Ulianzaje kujenga?

airwing

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
306
398
Habari za muda huu wanajamvi wenzangu

Kama uzi unavyojielezea, kuna watu wengi wanatamani kumiliki mjengo mjini lakini hawajui waanzie wapi, wapitie wapi, wafanye nini, watiririke vipi hatua kwa hatua za ujenzi na hivyo kukamilisha ndoto zao.

Kwa wewe mwenye uelewa au uliyefanikisha katika hili tunaomba tips zako, na vile ulivyofanikisha kusimamisha mjengo mjini.

NB: Mimi bado sijafanikisha hivyo naamini kuna vitu vingi nitajifunza hapa.

Karibuni
 
Kama unafanya kazi ya kuajiriwa, basi tafuta dili za pembeni ili u save mshahara na pesa ya vijishughuli itumike kaa ajili ya kuendesha maisha (kula/kuvaa)...

Nunua kiwanja nje ya mji, eneo lenye dalili za kuja kukua...

Dunduliza hela hatua kwa hatua, nyumba huanza na msingi hivyo target ya kwanza iwe ni namna ya kuanza kujenga msingi...
 
Nilianza kutafuta ramani ninayo ipenda na nyumba ndogo ya wastani ambayo inaendana na hali ya uchumi wangu

Kazi yangu haina mshahara, ni commission so pesa zangu hazitathiminiki

Niliamua kulipia kidogo kidogo kulingana na makadirio ya mahitaji ya ramani yangu kwenye hardware ninayo iamini, nililipia takribani miezi 6 na baada ya kuona vifaa vinaweza kusogeza mjengo, nilianza kutafuta mzigo wa fundi

Baada ya hapo nilianza ujenzi kama tajiri flani hivi kumbe sales tu. Mungu ni mwema japo sijamaliza ila nmefikia pazuri
 
Wakati unafanya haya malipo kidogo kidogo ulikuwa teyari na kiwanja? Je, hiyo hardware ulikuwa unafanyia malipo ilikuwa karibu na kiwanja chako?
 
Kiwanja nilikuwa nacho tangu mwaka jana mwezi wa 4, kiwanja changu nililipia taratibu taratibu pia

Baada ya kumaliza kulipia kiwanja nilianza kulipa hardware, nililipia kwenye hardware mbili tofauti, moja karibu na nyingine mbali kidogo ila baadae niligundua kuwa nilifanya kosa kulipa kwenye hardware ya mbali. Hardware ya karibu na kilipo kiwanja inasaidia sana kwenye transport
 
Baaada ya kununua kiwanja nilijenga kwa awamu Tatu na nimerumia almost miaka miwili na nusu

1)awamu ya kwanza nilitafuta milioni 10 nikanunua mifuko ya sementi, tofali,nondo, nikalipa fundi, jenga ukuta na kuchimba mashimo ya vyoo

2) awamu ya pili nilikaa miezi kama 12 nikapasahau pakaota mpaka majani nikajichanga milioni 12 nikapaua nyumba, bandaling kabisa, chonga madrisha ya gril, milango nilichongea kijjn coz mbao ni rahisi nilipelekea fundi sampo ya mlango, grill ya mbele na nyuma na vyoo nikanunua kabisa, nikaomba umeme,nikavuta na maji,

3) awamu ya tatu nikajipanga na 2mill nika pinga plazta vyumba viwili nikatengeneza chumba changu nikahamia

4) awamu ya nne natengeneza chumba kimoja kimoja mana siulizwi na mtu kwanza naishi kwangu na dilisha zangu za wavu nikipata ka laki nanunulia tiles mbona sina mwaka nyumba itaisha
 
Hongera
 
Back
Top Bottom