Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu,

Natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA, jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya mzigo, nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.

Ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana, duka hili lipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya Uhuru kwa jambo hili walilonifanyia kama mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sababu.

TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tuna matatizo makubwa sana.
 
Risiti inasaidia. Mfano umeingia kwenye daladala mtu kabeba mzigo wako utathibitisha vipi ni wako? Au umevunjiwa nyumba bahati nzuri polisi wamekata vitu vya wizi siku chache mbeleni ukienda kuvitambua utathibitisha vipi ni vyako?
Hahahahaaah risiti ya efd wiki tu maandish yanafutika unathibitisha vipi mkuu
 
Hivi kumbe watu hamjui umuhimu wa risit...
Nunua bidhaa nyingi za ghali halafu usichukue risit uone...
Like seriously hutaki risiti..kweli wabongo sisi bado....bado...bado
risit ni kwa faida yako achana na mambo ya kodi
Haya umeuziwa kitu kibovu..unarudishaje.?
 
Hivi kumbe watu hamjui umuhimu wa risit...
Nunua bidhaa nyingi za ghali halafu usichukue risit uone...
Like seriously hutaki risiti..kweli wabongo sisi bado....bado...bado
risit ni kwa faida yako achana na mambo ya kodi
Haya umeuziwa kitu kibovu..unarudishaje.?
Shely je??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA. jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya Mzigo nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na Kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.
ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana.. duka hili lipo mtaa wa livingstone kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya uhuru.
kwa jambo hili walilonifanyia kama Mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sabbu.
TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi
nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani smartphone yako ina kazi gani?? Ungepiga picha hilo duka hata kwa nje.
 
Hiyo kodi imekusaidaje wewe bunafsi kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimebahatika kutoka nje kidogo ya Nchi yetu na kuona watu wao walivyo makini kutoa risiti kwenye kila huduma wanayotoa.
nimeenda kampala Ugana kwenye kila duka liwe dogo au kubwa baada ya manunuzi watakupa risiti.
nimeingia kwenye migahawa midogo ya chakula kwenye jiji la kampala unapolipa chakula chako unapewa risiti..hata ule (katogo) bado utapewa risiti.
nimeenda Malawi kila bidhaa unayoipata toka dukani unapewa risiti..
nimekwenda kula kwenye mgahawa bado nikapewa risiti.
je watu wao ni wapumbavu ama wajinga? Kwanini kwetu Watanzania iwe shida kutoa risiti?
mimi binafsi kodi inanisaidia sana tu..
bado natumia hosptali za umma ambazo ninaweza kumuona daktari kwa bei nafuu sana.!
bado mwanangu anasoma kwenye shule za serikali ambako pamoja na upungufu uliopo bado mwanangu anapata elimu..
bado ninasafiri kwenye barabara za umma ambazo pamoja na mapungufu yake naamini kodi yangu inahisika.
hivyo mtu akiniuliza kodi yangu inanisaidiaje hayo ni kwa uchache ninayoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kumbe watu hamjui umuhimu wa risit...
Nunua bidhaa nyingi za ghali halafu usichukue risit uone...
Like seriously hutaki risiti..kweli wabongo sisi bado....bado...bado
risit ni kwa faida yako achana na mambo ya kodi
Haya umeuziwa kitu kibovu..unarudishaje.?
hawajielewiiii nadhani wanaobeza umuhimu wa kudai risiti kama wamesoma bac elimu zao hazijawasaidia kitu!!
 
Punguza kiherehere...yaani mi nilipe kodi alafu fisadi la chatto likaitumie lenyewe na mtoto wa dada ake...sifanyi huo ujinga
Mkuu kama una uthibitisho kwanini usitumie fursa hiyo kuueleza umma hiyo habari yako?
Huoni kuwa utakuwa umewasaidia Watanzania kuokoa matumizi mabovu ya kodi inayotokana na jasho lao.?

kama matumizi mabovu ya fursa ya ndugu JPM hawezi kuwa wa kwanza tumeyaona hayo katika ngazi ya chini sana ya familia pale mmoja kati ya wanafamilia akiwa na fursa au uwezo wengine wanavyotumia jina lake kujinuafaisha huku mwenye jina akiwa hana habari..
Mh Rais ana mambo mengi sana ya kufanya ungeweka habari za huyo mtoto wa dada yake hapa. Za uhakika Ili umsaidie kupata taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me kwakweli huwa hela ninayonunulia mzigo na risit napewa chini ya hela niliyotoa huwa siulizi sababu bila risit njiani lazima uulizwe pole kwa kujifanya mzalendo
Mkuu vipi ikitokea unatakiwa urudishiwe pesa uliyotoa na ukamkuta mhusika mwingine kwenye hilo duka sio yule aliekuhudumia awali.!
je utakuwa radhi kupokea kiwango kilichoandikwa kwenye risiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom