BM X6
JF-Expert Member
- Nov 24, 2020
- 1,360
- 4,149
Kuna jamaa leo kaniharibia siku mapema sana, Nimekutana nae kwenye Daladala tumekaa Siti moja Mimi nikiwa naelekea kazini mkononi nimeshika baadhi ya mafile na laptop,
Kosa nililofanya ni kumuuliza jamaa saa, ikawa kama vile ndio nimefungulia maongezi, baada ya kunijibu "saa mbili kasoro" akanambia "inaonekana unawahi Ofisini kijana" Nikamwambia ndio siunajua kazi za watu pengine Mungu atatubariki na sisi tumiliki Kampuni zetu
Basi yule jamaa aliniangalia halafu akatabasamu kwa kusikitika akanambia
"Kijana hadi umefikia kuajiriwa kwenye maofisi ya watu ni wazi kuwa Kuna mambo flani flani unayajua lakini nikwambie tu kwamba ukitaka kufanikiwa Sahau yale Unayoyajua"
"Ulimwengu uliolelewa sio ulimwengu ambao utafanikiwa. Jipange upya. Ulimwengu wa kweli ni zaidi ya yale uliyofundishwa. Una rasilimali nyingi kuliko kizazi chochote kabla yako, Kazi njema Konda niache mnazi hapo"
Jamaa akashukia hapo lakini amefanya niwaze siku nzima, Yani bidii zote hizi za Mimi kufanya kazi, kuamka Kila siku Asubuhi ni kazi Bure!!!