Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Unataka risiti halali huku unalialia upunguziwe bei
Anachoshindwa kuelewa ni kua, lile punguzo la bei alilodai limetoka kwenye kodi aliyotakiwa kulipa.., ukitaka bei ya chini basi jua unaiibia serikali, maana hata risiti utapewa ya chini ili kufidia pesa uliyopunguziwa
 
me naangalia mwenye duka ananiuziaje mzigo, na kama ananiuzia bei poa nikapate faida nzuri niweze kulisha familia, sasa nidai lisiti ya nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unanunua kwa bei ileile isipokuwa kwenye risiti anakuandikia pungufu anakwambia kwani hiyo si ya njiani tu. Kama ukikamatwa.!
Yaani kwa mfano bidhaa unanunua kwa tsh 100000 ikiwa ndio bei yake halisi. na unatoa hiyo laki moja
lakini kwenye risiti unaandikiwa tsh 40,000.
Ukiuliza anakwambia aah wewe si mteja wangu ndugu? Mjini hapa tusaidiane. Si unajua biashara tena.!
hivyo ina maana kama mtu huyu anawauzia wateja 100 kwa siku.. wa 100000. Anakua na mauzo tsh milion kumi. Halafu kwenye mashine inaonekaba kama milion 4 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongea tuu kwakua wewe ni msukuma ila hujui tuu. Mnataka mpunguziwe vitu kwa bei chee na risiti, ukiambiwa uongeze asilimia 18 ya bei mnalia hadi machozi. Siku yyte ukifanya manunuzi ukitajiwa bei waambie nnaongeza 18% ya bidhaa au ya huduma uliyopata. Hamna mfanyabishara ambaye hapendi kulipa kodi hapa duniani ila ni mfumo wa ulipaji unamnyonya mfanyabishara anaambulia faida kidogo ambayo haikidhi.
Mkuu huwa sina muda wa kudai kupunguziwa.! Lakini swali la msingi kwanini hiyo kasumba tuwe nayo sisi tu..!?
Kwanini wengine hawakwepi hiyo kodi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me kwakweli huwa hela ninayonunulia mzigo na risit napewa chini ya hela niliyotoa huwa siulizi sababu bila risit njiani lazima uulizwe pole kwa kujifanya mzalendo
apo shunie umenena ata kama nimenunua laki wakiandika elfu kumi poa tu ili mradi niwe nacho chakuzugia tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali iandae mfumo mzuri ambao hautamuumiza mfanyabiasha
Nadhani kwa malalamiko haya ya wanunuzi na endapo wanunuzi wote watakataa kupewa risiti feki
wafanyabiashara wanaweza kupeleka hiyo hoja yao serikalini na ikasikilizwa kuliko ujanja ujinga wa kuwaibia maskini wa Nchi hii kwa kukwepa kodi kipuuzi.
kuna Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania natumai mkiitumia vema kilio chenu chaweza pata nafasi.
toeni risiti halali uzalendo unaanza na mimi na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kwa malalamiko haya ya wanunuzi na endapo wanunuzi wote watakataa kupewa risiti feki
wafanyabiashara wanaweza kupeleka hiyo hoja yao serikalini na ikasikilizwa kuliko ujanja ujinga wa kuwaibia maskini wa Nchi hii kwa kukwepa kodi kipuuzi.
kuna Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania natumai mkiitumia vema kilio chenu chaweza pata nafasi.
toeni risiti halali uzalendo unaanza na mimi na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaaani usiongeee kabisa maanake hujui chochote kwenye hili waswahili wanasema raha ya ngoma uingiee ndani ucheze huo umoja wa wafanyabishara viongozi wake ni mapandikizi
 
Mkuu kama una uthibitisho kwanini usitumie fursa hiyo kuueleza umma hiyo habari yako?
Huoni kuwa utakuwa umewasaidia Watanzania kuokoa matumizi mabovu ya kodi inayotokana na jasho lao.?

kama matumizi mabovu ya fursa ya ndugu JPM hawezi kuwa wa kwanza tumeyaona hayo katika ngazi ya chini sana ya familia pale mmoja kati ya wanafamilia akiwa na fursa au uwezo wengine wanavyotumia jina lake kujinuafaisha huku mwenye jina akiwa hana habari..
Mh Rais ana mambo mengi sana ya kufanya ungeweka habari za huyo mtoto wa dada yake hapa. Za uhakika Ili umsaidie kupata taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilete ushahidi nitekwe??mkuu we jua tu kuwa wanasiasa wote sio upinzani wala ccm ni wachumia tumbo...tena moja kati ya njia watumiazo mafisadi papa ni kufanya maigizo kuwaaminisha watu kuwa wao ni watu wema..na kuna mmoja amefanikiwa kweli watu wanamuona kama malaika wakati ndo jizi ambalo halijawahi tokea kwenye historia
 
TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.
17546753_1880470288835585_1577424846985409113_o.jpg

Kama mbwai iwe mbwai...
 
