Ulikuwa wapi kabla haujaja duniani kama kiumbe hai? Umewahi kutaka kujua ulipotoka?

Kwa hiyo mkuu,ili kusherehesha mada yako ukaona kuna ulazima wa kuchomekea jina la Don Nalimison 🤣

Anyway mkuu,haya mambo yanapasua sn kichwa..hata usije tena kuendelea yashanichosha kuyajadili😁....hebu rudia Kusema kimeumana🤣
Kuna watu usipowataja hoja yako inakosa credibility kabisa. Lazima ma-legend kama Don Nalimison waandikwe ili kizazi kijacho kipate kuifahamu historia hii adhimu ya watu mashuhuri kama Don.

Au nasema uongo ndugu zangu..!?😂😂😂
 
Roho ya mtoto inapatikana muda gani baada mbegu kurutubisha yai? Hiyo roho huwa inatoka wapi?
Roho ya mwanadamu ni nini?
Roho ni pumzi na hii pumzi ndiyo ile ambayo MUNGU alimpulizia Adamu puani baada ya kumuumba.

Mtoto anapokuwa tumboni havuti pumzi bali anapozaliwa na kutoka nje ndipo anapoanza kuvuta pumzi. Hiyo pumzi ndiyo roho yake sasa inapomuingia kwa mara ya kwanza.

Na hiyo pumzi ikiondoka ndipo mtu anapokufa. Hivyo roho yako ni pumzi unayovuta na hiyo pumzi ilitoka kwa MUNGU.
 
Kwani wale kuku wanaofugwa huwa wanakuwa wapi kabla hawajatotolewa? What if binadamu tuna kauspecial fulani hivi tumejipa sababu ya high IQ ila hakapo na hatma yetu ni sawa tu na wanyama wote?
 
Wewe unazungimzia mwili.

Mtu anakufa na mwili wake uko vile vile.

Tunataka kujafili hiki kinachomfanya mtu afe ni nini kinaondoka ?

Concept zinasema ni roho hiyo,roho ni nini hatujui.

Ukizungumzia seli zipo,tena mtu alianza kama seli moja tu baadae zikajigawa akawa mtu kamili,lakini ajabuu mtu huyu anakufa akiwa na trilion of cell lakini anakufa licha ya uwingi alokuwa nao wa seli zake.

Hivyos seli za mwili au mwili haumati katika mjadala huu,kinachomata ni roho
Kwani mtoto anapozaliwa tu na kutoka tumboni mwa mama yake ni nini humtokea ?
 
Niliwahi kujiuliza ila nilipata jinu kirahisi sana, haijarishi roho ama mwili ila kiuhalisia ni sie tupo kutokana na DNA, tabia zetu zimetokana na wazee watu waliokuwa kabla yetu na mama zetu kabla ya sie kuwepo, ndo maana kila jibu au tabia utayoiona unayo, ama aibu au hasira ni imetoka sehem, either wazazi wako ama wazazi wa wazazi wako, mwili pia uko hvyohvyo,
Ukijiuliza ni bora ungezaliwa au ungekuwa mtoto wa mtu flan jibu pia linakuja "NO", Isingewezekana maana usingekuwa na akili hyo

Ko kabla hujakuewepo, hukuwepo, ata roho yako haikuwepo
 
Jibu k
Dini zote duniani zina nadharia na mafundisho tele kuhusu maisha baada ya kifo. Kila dini ninayoifahamu imelizingumzia suala la maisha ya baada ya safari ya uhai wa binadamu kufika mwisho kwa undani sana tofauti na suala la alipotoka binadamu.

Japo kuna mjadala mkali kwa mafundisho na nadharia hizo lakini hakuna ubishi kwamba zipo, hii ni tofauti sana na mafundisho kuhusu alipotoka binadamu

Sehemu kubwa ya dini ninazozijua hazizungumzii alipokuwepo binadamu fulani kabla hajazaliwa na kuanza kuishi duniani.

Je mtu huwa anakuwa wapi kabla ya kuzaliwa kwake hapa duniani?

