Ulimwengu umeniendea kombo

SaveTheOthers

Member
Jan 29, 2017
99
250
Wakuu
Uchumi wangu umepolomoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana Mkuu kwa Uchumi kuporomoka. Siyo kwako tu, ni janga la wengi.

Pamoja na hilo, kuwa na la kushukuru. Una afya njema, unapumua vizuri na viungo vyako vinafanya kazi vema.

Kuna wengine pamoja na kuwa Uchumi na kudorora lakini wana hali mbaya kiafya, wana msongo wa mawazo na pengine wapo katika hatihati ya kukata roho.

Kuna Mhenga aliwahi kusema, kama unakula na kuvaa, mengine hayo ni ziada tu. Shukuru Mungu kwa hayo mawili.

Pili, kama afya yako i njema amini hata kesho utapambana na Uchumi wako utatengamaa.
 

Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,919
2,000
Wakuu
Uchumi wangu umepolomoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,

Pesa maua, muhimu uhai.

Ngoja tushirikishane experiences hapa, labda utapata faraja.

Alhamisi Donald Trump kasema mbovu ma Stock market yameanguka. Dow Jones imeanguka 274 points. Nimepoteza USD $23,000 katika masaa 18. Hizo ni kama shilingi milioni 52 za kibongo.

Na wala halijaninyima amani. Kwa sababu najipanga kuzirudisha zote na zaidi katika wiki chache zijazo.

Kwa hiyo inawezekana ukaona kwako kunaungua, kumbe kwa mwenzako kunateketea.

Kuna mtu kaambiwa ana ngoma leo, lakini anaishi kwa matumaini. Nini Uchumi?

Dow drops 274 points as Trump crisis grips Washington
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom