NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Hakika ilikuwa ni siku ambayo binafsi niliumia, ni baada ya kushindwa kuendelea na elimu yangu nilipomaliza form 4 mwaka 2012..
pale home nilionekana nipo nipo tu, ikabidi nitafte mishe ya kujifunza useremala lengo likiwa nikianza kupata pesa nihame, haikuwa kama nilivyotegemea maana hata nilipopata sehemu ya kujifunzia mtaani na kumsaidia fundi nilikuwa sipati chochote zaidi ya chakula tu kwa fundi, hata nauli nilikuwa sina nakanyaga kwenda na kurudi, yani nikifika nyumbani nlikuwa sina amani maana sirudi na chochote.
Hii ilinifanya niongeze juhudi zaidi kujifunza kwa spidi, ndipo baada ya miezi kama 10 hivi nikaanza kupata vihela.
Sikulaza damu nikaondoka pale nyumbani fasta sana kwenda kupanga geto la elf 10 hapo nikiwa miaka 18 ukingoni.
Nakumbuka ndio siku ambayo nilimuona mama yangu analia iliniuma sana kwakweli, mzee nae akawa ananibembeleza nikae kae hapo home ila nilishakata shauri nikasepa.
Maisha ya mtaani yalikuwa tofauti sana, ila yalinifanya nipige kazi zaidi angalau nikaanza kupanga nje ya uswahilini
Anyway nilichojifunza hadi sasa hata upangishe nyumba hakuna uhuru, ilinibidi ninunue kiwanja na kwa sasa mdogo mdogo na mimi najenga kwangu japo ni kanyumba ka kawaida nitapata amani kuwa na kanyumba kangu.