondoka zangu huku nikimuacha akilia kama mtoto.
Nilichokuwa nikitaka ni kumuumiza tu.
*
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Ijumaa.