Je, Taoism ni uchawi? Je, unaweza kutumia Taoism kutabiri mambo ya mbeleni? Nitajaribu kukuelewesha

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses and roses.

Nimekua napokea maswali mengi kiasi kutokana na maandiko yangu kadhaa nioandika hapa siku za nyuma. Lakini maswali mengi yanajikita kwenye haya mawili, Je Taoism ni uchawi? Na je unaweza kutumia Taoism kutabiri yatakayotokea mbeleni?

Kabla ya kujibu hayo maswali labda nielezee Taoism ni nini kwa maneno ya kawaida kabisa.

Taoism ni Namna ya kuishi kwa kuendana na lengo la Nguvu kuu inayoendesha au iliotengeneza ulimwengu. Hivi ulishajiuliza kwamba force of gravity ingekua kubwa zaidi ya ilivyo basi nini kingetokea? kila kitu kwenye ulimwengu huu kingevutwa sehemu moja kama sumaku vile, na pia ushajiuliza kama gravity ingekua ndogo zaidi ya ilivyo kila kitu kingepepea infinitely?

Na ushawahi kusikia kuwa kiasi cha nishati (energy) hapa ulimwenguni kiko fixed? Ila tu nishati ile ile inajibadili badili? Sasa hizo facts nlizosema hapo na nyingine zote zinamaanisha kwamba duniani kuna NGUVU moja kuu ambayo ndio ilioweka na inayomaintain hio BALANCE.

Hio Nguvu kuu inajionesha kwa mambo mengi, na ndio maana ina majina mengi kutokana na watu tofauti. Wengine wataita Mungu, Wengine Allah, na kadhalika.

Kazi kuu ya Taoism ni kuhakikisha binadamu anaishi kutokana na matakwa ya hio Nguvu Kuu. Kwenye Taoism hio nguvu tunaiita "Tao" au "The Way" kwa kiingereza. Na hio Nguvu, haielezeki, wala haina jina. Ndo maana kwenye kitabu kikuu cha Taoism kinachoitwa Tao Te Ching,kuna aya inaaema ".....The Tao that can be named is not an eternal Tao....."

Sasa Taoism imekuwepo toka zamani saaaaana, na Taoism sio dini. Ni njia ya moja kwa moja ya kufikia hio Nguvu kuu, lakini dini ni kama Agent anaekupromise atakukutanisha na hio Nguvu kuu. Kwa sababu Taoism imekuwepo toka zamani basi imekutana na maboresho mengi ambapo watu baadhi hutumia mafundisho yake kufanyia mambo mbalimbali. Mfano, ulishasikia Tai Chi? Hio ni style ya kupigana kwa kutumia body balance na softness ili kumshinda adui yako, lakini imezaliwa na Taoism.

Kwa maana hio kuna watu walitumia mafundisho ya taoism kutengeneza factions za kichawi, hapa ninajibu swali la kwanza, je Taoism ni uchawi? Kiufupi taoism sio uchawi, ila mafundisho ya Taoism yanabeba mambo mengi sana ambapo ukiweza kutumia ukaapply kokote kule iwe kwenye Siasa, Biashara, Vita, Uchawi, nk nk... utapata matokeo unayotaka sababu Taoism inakuonesha Nguvu kuu inataka nini, na ukiweza kuji-align na hio Nguvu basi utapata chochote unachokitaka. Kuhusu swala la uchawi kwenye taoism, haina tofauti na mtaalam wa physics akatumia ujuzi wake kutengeneza Nuclear bomb.

Swali la pili kuhusu kutumia Taoism kutabiri mambo ya mbeleni. Hili mitalijibu kiufupi sana ili nisikuchanganye ndugu msomaji.

Hivi mfano wewe si unajua kwamba ukivuta mlango kwa nguvu na mlango ukiwa hujawa locked basi mlango utafunguka?

Sasa kwa mfano huo hapo juu, chukulia una manuals (mafundisho) yanayoelezea kila kitu au kila tendo na outcome yake. Sasa utashindwa nini kutabiri kitu gani kitatokea baada ya kitu fln kufanyika? Kama nilivyosema awali kwenye Taoism kuna mafundisho meengj sana, mengine hadi ukitumia unaweza tabiri kabisa moves za adui yako, hili linatumika hata kwenye Tai Chi, kwa masters wa Tai Chi, wao ukipigana nao anakua anajua next move yako ww ni ipi. Sasa jiulize kama Taoism imezaa Taaluma kama hio, kwa nn mafundisho yake yashindwe kukufanya ww kutabiri mambo yatakayotokea? Kuna mafundisho mengi sana kwenye Taoism, na kuna Sages wengi sana wameandika. Na nisikudanganye, sio kila mtu anaweza kufikia hio level ila nakwambia hapa uhusiano wa Taoism na utabiri wa mambo ya mbeleni