Nilete ushahidi nitekwe??mkuu we jua tu kuwa wanasiasa wote sio upinzani wala ccm ni wachumia tumbo...tena moja kati ya njia watumiazo mafisadi papa ni kufanya maigizo kuwaaminisha watu kuwa wao ni watu wema..na kuna mmoja amefanikiwa kweli watu wanamuona kama malaika wakati ndo jizi ambalo halijawahi tokea kwenye historia
Ukweli humuweka mtu huru.!
endapo una hakika na kile ukisemacho mkuu nakutia shime wala usitie shaka jamii itakuwa nyuma yako.
hata mimi binafsi nitakuwa nyuma yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimebahatika kutoka nje kidogo ya Nchi yetu na kuona watu wao walivyo makini kutoa risiti kwenye kila huduma wanayotoa.
nimeenda kampala Ugana kwenye kila duka liwe dogo au kubwa baada ya manunuzi watakupa risiti.
nimeingia kwenye migahawa midogo ya chakula kwenye jiji la kampala unapolipa chakula chako unapewa risiti..hata ule (katogo) bado utapewa risiti.
nimeenda Malawi kila bidhaa unayoipata toka dukani unapewa risiti..
nimekwenda kula kwenye mgahawa bado nikapewa risiti.
je watu wao ni wapumbavu ama wajinga? Kwanini kwetu Watanzania iwe shida kutoa risiti?
mimi binafsi kodi inanisaidia sana tu..
bado natumia hosptali za umma ambazo ninaweza kumuona daktari kwa bei nafuu sana.!
bado mwanangu anasoma kwenye shule za serikali ambako pamoja na upungufu uliopo bado mwanangu anapata elimu..
bado ninasafiri kwenye barabara za umma ambazo pamoja na mapungufu yake naamini kodi yangu inahisika.
hivyo mtu akiniuliza kodi yangu inanisaidiaje hayo ni kwa uchache ninayoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua Watanzania tuna matatizo makubwa sana. Wengi hapa wanashabikia huu ukwepaji kodi. Lakini hawa hawa utawakuta kwenye thread nyingine wanaponda serikali kushindwa kutoa huduma fulani kwa jamii. Sijui wanafikri serikali hela inapata wapi kama sio kodi.
 
hawajielewiiii nadhani wanaobeza umuhimu wa kudai risiti kama wamesoma bac elimu zao hazijawasaidia kitu!!
Kweli kabisa. Yaani huwezi kuaamini comments hizi zinatoka kwa the so called 'Great Thinkers'
 
Wakuu,

Natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA, jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya mzigo, nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.

Ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana, duka hili lipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya Uhuru kwa jambo hili walilonifanyia kama mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sababu.

TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii Sio wewe peke.yako.kitu kinachoitwa uzalendo kwa maduka ya Kariakoo ni msamiati hasa maduka ya watu binafisi hawatoi risiti halali hata wakitoa hutoa risti isiyoendana na thamani ya manunuzi uliyofanya.
Ukilazimisha wako tayari hata kutokuuzia mzigo.

Kariakoo kama kitovu cha biashara nchini ni tatizo hata kwa wafanyabiashara wa mikoani maana bila kupata risti halali sidhani kama wengine hasa wa mikoani wataweza kutoa risti halali.



Ukitaka kupewa risti halali ununue kwenye maduka ya makampuni angalau huko kuna risti halali.

Tra imulikeni Kariakoo ni tatizo kwa ukusanyaji wa Kodi nchini.
 
Tatizo linaanzia Tra kwenyewe. Bandarini wana uplift kodi, afu rates zao ni kubwa, yani ukienda haki bin sawa, iyo biashara unaifunga 'within a week'.
 
Back
Top Bottom