Ulinisaliti Juliet

Ulinisaliti Juliet

SEHEMU YA 15 *
*
*
“Si umesema haujui! Sasa utamwambia Mungu kwamba nilikuua kwa kuwa haukutaka kuniambia ukweli,” nilimwambia huku nikiwa na hasira, nikaikoki bastola yangu.

Kiukweli siku hiyo nilibadilika, sikuonekana kuwa na utani hata mara moja, kila nilipokuwa nikimwangalia Mchichi, hasira zilikuwa zikiongezeka. Kwa muoekano wake tu, ilionyesha kwamba kulikuwa na kitu alichokuwa akikifahamu ila hakutaka kuwa muwazi.

“Ninakuua,” nilisema kwa hasira.
“Naomba usiniue, nitakwambia ukweli,” aliniambia Mchichi huku akilia, muda huo alikuwa amepiga magoti chini.
“Niambie nini kinaendelea.”

“Shemeji anatembea na rafiki yako Chistopher.”
“Sawa, ndani hayupo, yupo wapi?”
“Ametoka, amesema kwamba anakwenda kuonana na Christopher.”

“Wapi?”
“Hakuniambia lakini nilisikia akisema Monalisa hoteli.”
“Sawasawa. Nakwenda huko. Nipe simu yako.”

Akanipa simu yake, sikutaka kuridhika, nikaenda ndani na kuchukua simu ya mfanyakazi wa ndani. Nilikuwa na jukumu moja tu kwa wakati huo, kuwaua wote wawili.

Nilikuwa na hasira sana na hakukuwa na mtu wa kunizuia kufanya kile nilichokuwa nikitaka kukifanya.
Nilipoona kwamba simu zao zote nilikuwa nazo, nikachukua gari langu na kuelekea Kinondoni katika Hoteli ya Monalisa.
Bastol yangu ilikuwa pembeni.

Kwa wakati huo, hata gari niliyokuwa nikiiendesha ilionekana kwenda taratibu sana, nilitamani ipae. Sikutumia muda mwingi sana, ndani ya dakika tano nilikuwa nje ya hoteli hiyo.
Nikateremka na kuelekea ndani.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
Hawa watu Hawa
 
Back
Top Bottom