Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Wakuu,

Natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA, jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya mzigo, nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.

Ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana, duka hili lipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya Uhuru kwa jambo hili walilonifanyia kama mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sababu.

TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi wala sidaigi risiti! ni heri niwaachie wauza duka kodi yangu maana najua wataitumia wao na familia zao kuliko kuacha iende kuhonga upitishwaji wa mikataba hewa bungeni!! mbaya zaidi kodi hiyo hiyo inatumika na wale wanaotuta vilaza na wapumbavu!!! bora nimwachie muuza duka!!
 
Tatizo linaanzia Tra kwenyewe. Bandarini wana uplift kodi, afu rates zao ni kubwa, yani ukienda haki bin sawa, iyo biashara unaifunga 'within a week'.
Mwisho wa siku sisi tunaonunua hatuhusiki na hizo konakona zao.!
kwanini nikupe pesa yote kisha unipe risiti pungufu?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wala sidaigi risiti! ni heri niwaachie wauza duka kodi yangu maana najua wataitumia wao na familia zao kuliko kuacha iende kuhonga upitishwaji wa mikataba hewa bungeni!! mbaya zaidi kodi hiyo hiyo inatumika na wale wanaotuta vilaza na wapumbavu!!! bora nimwachie muuza duka!!
Akili yako unaijua mwenyewe!
ndio nyie mnaoacha bomba linavujisha maji nyumbani kwako kisha unalalamika bili unayolipa kubwa sana.!unaiba upande huu halafu unalalamika upande huu pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania hamna kitu apa pweehh !!! Aya ata risiti utaki kudai,.. Sasa unalalamika nn madarasa hayapo,..
 
Akili yako unaijua mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio naijua mwenyewe, we shida yako nini?
ndio nyie mnaoacha bomba linavujisha maji nyumbani kwako kisha unalalamika bili unayolipa kubwa sana.!unaiba upande huu halafu unalalamika upande huu pole sana.
Ivi kodi ukilipa, baada ya kwenda tra inaishia wapi? sio kwa wananchi? je muuza duka sio mwananchi?
 
Hivi kumbe watu hamjui umuhimu wa risit...
Nunua bidhaa nyingi za ghali halafu usichukue risit uone...
Like seriously hutaki risiti..kweli wabongo sisi bado....bado...bado
risit ni kwa faida yako achana na mambo ya kodi
Haya umeuziwa kitu kibovu..unarudishaje.?
Risiti ni muhimu. Hakuna duka lolote utakalonunua usipewe risiti ila za EFD ndiyo hawataki kutoa ila za kawaida hutapata.
Hata mm siwezi kununua kitu bila kupewa risiti sbb kuna kufanana kwa bidhaa hapo risiti ni muhimu kuwa nayo. Mtoa uzi aliomba za EFD hapo ikawa kasheshe. Kiukweli mm ili mradi ni risiti tena ya kawaida ni nzuri zaidi. UZALENDO USHAKUFA SIKU NYINGI KTK HII NCHI. MM MPAKA KESHOKUTWA SIWEZI KUWA MZALENDO KWA NCHI INAYOITWA TANZANIA.
Safi sana na hongera kwa mwenye duka. Km mtu anafuta ajira, usitegemee mwenye duka naye awe mzalendo km shetani mweusi. Never
 
Mkuu hii Sio wewe peke.yako.kitu kinachoitwa uzalendo kwa maduka ya Kariakoo ni msamiati hasa maduka ya watu binafisi hawatoi risiti halali hata wakitoa hutoa risti isiyoendana na thamani ya manunuzi uliyofanya.
Ukilazimisha wako tayari hata kutokuuzia mzigo.

Kariakoo kama kitovu cha biashara nchini ni tatizo hata kwa wafanyabiashara wa mikoani maana bila kupata risti halali sidhani kama wengine hasa wa mikoani wataweza kutoa risti halali.



Ukitaka kupewa risti halali ununue kwenye maduka ya makampuni angalau huko kuna risti halali.