Kwa nini binadamu wengi pia hawahangahishwi na kutaka kujua walipokuwa kabla ya kuzaliwa?
Jibu Kwa swali lako is rather simple,nitakujibu kwa rhetorical question, Unapowasha Moto kwenye mshumaa,ule moto ulikuwa wapi kabla ya kuuwasha,na moto huo huenda wapi baada ya kuuzima?
 
mara kadhaa nimekuwa najiuliza hili swali.
roho yangu kabla mimi sijazaliwa na kuwa binadamu, ilikuwa inaishi wapi. nakosa jibu. sikubaliani na hoja za wafuasi wa imani za kidini.

labda roho yangu ilikuwa sayari nyingine au pengine ilikuwa inarandaranda hapa duniani ikiwa imejihifadhi kwa wanyama kama kuku, ngo'mbe au mbwa.

kiukweli kuna siri nzito sana inayohusu uumbaji wa mwanadamu, sidhani kama yupo anayeweza kuielezea kwa usahihi akaeleweka.

labda huku tulipo(duniani), tupo gerezani kutumikia adhabu baada ya roho zetu kutenda makosa kwenye universe nyingine.

labda kifo ni portal(mlango) ya kurudisha roho zetu kwenye universe yake ya awali baada ya kumaliza kutumikia adhabu hapa duniani(gerezani).

najiuliza maswali haya kwasababu sayari tuliyopo haina usawa, ina watu wanyonge sana, watu makatili sana, watu matajiri, watu masikini, watu wenye madaraka, wasio na madaraka na kadhalika.

ni kama tupo kwenye uwanja wa vita vile.
Ina make sense.
 
Mi nafikiri binadamu hatuna tofauti na gari na kompyuta. Computer ilikuwa wapi kabla ya kutengenezwa? Gari lilikuwa wapi kabla ya kutengenezwa?

Havikuwa kitu chochote bali elements zilizoyatengeneza, Chuma nk. Hata sisi hatukuwa kitu bali Carbon, Oxygen Calcium nk
 
Lakini binadamu anao uhai na utashi tofauti na hivyo vitu vingine ambavyo yeye kavitengeneza.
Mi nafikiri binadamu hatuna tofauti na gari na kompyuta. Computer ilikuwa wapi kabla ya kutengenezwa? Gari lilikuwa wapi kabla ya kutengenezwa?

Havikuwa kitu chochote bali elements zilizoyatengeneza, Chuma nk. Hata sisi hatukuwa kitu bali Carbon, Oxygen Calcium nk
 
Dini zote duniani zina nadharia na mafundisho tele kuhusu maisha baada ya kifo. Kila dini ninayoifahamu imelizingumzia suala la maisha ya baada ya safari ya uhai wa binadamu kufika mwisho kwa undani sana tofauti na suala la alipotoka binadamu.

Japo kuna mjadala mkali kwa mafundisho na nadharia hizo lakini hakuna ubishi kwamba zipo, hii ni tofauti sana na mafundisho kuhusu alipotoka binadamu

Sehemu kubwa ya dini ninazozijua hazizungumzii alipokuwepo binadamu fulani kabla hajazaliwa na kuanza kuishi duniani.

Je mtu huwa anakuwa wapi kabla ya kuzaliwa kwake hapa duniani?

Kwa nini binadamu wengi pia hawahangahishwi na kutaka kujua walipokuwa kabla ya kuzaliwa?
We Kwani umetokea wapi ?? Ulipotokea ndipo ulipokuwa
 
Mada nzuri sana hii. Nina amini kwamba mimi (mwili na roho) nilikuwepo nipo na nitaendelea kuwepo. Hii ni kwa sababu sifikirii kama time ipo linear kwamba unatoka point moja kwenda nyingine. Ninafikiria time kwamba ni kila kitu kinatokea kwa muda mmoja.
Pia nina amini kwamba tupo kama mfano wa Mungu na hivyo tupo tulikuwepo na tutaendelea kuwepo.
 
Kwa mfano wa Mungu..

Hivyo Mungu ana mwonekano kama wetu...mikono miwili,kichwa,miguu miwili etc.
 
Back
Top Bottom