Ulifanya kosa gani mpaka ukapewa suspension shuleni?

Rafiki yangu alipewa suspension alikuwa akiona hamna mtu kwenye dinning hall anabeba cd yake ya x kwenda kucheki kwenye tv ya shule,

Tabia ikawa mazoea, siku akadakwa live, alipewa suspension wiki 2.
.........Alikuwa amevurugwa haswaa!!
 
Ilikuwa mwaka 2008 form four shule fulani nzega tabora , monitor wa kike alikuwa mkuda watu wanamuogopa akisema acheni kelele watu wote wanafyata , sasa siku moja sisi back bencha tukamwambia usitutanie story tunapga na hukuna kitu utafanya ,
Akaandika majina akapeleka kwa second master tukaitwa staff office tukapgwa fimbo nne kila mmoja na tukarudi class .
Sasa baada ya kurudi class tukamchimba biti yule monitor kiwa hapo amezua kesi tutamfanyia kitu mbaya , akarudi tena kwa second kumwambia tukaitwa tena ofisini kula fimbo up upya na suspension week 1 kuja uje na mzazi ilikuwa kizaa zaa jinsi ya kueleza nyumbani .....
 
Siku hiyo kulikua na wageni shuleni japo sikumbuki ni nani alikuja nikatumwa na mwalimu kupeleka mifuko ya kutunzia mahindi kwa mwalimu aliekua akiishi mbali kidogo na shule nikasingizia tumbo linauma lakini nikalazimishwa kupeleka nikajawa na hasira wakati naondoka nikawaza nifanyeje ili nimkomoe huyu mwalimu?

Kuna nyumba za walimu zilikuwa tayari zimekamilika wanajiaandaa kuhamia nikajisemea kimoyomoyo (kwa dharau nakunya kwenye hili jengo) ni moja wapo ya zile nyumba zilizo kamilika nikaingia ndani nikatafuta chumba chenye giza nikanya humo ndani nikamaliza sasa wakati najiandaa kutoka nje nikasikia sauti za watu kama wanakuja vile nikatembea harakaharaka mda huo nikiwa nafunga mkanda wakati nafika sebleni nikakutana na kundi la watu wenye vitambi na suti zao wakiwa na baadhi ya walimu wa shuleni kwetu akiwemo na yule mwalimu alienituma kumbe ni wale wageni walikuja kukagua yale majengo yaliyokamilika yule mwalimu akaniuliza unafanya nini humu ndani nikakosa majibu akanambia nisubiri hapo nje wale watu kuingia nilikotoka wakakutana na mzigo wa hatari walichoulizana sikujua tena safari ya kupeleka mifuko ikaishia hapo nikaletewa wanafunzi wanne wakubwa ili wanilinde nikawa chini ya ulinzi mpaka wageni walipoondoka mda huo nilikuwa nimefungwa mikono kwa nyuma ili nisikimbie wageni walipoondoka mda kidogo kengele ikagongwa wanafunzi wote wakawekwa assemble nikaletwa mbele ya wanafunzi woote nikasomewa mashitaka yangu mbele ya shule nzima nikashikwa miguu na mikono nikaning'inizwa nikala fimbo zisizo na idadi kisha nikaambiwa nisafishe matundu 10 ya choo peke yangu na maji yalikua ya shida kweli mm nikakaa huko chooni toka saa6 mchana mpaka saa 10 jioni bila kusafisha hata tundu1 nikamtuma rafiki yangu akaniletea daftari zangu nikapita hukohuko nikaenda nyumbani kesho yake sikwenda shule siku iliofuata nikaenda ilipofika mda nikaletwa mbele ya wanafunzi woote nikasomewa mashitaka yangu mbele ya shule nzima nikashikwa miguu na mikono nikaning'inizwa nikala fimbo zisizo na idadi kisha nikaambiwa nisafishe matundu 10 ya choo peke yangu na maji yalikua ya shida kweli mm nikakaa huko chooni hadi jion bila kufanya usafi wowote nikamtuma rafiki yangu john akaniletea bag nikaenda home kesho yake sikwenda shule after two days nikaenda nikijua wamesahau ilipofika mda wa kuingia darasani kengele ikagongwa tukafolenishwa mwalimu akaja mbele akatoa maelekezo ya kila siku aliponiona akanita nipite mbele mimi nikachomoka mbio nikafukuzwa na shule nzima aseee hizo mbio sijui nilizitoa wapi siku hiyo nilikimbia zaidi ya mwizi nipofika mbali nikaokota mawe nikaendelea kukimbia nyuma yangu waliokuwa bado wananifukuza walikua watatu nikasimama gafla mmoja aliekua mbele akanikaribia nikampiga jiwe la kichwa nikaendelea kukimbia sikuona mtu tena nyuma yangu kumbe yule niliempiga jiwe aliumia sana hadi kudondoka chini baada ya kutokwa na damu nyingi lakini sikuweza kujua kilichoendelea kwa mda huo nilienda mbali na maeneo yale nikakaa hadi mda wa kutawanyika mchana kwenda kula nikaenda nyumbani sikurudi shule mchana daaaah,