Tra imulikeni Kariakoo ni tatizo kwa ukusanyaji wa Kodi nchini.
Kulipa kodi ni usengerema kwa nchi hii. Bora nimuachie mwenye duka akale na familia yake kuliko kumpa shetani mweusi kupitishia mikataba ya kuwagandamiza wananchi
 
Hujajibu swali nililouliza mkuu!!
Kodi inapopelekwa serikalini serikali inapanga matumizi kwa mahitaji ya jamii. Mfano Elimu, Afya, na miundo mbinu ukiiacha kwa huyo mfanyabiashara haiwezi kufanya yale ambayo serikali imepenga kwa faida ya jamii nzima.
mkuu sijui jinsia yako kama ni Ke au Me.
mfano baba anapotoa pesa kumpa mama kwa matumizi ya familia mama ndio anayejua kitu gani kitahitajika kununuliwa nyumbani na mtoto yupi anahitaji nini.
ni tofauti na baba kumpa mtoto pesa ya mahitaji ya nyumbani bila maelekezo kinachofuata baada ya kupewa hiyo pesa kinaweza kisiwe kwa msaada wa familia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Risiti inasaidia. Mfano umeingia kwenye daladala mtu kabeba mzigo wako utathibitisha vipi ni wako? Au umevunjiwa nyumba bahati nzuri polisi wamekata vitu vya wizi siku chache mbeleni ukienda kuvitambua utathibitisha vipi ni vyako?
Kuna watu wanashangaza. Wanadhani risiti ni kwa ajili ya TRA tu wasikukamate,kuna mtu alinunua marumaru katoni 10 katika ujenzi wake,baadae kuna store ya mtu ikavunjwa miongoni mwa vilivyoibiwa ni marumaru, wambeya wakatonya kuwa kuna jamaa alionekana anajengea marumaru mtaa wa tatu,basi jamaa kilichomsaidia ni risiti halisi yenye idadi ya katoni alizokuwa nazo home kwake
 
Kodi inapopelekwa serikalini serikali inapanga matumizi kwa mahitaji ya jamii. Mfano Elimu, Afya, na miundo mbinu ukiiacha kwa huyo mfanyabiashara haiwezi kufanya yale ambayo serikali imepenga kwa faida ya jamii nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Matumizi gani yamepangwa hadi sasa hivi?? jamii nzima gani?? kwanini nitoe kodi ili watutukane wapumbavu na vilaza??

mkuu sijui jinsia yako kama ni Ke au Me.
Ukijua itakusaidia nini? au unatafuta mume?
mfano baba anapotoa pesa kumpa mama kwa matumizi ya familia mama ndio anayejua kitu gani kitahitajika kununuliwa nyumbani na mtoto yupi anahitaji nini.
ni tofauti na baba kumpa mtoto pesa ya mahitaji ya nyumbani bila maelekezo kinachofuata baada ya kupewa hiyo pesa kinaweza kisiwe kwa msaada wa familia nzima.
Mkuu wangu naona umeandika maneno mengi yasiyo na maana!! Cha msingi baki na uaminicho niache mimi nibaki na nnachokiamini!!
 
Nimebahatika kutoka nje kidogo ya Nchi yetu na kuona watu wao walivyo makini kutoa risiti kwenye kila huduma wanayotoa.
nimeenda kampala Ugana kwenye kila duka liwe dogo au kubwa baada ya manunuzi watakupa risiti.
nimeingia kwenye migahawa midogo ya chakula kwenye jiji la kampala unapolipa chakula chako unapewa risiti..hata ule (katogo) bado utapewa risiti.
nimeenda Malawi kila bidhaa unayoipata toka dukani unapewa risiti..
nimekwenda kula kwenye mgahawa bado nikapewa risiti.
je watu wao ni wapumbavu ama wajinga? Kwanini kwetu Watanzania iwe shida kutoa risiti?
mimi binafsi kodi inanisaidia sana tu..
bado natumia hosptali za umma ambazo ninaweza kumuona daktari kwa bei nafuu sana.!
bado mwanangu anasoma kwenye shule za serikali ambako pamoja na upungufu uliopo bado mwanangu anapata elimu..
bado ninasafiri kwenye barabara za umma ambazo pamoja na mapungufu yake naamini kodi yangu inahisika.
hivyo mtu akiniuliza kodi yangu inanisaidiaje hayo ni kwa uchache ninayoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzalendo haupo. Km tu yule bwana anajua kbsa wengi waliosoma ualimu ni watoto wa masikini halafu anafuta ajira. Utategemea huyu atakapoanza kuuza duka atakupa risisi ya EFD? Never
Mm ili mradi iwe risiti km ni vitu vya kula huwa sichukui risiti.
Pole kwa kujifanya mzalendo
 