Mwisho kama unataka kuona nilichoandika hapa ni porojo au sio porojo, chukua muda, soma kitabu kinaitwa TAO TE CHING. Ni kitabu ambacho kiukweli kimebadili maisha yangu na namna ninavyoona vitu au situations mbalimbali. Ni ktabu ambacho nikiwa naona nimefail au nimekwama kabisa basi nakisoma na napata jibu nifanye nini. Ni kitabu kifupi sana, kiliandikwa kwa kichina miaka ya zamani lkn kuna tafsiri nyingi sana zipo mtandaoni.

Remember, the goal is to be a decent human being. Until next time, stay safe!

~ kali linux
 
I can agree with you.

I havent been so deep into TAOISM, lakn firsst time i knew about it n kwenye kitabu fulani kinachohusu mambo ya mapenzi.

In this book walikua wanaelezea taoist methodologies on how to have multiple orgasms bila ku ejaculate n.k. ni mambo kibao.

But waliongelea this "energy" and how to channel it in the human body kwa ajili ya kupata faida lukuki.
Good thing ni kwamba it really works, but it takes time and a lot of practice.

Taoist monks walikua na vast information on different matters and one thing i love about it n kwamba hakuna kitu chochote kinachofanania na ushirikina.

I think as human beings, tuna a very great potential but we know so little about ourselves (though kienyeji tunahisi tunajua), but ukiweza kuingia deep and unlock the secrets of the human body and mind you might be amazed at how great we are.

Wengi hatuongezi maarifa kwa kusoma vitu tofaut so we kinda live in the matrix of existence but we dont really exist.

In JF kuna watu wengi ambao wanaenda deep to gather knowledge abt different matterS, e.g Kiranga , lakini ukiangalia wengi hua wanapinga without justification maana wengi hawana knowledge.

Kongole kwako kali linux on this. I remember uzi wako about psychedellic mushrooms, that was dope too.

Tuzidi kujifunza.
 
Kwa hisani ya Google nanukuu hapa hapa mkuu "Uchawi (kwa Kiingereza "Witchcraft") ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni." Moshi wa kunukuu

Vizuri.

Unajuaje maarifa haya ni ya kisayansi na haya si ya kisayansi?

Hususan kwenye vitu ambavyo huvijui kabisa na ni mara yako ya kwanza kuviona.

Nakupa mfano.

Mimi nilivyokuwa mtoto mdogo, nilikuwa nina rafiki yangu mmoja mkubwa kwangu. Yeye alijua kuwa gari kabla ya kukata kona inawasha indicator. Mimi sikujua.

Basi tukafanya mchezo. Kila gari ikija, tunaotea kama itakata kulia, kushoto au itaenda mbele bila kukata.

Yule jamaa alikuwa anaanza kuotea yeye. Kila akiotea alikuwa anapatia. Akasema ana uchawi wa kujua kuotea gari litakwenda wapi. Bado kidogo nimuamini. Akaniambia unaiona ile taa? Basi ile taa ndiyo inakuonesha gari linaenda wapi.

Sasa hapo, kabla sijajua kuwa kuna taa inaonesha gari linaenda wapi, kama naamini uchawi, si ningeweza kuamini huyu jamaa mchawi tu, anaweza kuotea gari linaenda wapi na likaenda huko huko.

Unaona hapo kitu usichokijua kinavyoweza kukufanya ukubali uchawi, sehemu ambayo haina uchawi kabisa?
 
Hello bosses and roses...

Nimekua napokea maswali mengi kiasi kutokana na maandiko yangu kadhaa nioandika hapa siku za nyuma. Lakini maswali mengi yanajikita kwenye haya mawili,...
It's nothing new, hata sisi hapa kwetu hapa Afrika tuna imani zetu ambazo ni kongwe zaidi ya Taoism na hizi dini za kuletewa ila tumechanganywa akili na wazungu na Waarab kwa kuletewa dini zisizo na mashiko maishani mwetu na kuacha imani yetu ambayo ndiyo our true identity.

Kufuata hizi dini za watu ni kuasi imani na mila yako kushadadia imani na mila za wengine kama ilvyo hapa Tanzania. Unakuta mtu hajuwi chochote kuhusu historia ya Mwarab lakini anajifanya Mwarab na kuona sifa, huu ni ujinga uliotukuka. Tumekuwa watumwa wa dini wakati hatuelewi lolote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom