Ulianzaje kukaa gheto?

Nilianza na godoro tuu 6/8 inch 10 ambalo nililichongesha Moja kwa moja kutoka Kiwandani since kitanda kikubwa ni ugonjwa wangu....sikua na bakuri wala kijiko....nilikua namiliki smartphone... Nguo zangu na mashuka ma4 baas
ulichongesha shilingi ngapi mkuu maana na mimi bado naishi gheto
 
Nakumbuka mimi nilijaribu kumwambia mzazi kwamba ni muda wa mimi kuanza kujitegemea...aisee nilifokewa vibaya mno maana niliambiwa bado mdogo na mimi nikawa mpole lakini baada kama ya miezi sita nikatafuta room nikanununa vitu muhimu na kama mwezi mmoja nimelipia gheto lakini nikawa sijahamia maana nilikuwa naogopa nitaanzaje..
Nilichofanya ni kumtafuta ndugu yangu mkubwa na kumuomba nimpeleke sehemu na baada ya kumpeleka gheto kwangu alishangaa na hakuamini vile vitu nilipataje na akanipa hongera kubwa na kusema kazi ya kuwaambia wazazi nimuachie yeye
 
Nakumbuka mimi nilijaribu kumwambia mzazi kwamba ni muda wa mimi kuanza kujitegemea...aisee nilifokewa vibaya mno maana niliambiwa bado mdogo na mimi nikawa mpole lakini baada kama ya miezi sita nikatafuta room nikanununa vitu muhimu na kama mwezi mmoja nimelipia gheto lakini nikawa sijahamia maana nilikuwa naogopa nitaanzaje..
Nilichofanya ni kumtafuta ndugu yangu mkubwa na kumuomba nimpeleke sehemu na baada ya kumpeleka gheto kwangu alishangaa na hakuamini vile vitu nilipataje na akanipa hongera kubwa na kusema kazi ya kuwaambia wazazi nimuachie yeye
Braza ulitisha sana...Big up mkuu
 
Mimi nilivyomaliza chuo mwaka jana nilirudi home sina hata pesa niliyokuwa naweka akiba kwa sababu nilikuwa sijapata mkopo baada ya kukaa home nilipata kazi mkoa wazazi wakanipa pocket money kiasi kidogo pamoja na nauli, nilitafuta chumba cha 25000 nikalipa kodi ya miezi miwili na godoro langu dogo. Maisha yalikuwa siyo mazuri sana cz mshahara nilikuwa nalipwa laki mbili na nusu tu. Nimekaa mwezi mmoja najitegemea ndugu yangu akaja akafikia kwangu kwa lengo la kuwa amekuja kufanya interview sehemu flani. Cha kushangaza hiyo interview hakwenda alikuja tu kupumzika. Maisha ya geto yalianza kuwa magumu sana cz mwanzoni nilikuwa najibana ili ninunue kitanda na vitu vinginevyo vya ndani. Huyu ndugu yangu alikuwa hajali wala hakuwa na mpango wa kuondoka kurudi kwao na isitoshe alileta marafiki zake wakawa wanakaa kwangu hata wiki mbili! niliwaza njia za kumkimbia nikashindwa, bahati nzuri nilipata training ya kazi nyingine ya muda, nikapata upenyo wa kumuondoa. Geto nililivunja nikarudi home kwa sababu kazi nilifanya karibu na nyumbani. Ila kwa sasa natamani tena nitoke nikapange tena nipambane na maisha.
ONYO. Ukiamua kupanga usipende sana kuendekeza ndugu. Watakurudisha sana kimaendeleo.
Nilichojifunza kama nna likizo nataka kwenda kwa mtu huwa natoa taarifa. Ukija getto kwangu bila taarifa utalala ila sitakutafutia kitu cha kula. Utajijua mwenyewe maana sijakuleta umejileta mwenyewe.
 
Ghetto life
1544610880108~2.jpeg
 
Kufupisha story ni kwamba gari ile niliifanya uber kipindi hicho ndo uber imeanza hope nilizisha mapambano kwani nlikuwa nahakikisha nalaza laki kila siku ya mungu na wife wakati yupo na ujauzito mkubwa akaajiri mtu wa kusambaza vitu vyake kwa wateja huku na mimi nikisambaza vyangu kwa gari huku wakati mwengne nikimsambazia na yeye,mwisho wa siku nilifungua duka ambalo wife baada a kujifungua akawa ndo msimamizi na pia deni la mzee la 20k kila siku nililitimiza na mwisho wa siku gari ikawa yetu,nakumbuka siku ya harusi babamkwe akatupa kiwanja kwa ksema altupa mtihani wa kujinunulia wenyewe means ile hela tulokuwa tunampa kila siku aliitu za na kutununulia zawadi ya kiwanja huk nasi tukiwa na vingine vitatu hiyo ndo story yangu ya geto ambayo imenipa mke na nyumba ambayo naimalizia now,watoto wangu mapacha,pamoja na gari 3,maduka na biashara nyingine na kunifanya nisahau kuajiriwa japo nna degree yangu ya first class
Daahhhh...
 
dah siiti getto saivi napaheshimu sana!!
ilikua baada ya kumaliza chuo.. niliumiza kichwa sana ntafanyaje nikae home.. hapana nitadharaulika sana.. kuna mshkaji mmoja nilisoma nae premary alikua mwanza anapiga mishe zake za boda boda.. nikaongea nae jamaa fresh.. nikatoka home bila kuwaanbia naenda mwanza.. ilibd niwadanganye maana wasingeruhusu niondoke bila hela... nilikaa kwa mshakaji mpk kesho ananiheshim sana.. nilikua nalala kwenye sofa.. usiku jamaa anakuja kalewa kinoma.. anankuta macho inabidi nitoke amgonge dem wake.. (nimepigwa exile sana).. ikawa kidogo tabu kupata kazi ya taaluma yangu.. nikaamua kushika chaki.. nikafundisha fizikia na hesabu.. nikawa nalipwa vizur.. mshahara wa kwanza tuu.. nikahama na kununua kitanda. mshahara wa pili nikaanza kununua vitu vingne.. nilikua na jeuri sana.. maana nilikua sinunui kitu cha kawaida.. yaan najibana miezi mitatu.. then naenda nunua bonge la kabatii.. nikilileta geto nasema sinunui tena kabati maisha yangu yote.. lbd anunue mwanamke.. saiv nikimkaribisha dem geto lazm aulize umeoa!?? nimejifunza mengi sana.. hapa ni nyumbani si geto tena!!
Hogera mkuu
 
Niliamua mwenyewe kwamba nahama, alafu sikusema. Nikanunua Kila Kitu ndani kwa siku moja ( nilikuwa na hela). Nikaa kama mwezi , nikasikia nyumbani kinawaka Mama hadi wajomba pia zangu wanawaka. Nakawapigia simu mmoja moja nikawaambia Mzee wangu hakuwa na Shida ila Mama ilikuwa taabu nakumbuka hadi nilimwambia " aah! sasa hivi nina marafiki wengi kuliko mwanzo, nina Marafiki wa Kiume na Kike pia alafu Mamaangu sasa hivi nakosa uhuru hapo kwako kuna mambo mengine siwezi kufanya nikiwa hapo ila nikiwa peke yangu nafanya. Najua hata hapo kwako siwezi kukaa milele, nitatoka na huu ndio muda wa kutoka" Mama akacheka akaniambia basi usipende kupikapika saana muda mwingine uwe unakula kwa Mama au Baba lishe ( hili neno lake nililing'amua baadae sana).
Maisha yanaendelea, haki nimejifunza mambo mengi huku kitaa!
Mkuu alimaanisha nini usipende kupikapika
 
Back
Top Bottom