Ule upendo wa kweli bado upo?

Ule upendo wa kweli bado upo?

No No,kwani unazungumzia upendo wa agape???

Kwakweli nina muda sana kuona,ata mm nautafuta sana,kuna wimbo ameimba jamaa mmoja anaitwa ambwene mwasongwe unaitwa upendo wa kweli nadhani ndicho unazungumzia.
Tuendelee kutafuta mkuu..kama sie tunao tutapata wa kufanana nao
 
Naulizia ule upendo unaopenda toka moyoni Kwa Nia ya dhati.
Ule upendo ambao hauangalii una Nini au we ni nani au ukoje,unaakuangalia moyo wako.

Unaowaunganisha watu Kwa mioyo Yao na sio walivyo navyo.
Ule upendo ambao hata ukiporomoka Hadi 0 mwenzio bado anakwambia nipo nawe.tutatafuta tutapata na Maisha yataendelea.

Ule upendo hata ukiwa hoi unaumwa mfano umepata ajali bado mwenzio yupo pembeni yako,anakwambia utakuwa sawa na Maisha yataendelea.

Ule upendo unaojali bila ubinafsi.
Ukipatwa na aibu yuko mstari wa mbele kukusitiri
Unapojikwaa ndie wa kwanza kukuinua

Unaoheshimu viapo na ahadi.
Bado upo?
Maana siku hizi ndoa zinavunjika kirahisi sana.

Ukikosa kazi tu mwenzio huyo anaondoka. Akiona unachelewa kuzaa kashatafuta mimba nje
Ukipata ajali au ugonjwa ukakuacha mlemavu msahau!
Wanandoa wanakimbiana.watoto wanatelekezwa.

Mtu anaamua kuwa nawe sababu unaweza kumpa hiki ama kile lakini sio Kwamba anakupenda wewe kama wewe.

Wengine huenda Hadi madhabahuni kula kiapo ila after few months anaondoka.
Ama mwingine anaingia sababu unaweza mpa ndoa lakini hakupendi,unaletewa mimba sio zako,anafanyana na anaowapenda na kukuletea wewe damu sio zako.

Anazaa watoto nje Kwa anaowapenda lakini hawana vigezo vya kuwa wake,yuko nawe sababu unafit na uko tayari kuwa mke.

Upendo genuine kabisa ule upo?
Nasikia upo🤔
 
Back
Top Bottom