Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Kwanza nilikubali nimepoteza pili nikaangalia nilikosea wapi tatu nikaanza upya kwa energy mara 10 yake. Nipo tu kwenye usafiri ila nikipata nafasi nitaandika.

Now am happy alhamdulillah
Mkuu ulishashuka kwenye daladala utupe mawili matatu.
 
faida mara mbili kwa dagaa ni uongo. Labda awe anamitubwi yake mwenyewe na anauza straight kwa mlaji wa mwishi Dsm.
Lakini kama kajichomeka somewhere kwenye chain iyo ni kamba umepigwa.
Mkuu nipe projections nisijekuwa nimepigwa kamba nalisha watu matangopori. Ukinunua dagaa wabichi ukawaanika na kutoa gunia moja, utatumia kiasi gani. Na ukija Dar litauzwaje, na gharama za usafiri ni kiasi gani. Najua kuna price fluctuations ila inakuwa reflected kwa mzalishaji na kwa consumer.
 
Tunaendelea kujifunza.
Biashara ni uthubutu,imani,bidii na uvumilivu. Mungu atusaidie wapambanaji wote tusikose pesa ya kujikimu na kuhudumia wapendwa wetu.
 

Attachments

  • 208c3ea8c45b4c02b967d3771a4c6d1d.jpg
    208c3ea8c45b4c02b967d3771a4c6d1d.jpg
    52.5 KB · Views: 12
Nimeshuhudia biashara ya mtu mmoja mlokole inafanikiwa sana, sema yule mtu anatoa zaka, alafu kwenye maombi usiseme alafu anaishi maisha matakatifu sana.

Aisee 🤣 umwambie mtu aache uzinzi, anaona Bora aende upande wa pili.
Hii kweli Kaka usipokuwa na uimara kiroho lazima utaishi kwa kuwafanyia watu Kazi na faida hautaweza kuipata.
 
Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???
 
Pole mkuu, mimi ni tofauti naingia visiwani mwenyewe nakusanya napeleka mwanza kuuza mwenyewe.

Pole mkuu, mimi ni tofauti naingia visiwani mwenyewe nakusanya napeleka mwanza kuuza mwenyewe.
Kiongozi vp upande wa dagaa kutoka visiwani na kuwaleta mwanza? Hapo naulizia mtaji wa shilingi ngapi? Na sehemu ya kuuzia ukishazifikisha mwanza na ukiwa mgeni ukienda kule visiwani hamna shida au usumbufu unaoweza kukupata?
 
faida mara mbili kwa dagaa ni uongo. Labda awe anamitubwi yake mwenyewe na anauza straight kwa mlaji wa mwisho Dsm.
Lakini kama kajichomeka somewhere kwenye chain iyo ni kamba umepigwa.
Hizo stori za kusimuliwa kuwa biashara fulani inalipa sana ndio kitu huwa kinawaingiza chaka watu wengi sana,kwa mfano amesimuliwa hivyo siku akipata mtaji anaingia kichwakichwa bila kuchunguza mwisho wa siku anakula za uso.
 
Nakumbuka kuna center moja nilikamata sehemu. Kila mtu ananiambia daah hapa mwanangu umeula kwa eneo hili utapiga business mpaka uchoke. Weee..! 😀 Mbata! Mbata! Kofi! Teke! Mtamaa..! Kichwa chini miguu juu hata miezi 6 haikuisha dadek😄
Ulipakimbia? Alafu ukifungua sehemu biashara alafu Kila anaekuja anakwambia hii sehemu utapiga sana pesa, hiyo ni alarm ya kukuamsha. Mie mwenyewe Kuna mahari location iko vzr sana sasa wakati wa ufunguzi wa hiyo biashara yangu watu wengi sana walikua wakiniambia hapo nimelenga, mara hapo nitapiga sana pesa, na kauri hizi sio majirani zangu tu ni mpaka wapita njia.

Kiukweli ile siku ya kwanza nafungua hii biashara yangu nilifanya kazi sana na siku iliyofuatia nilifanya kazi sanaaaaaa but baada ya hizo siku mbili za mwanzo naona biashara imepoa ghafla. Lkn kwa aina ya biashara yangu nimejipa muda kwani ni biashara ambayo inakua taratibu(nauzoefu nayo)
 
Back
Top Bottom