Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Nakumbuka kuna center moja nilikamata sehemu. Kila mtu ananiambia daah hapa mwanangu umeula kwa eneo hili utapiga business mpaka uchoke. Weee..! 😀 Mbata! Mbata! Kofi! Teke! Mtamaa..! Kichwa chini miguu juu hata miezi 6 haikuisha dadek😄
😂 hizi biashara zina mambo mengi sana, kuna muda kuwa na mtaji sio suluhisho la kufanikiwa.
 
Nakumbuka kuna center moja nilikamata sehemu. Kila mtu ananiambia daah hapa mwanangu umeula kwa eneo hili utapiga business mpaka uchoke. Weee..! 😀 Mbata! Mbata! Kofi! Teke! Mtamaa..! Kichwa chini miguu juu hata miezi 6 haikuisha dadek😄
😀😀😀😁😁nimecheka kiboya sana
 
Tatizo haukushirikisha wazee wa kimila kwenye biashara machuma ulete niyakufikia, kuna kutupiana majini mazongo na kuna kutupiana mikosi salala, unafungua duka unaona wenzio wanasonga wewe hamna, wateja wanakupita wengine unawafuata kwa nguvu hamna hawaji kwako

Nenda stand saa kumi usiku stand nzima inanuka udi
 
Mkuu bado hujachelewa 40+kijana Bado na una afya halafu pia ni mpambanaji Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi ufanikiwe Sana na kwenye madini Rudi unayadai Sana na utafanikiwa.
 
Nimeshuhudia biashara ya mtu mmoja mlokole inafanikiwa sana, sema yule mtu anatoa zaka, alafu kwenye maombi usiseme alafu anaishi maisha matakatifu sana.

Aisee [emoji1787] umwambie mtu aache uzinzi, anaona Bora aende upande wa pili.
Siri yake hapo ni kutoa Zaka/sadaka.

Imeandikwa *mjaribuni kwa matendo yaliyo Mema"

Usione tabu kutoa fungu la kumi (10%) kwa unachoingiza

Umepata faida 100k siku ya Leo toa 10k wape watoto wa mtaani wapate Chakula, WAzee walemavu, na wenye shida

Mi huwa sipeleki Hela kanisa Hawa watu ndio Naona baraka zinakuja Moja kwa moja.

Na nishafanya sana hii kitu na nikaja pata Hela ndefu somewhere. Sometimes huwa hata nasahau niliowasaidia.

Mtu anakuja unamuona kabisa ana shida ila unamkaushia sio vizuri unazikosa baraka zako.
 
Mlilima kitu gani boss
 
Biashara ni ngumu sana binafsi naona mtu ni bora uajiriwe tu, watu ni wachawi sana hawataki upige hatua hii ni hadi kwenye kilimo wakiona shamba lako limestawi vizuri unapigwa kombora hatari.

Kuamini ushirikina ni ujinga.
 

Pole sana. Kwenye dhahabu ulikua upande gani mchimbaji, broker/dealer, muuza madawa/vifaa au?

I know a thing or two naweza shauri.
 

Exactly. Kilimo cha acre 10 sijui 20 sio biashara ni kutafuta hela ya kula tu. Huyu bado hajaanza biashara bado anajitafuta hajui nini anataka kufanya.
 
Kila biashara ina KSF zake boss kama zinapelea kimbia. Kwa sisi tuliopo kwenye biashara miaka mingi nikikaa nawewe wiki tu nishajua biashara gani utatoboa na gani utafeli.

Mfano kuna biashara ambazo pesa kubwa ndio KSF, kuna nyengine connection, kuna nyengine exposure, kuna nyengine bidii, etc etc.

KSF = Key Success Factor
 
Tunaomba mifano wa KSF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…