Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,556
- 46,095
Dini zote duniani zina nadharia na mafundisho tele kuhusu maisha baada ya kifo. Kila dini ninayoifahamu imelizingumzia suala la maisha ya baada ya safari ya uhai wa binadamu kufika mwisho kwa undani sana tofauti na suala la alipotoka binadamu.
Japo kuna mjadala mkali kwa mafundisho na nadharia hizo lakini hakuna ubishi kwamba zipo, hii ni tofauti sana na mafundisho kuhusu alipotoka binadamu
Sehemu kubwa ya dini ninazozijua hazizungumzii alipokuwepo binadamu fulani kabla hajazaliwa na kuanza kuishi duniani.
Je mtu huwa anakuwa wapi kabla ya kuzaliwa kwake hapa duniani?
Kwa nini binadamu wengi pia hawahangahishwi na kutaka kujua walipokuwa kabla ya kuzaliwa?