Kumbe waganga nao wanaweza kurogwa

Kumbe waganga nao wanaweza kurogwa

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
548
Reaction score
661
Kuna jirani nasikiaga ni mganga wa kienyeji, kila akienda huko ofisini kwake (Nadhani ni Manzese na Kariakoo) huwa anarudi na nyama za mbuzi, kondoo, kuku nk. (wanasema za wanyama alioletewa kwa ajili ya kafara na wateja wake) Siku zingine anagawa kwa jirani zake. Mganga mwenyewe bwana mdogo tu, around 30 yrs.

Kuna dada mmoja jirani ana watoto wake wawili wa kike, mdogo alikuwa form 4 kipindi tunahamia hapa. Hii familia walikuwa wanamshobokea jamaa (Mganga) kwa sababu ana visenti na anawagawia sana hizo nyama akija nazo kwa sababu wao ni familia kubwa. (Mama [huyo dada sasa], watoto wawili wa kike, wajukuu wawili wa binti mkubwa, mtoto wa ndugu yake, na mtoto wa mme wake anayeishi nae kwa sasa, na mmewe mwenyewe). Mganga ana mke na mtoto mmoja. Kwa hiyo hizi familia mbili ni marafiki kwa sababu mke wa mganga ni age ya hawa binti za huyu dada. Kwa kifupi mganga maisha alikuwa mambo safi kwa standard za huku machakani kwetu, tukiangalia life style na kwamba alikuwa na bodaboda mbili.

Sasa picha lilianza pale mke wa mganga alipoenda kwao kusalimia. Hawa binti za huyu dada ndio wakawa wanampikia mganga, wanamuandalia maji ya kuoga, wanamfanyia usafi ndani na mambo mengine. Sasa wakati wa kudeki wanaweka mizizi humo kwenye maji, akitoka kwa muda mrefu wanafukiza madawa sana humo ndani, wakimuandalia maji ya kuoga wanaweka majani majani kwanza halafu wanayachuja. Majirani wanaona lakini mganga nadhani ni don't care, anajua hawamuwezi. Sasa mganga akaanza kutafuna binti mdogo huyo wa form four. Jamaa akirudi kabinti kanampokea kama wife kabisa chap kwa haraka, kanamfungulia mlango, maji ya kuoga fasta, akioga wanajifungia huko ndani sana wanapiga stori. Baadae mama wa binti akipika kabinti kanaenda kuchukua msosi kanamletea jamaa, kenyewe kanaenda kula kwao. Kakila, usiku mnene watu wakiingia kulala, kanaingia kwa mganga kulala katatoka kabla hakujapambazuka, kumbe wambea wanachunguza.

Baada ya mwezi hivi, majirani wakamfikishia umbea mke wa mganga kinachoendelea huku (Kuna vyumba 30 hapo na wapangaji zaidi ya 20, baadhi wana vyumba viwili viwili). Ghafla bin vuu binti wa watu akarudi kutetea ndoa yake. Mganga akampa talaka 3. Kosa la kwanza walikubaliana anaenda home atakaa miezi 2 karudi baada ya mwezi mmoja. Kosa la pili katoka Tanga mpaka Dar bila taarifa kwa mumuwe, angekumbwa na tatizo njiani je? Ndoa ikaishia hapo.

Sasa mganga akabeba zake majukumu ya kusomesha binti (AKA wife mtarajiwa). Binti kamaliza form 4, akaenda form five na akahamia kabisa gheto kwa mganga, walipoona maneno yamekuwa mengi wakahama kabisa hapa wakahamia kwa mbele kidogo. Binti akamaliza form six akaenda chuo, na boom akawa anapata asilimia 100. Mwaka wa 2 chuo akashika mimba. Akajifungua, sasa hivi mtoto anakaribia mwaka. Muda mwingi mganga akaanza kukaa nyumbani analea mtoto, akienda kwenye mishe, mtoto anamleta kwa mama mkwe. Jioni akirudi anapitia kumchukua wakati huo na mzazi mwenzie anakuwa alishatoka darasani. Wanasepa zao walikohamia. Huu ni mwaka wa 3 binti yuko chuo atamaliza soon.

Huko mganga maisha yakaanza kuyumba, baadae akauza na boda zote. Binti (mkewe) chuo akaanza kwenda kwa mguu. Miezi 2 iliyopita yeye (mganga) na familia wamerudi tena nyumba ile ile aliyokuwepo zamani bwana witch doctor, karibu na kwa mama mkwe. Nadhani ili kurahisisha maisha. Mganga wa watu sasa yuko home fulltime kama houseboy. Ndio anafua nguo zote (zake, za mke na za mtoto), anadeki, anapika, anaosha vyombo, na kazi zingine zote. Kijana wa watu maskini kawa mnyonge kinoma, hapigi stori tena na watu kama zamani, akipita anaweza asisalimie sjui anawaza mnamsema! Ukienda kwake ukamkuta anafua nguo za wife, anakuangalia kwa macho ya huruma sana. Wakati mwingine vyombo havioshwi mpaka vinachafuka vyote, anatafuta vibeki tatu vya Jirani vikaoshe. Nasikia wanasema wanakutaga vyombo vinanuka balaa kwa sababu ya kukaa na uchafu muda mrefu. Na hako kawaifu ka chuo kikuu kapo tu kanasikiliza komasava!!!! Hakajali wala nini na hakafanyi kazi yoyote, hata nguo zake hakagusi.

Sasa tetesi ni kwamba kanasema kakimaliza chuo kakapata ajira kanampiga chini jamaa, kamechoka na maisha ya kichovu hayo, eti mganga hana future!!! Kuna magunia mawili ya mkaa yatahitajika siku si nyingi. Yetu macho.

Majirani na umbea wetu tunajiuliza KUMBE HATA WAGANGA WANAROGEKA???
 
Acha umbea!!!
20250404_092420.jpg
 
Screenshot_20250510_210420_Google.jpg
 
Sijajuq umemaanisha kulogwa kwa adjee, lakini waganga wanalogwa zaidi kwenye kazi zake, kama kusoma bao, ramli, dawa, wateja, nyota n.k ndo maana muda wote waganga wako active na hata ukampa kazi akaoona huyo aliyeloga katumia ufundi mwingi

Basi atalazimika kutuliza akili hata kushirikisha wataalanu wengine zaidi ili asije patwa na kitu kilichomzd nguvu,

Huyo nyege ndo zilizomharibia kazi, na hasa ikiwa uganga wake inategemea una masharti yapi
 
Huyo dogo alikuwa sio mganga bali ni tapeli tu kama matapeli wengine wanojificha kwenye kivuli cha uganga.
 
Back
Top Bottom