Jioni wanafunzi wenzangu ambao ni majirani wakaleta habari hadi home asubuhi nikamundishwa kupelekwa shuleni kufika shuleni walimu wakanikataa nikarudishwa nyumbani wazazi wakabembeleza lakini wapi nikakaa nyumbani wiki2 ndipo nikaruhusiwa kurudi shule hapo ilikua 2004 shule ya msingi.
Kwa member yoyote anaye kumbuka wimbo wa Mr sugu nipo mikononi mwa police nami nikiwa form1 nilikuwepo inauma sana tulimpoteza mwamba mmoja mpaka Sasa sura yake naikumbuka
 
Dah,umenikumbusha mbalii.
Nilipendwa na mtoto wa headmaster wetu,binti sijui kilimvutia nini kwangu kwakweli maana kamenisumbua sana,nimekula Chocolate balaa, biscuit naletewa Yale makopo,mpaka na msosi wa nyumbani kwao najilia kama boss.
Chakula cha shule nilikisahau kwa muda,mtoto alikolea na mimi akawa haambiwi asikii. Kulikuwa na kiongozi wa chakula anamuelewa sanaa binti,na amewekeza pocket money yake kwa binti,Ila mchuchu hajamuelewa mwamba hata kidogo.
Jamaa katuma sana zawadii, nyingine zinarudishwa lakini mwamba anakomaa tu,ikabidi jamaa aanze kuchunguza nani anamzidi kete kwa binti?
Kwenye fukunyua fukunya yake akazipata kuwa binti anamuelewa sana flanii mpaka zawadii anampelekea,na msosi wa nyumbani analetewa,weeeh!!
Balaa lilianzia hapo,ubaya sikuwa na status yoyote school,nikaanza kupewa vikesi vya ajabu ajabu, wakati huo sijashtukia mchongo kwamba kuna mtu anateseka na mimi.
Siku hiyo tulipewa kazi ya kupakua magunia ya mahindi kutoa stoo tupeleke mashineni,na nilipewa kazi ya kusimamia Ile shughuli.
Jioni nashangaa nafuatwa prepo na kiranja mkuu,unahitajika office ya mwalimu wa nidhamu. Tukaongozana,mara anauliza lile gunia uliloiba umelificha wapi,nikabaki mdomo wazi,kuiba gunia tenaa?
Kufika mwalimu akanimbia nina kesi ya wizi inanikabili,kama sitaki matatizo nihakikishe gunia linapatikana. Nikamwambia sina la kujitetea maana sijaiba,nasubiri hukumu,akang'aka balaa kumbe we kiburiii,badala uombe msamahaa unajifanya mjuaji,nikamwambia ticha sijawahi kuiba na sitarajii kuwa mwizi, kwahiyo usinilazimishe kuomba msamaha kwa jambo ambalo sijatenda,akanifukuza ofisini kwake akanimbia tutaona Kesho na ujuaji wako.
Mzuka wa kusoma ukakata,nikawaza hii imekuwajee,mimi huyuhuyuuu niibe gunia nalitoaje nje wakati shule inauzio?

HUKUMU.
Asubuhi kumekucha,ikapigwa kengele,tukakusanyika wote. Nikaitwa mbele na kusomewa hukumu yangu,kwamba mimi ni mwizi nimeiba gunia kwa kushilikiana na mpeshi,hivyo nikafurushwa wiki mbili nirudi na mzazi na mpishi akaachishwa kazi.
Kilichomkuta jamaa baada ya kujua katengeneza mchongo,hata sahau maishaa.
Ila mtoto wa headmaster sitamsahau,ilinipa ufalme kwenye milki ya Baba yake.
Nini kilimkuta jamaa alietengeneza kesi ya wizi wa gunia?
 
Kumtaka mwalimu wa HISABATI ahame alikuwa anatudanganya ,alikuwa hawez kufundisha eti mathe anataka tuandike nots. Aje kesho aelezeee ,kama upo umu nisamehe
 
Mwalimu aliuliza kati ya jiwe na Nazi vikigongana je nini kitapasuka

Kwa ujasiri Mimi nikainuka na kumjibu" jiwe litapasuka kwa sababu now days mawe ni mabovu ". Darasa lote vicheko

Ticha akavimba ......chaap nikapelekwa ofisin sper ya wiki tatu

.Tafsir.......kumbe swali sikuelewa ..alivyosema jiwe ...alimaaniesha yeye ni mwamba na sisi ni vifaranga wadogo .....so vikikutana nn kitatoke?
 
Mwalimu aliuliza kati ya jiwe na Nazi vikigongana je nini kitapasuka

Kwa ujasiri Mimi nikainuka na kumjibu" jiwe litapasuka kwa sababu now days mawe ni mabovu ". Darasa lote vicheko

Ticha akavimba ......chaap nikapelekwa ofisin sper ya wiki tatu

.Tafsir.......kumbe swali sikuelewa ..alivyosema jiwe ...alimaaniesha yeye ni mwamba na sisi ni vifaranga wadogo .....so vikikutana nn kitatoke?

Fala sana
 
Nakumbuka nilimpiga mwalimu mmoja anaitwa Kabuje pale Meta secondary ili nifukuzwe shule, mwalimu Kabuje akaamua yaishie palepale.
Kabuje mlezi wa hostel khaa wewe Mwamba? enzi hizo yule mwamba wa chemistry olevel alokuwa anatembea na Gongo (fimbo) alikuwepo? Kabuje kiswahili olvel
 
Back
Top Bottom