Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Kontena moja linatosha, kuanza maisha


1742036837215.png

1742036866226.png
 
Wanetu , njoonii tuuchangamshe Uzi wetu ............. Comment upo mkoa gani. Ki aina flani hivi ya kuficha CODE..mazee
Zilipo hustle zako....


Mimi......nipo mkoa ulio na mlim mrefu kuliko yote AFRICA. Wee je !!!
 
Hiki ni kisa changu. Nitaongea ukweli daima uongo kwangu mwiko

Mwaka mmoja baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo kikuu maarufu hapa bongo land nilikuwa nafukuzia fursa kadhaa mjini, wakati huo Bi mkubwa nimemkabidhi copy za vyeti vyangu na CV ili avipeleke kwenye maombi kwa nabii mmoja maarufu kutoka mji mmoja wa kanda ya nyanda za juu kusini wenye makanisa mengi kama Naijeria.

Fast forward. Siku hiyo baada ya kutoka kijiweni kucheza drafti nikapita kwenye kiosk kimoja hapo Mwaisa nikapiga viroba vinne vya ZED kisha nikaambaa mdogo mdogo mpaka kihome boy muda wa saa nane usiku, kufika home nikakuta taa zimezimwa na mlango umefungwa. Nikagonga kama mara nne kimya. Nikagonga tena na tena nikaona hakuna anayejibu.

Nikaanza kupayuka... "Ina maana mna dharau au hamnisikii, oyaa fungueni mlango bhana" . Hakuna aliyeitikia. Nikaona isiwe tabu, nikatoa msuba wangu wa bhange nikapuliza kama pafu nne kisha nikaazimia kuwa sitarudi tena maskani maana wamejikausha wote.

Nikaanza safari mdogo mdogo kwenda kwenye moja ya mabanda ya TV maarufu pale kitaa, hiyo sehemu ilisifika kwa watu kuangusha pale kwa kulipia pesa sawa na nauli ya kucheki muvi, yaani kwa jero tu unaangusha mpaka monii ila shuka utajua wewe na kitanda ni benchi au kiroba.

Pale nilikutana na wananzengo wana ndoto kubwa sana za kwenda mambele, wengine wanamafaili ya kufuatilia mirathi ya wazee wao, wengine mateja tu wanahesabu maokoto yao ya siku zile mia mbili mia mbili kisha wanaziuza kwa wauza chenchi. Tulipiga mastori mpaka saa 10 hivi ndio usingizi ukanichukua. Kushtuka saa 12 jamaa wameweka kanda ya X, nouma sana yaani madume tupu pale kila mtu mkono upo kwa mfuko macho kodo. Nikaona hiyo jau na mimi ni msomi nisiye na kitengo siwezi kujichoresha, nikaenda mitaa fulani maarufu kupiga supu ya kitimoto, enzi hizo ni mia tano kwa buku. Baada ya akili kukaa sawa sawa nikaona nikarudi nyumbani mdogo mdogo hiyo ni kama saa 2 asubuhi.

Mdogo mdogo njiani huku napiga mruzi, Kufika home nikakuta tranka langu la form six limewekwa nje, kuchungulia ndani kuna vyeti vyangu vyote vya elimu, vyeti vya ubatizo na nguo zangu. Dah! nilidata kucheki pembeni Bi mkubwa anapiga mswaki hata hana habari na mimi. Kumsalimia akaongea maneno ambayo nayakumbuka mpaka leo " Mzee wako amesema akirudi asikukute, kwa kukusaidia chukua lile godoro lako na sufuria mbili na ndoo ukaanze maisha yako".

Dah, hata kuoga sikukumbuka, sikuamini wanaona kijana wao wa miaka 25 nimekuwa na sina mchango wowote kwenye mjengo, nikachukua godoro huku nikimwangalia Bi mkubwa kwa macho ya huruma ili labda aseme jambo la huruma ila hakuongea chochote. Nikajua akufukuzae hana huruma na hacheki na nyani, nikasepa na tranka mkononi na gorodo kichwani. Hapo nilikuwa na akiba ya kama shilingi elfu 60 kwenye kibubu ndio mazima kwenda kupanga gheto la giza kwa miezi mitatu kwa Tsh. 45k.

Nilirudi nyumbani baada ya miezi tisa nikiwa nimekonda sana kwa kuchapwa na maisha ila nashukuru walinipokea na kunipa usia wa kuishi vizuri na walimwengu na kamwe nisiibe wala kutamani cha mtu. The rest is history.

Sio poa. Nimepitia mengi sana, nikipata nafasi nitatiririka. Trust the process.
 
Back
Top Bottom