Tatizo la nchi yetu , kila kitu utekelezaji wake umekaa ktk mfumo wa chuki. Muuzaji anaambiwa kwa chuki to a risiti kama vile ugomvi

Mnunuzi naye anaamrishwa dai risiti kama vile muuza duka ni Mwizi, hivi kwann jambo hili lisielekezwe kwa upendo,unajua haiingii akilini kwann muuza duka akatae kutoa risiti .

Kwani risiti INA nn ndani yake mpaka mm niidai na muuzaji akatae kuitoa, Mimi napata faida gani?kwa kuidai, muuzaji anapata faida gani? Kwa kukataa kuitoa.

Ni level gani? Ya wafanyabiashara wanaotakiwa kutoa risiti au ni manunuzi yoyote ninayotakiwa kuyafanya kwa mfanyabiashara yoyote? Hivi elimu hii iko kote au ni kwenye miji tu.

TRA si wanayo ruhusa kukagua mizigo iliyoko dukani na iliyouzwa kisha kubaini kama risiti zimetolewa au la! Ukiangalia matangazo ya uhamasishaji kwenye TV ni maduka ya mtaani yenye pipi? Unga,majini ya chai,miswaki na nk ndo uhamasishaji upo lkn mpaka sasa hayana risiti.
 
kama kodi wamekusanya miana 50+ wameshindwa kujenga madarasa kodi ya leo ndio wataweza kujenga??

Hawakua wanaichukua kwa ufanisi, na raisi ni mwingine,.. Nyie ndo mmoja akikosa unajumuisha wote, such a losser
 
Matumizi gani yamepangwa hadi sasa hivi?? jamii nzima gani?? kwanini nitoe kodi ili watutukane wapumbavu na vilaza??


Ukijua itakusaidia nini? au unatafuta mume?

Mkuu wangu naona umeandika maneno mengi yasiyo na maana!! Cha msingi baki na uaminicho niache mimi nibaki na nnachokiamini!!
Kama unasukumwa na nguvu ya siasa pinzani sio rahisi kuona upande mwingine.!
Lakini huenda mifano hii michache ikawa na hoja ya kusukuma uelewa.!
Barabara za BRT. Au barabara za lami zinazokufanya usafiri kwenda kwenu.au hata kama za vumbi zimechongwa na katapila lililotumia mafuta.
ambapo bila shaka alipewa mkandarasi alielipwa kodi yetu.
au shule ile ya msingi unayoifahamu wewe ambayo huenda mwanao hasomi pale wale watoto wanafundishwa na mwalimu ambae analipwa na serikali inayotumia kodi tunayolipa sisi..!!

ama wakati ule bibi yangu mzaa baba alipoenda hosptali alilazwa katika kitanda cha hosptali ya serikali ambacho kimenunuliwa kwa kodi niliyotoa mimi, na hata yule daktari aliemuandikia panadol au asprini mshahara wake analipwa na serikali ambayo inapata pesa kutoka katika kodi ninayolipa mimi.
natumai utakuwa japo kidogo umeelewa umuhimu wa kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu usilalamike sana wasamehe bure mimi juzi nimeuza biashara yenye thamani ya milioni na point nilatoa lisiti lakini sikufichi faida yangu yote waliichukua TRA nilibaki na elfu 16000 acha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom