Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Haijawahi kutokea hivyo mkuu tungoje hiyo siku yake
Kila la heri lakini ukiwa mfanyabiashara tegemea hilo kutokea lakini pia ni suala la hisia tu za ndani
ni sawa na kumuona mwizi anaiba nyumba ya jirani halafu anakwambia kausha usiseme.
au kuona bomba linavujisha maji nyumbani kwako halafu kwa sabbu ni kidogo unapuuzia.
unasahau kuwa bili ya maji ikija kubwa unaelazimika kulipa ni wewe mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Punguza kiherehere...yaani mi nilipe kodi alafu fisadi la chatto likaitumie lenyewe na mtoto wa dada ake...sifanyi huo ujinga
Ha ha ha ha ha kwani Dotto kafanyaje mkuu tueleweshe kidogo ili hata kama nao wamesahau wajue tunajua mkuu
 
Wakuu natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA. jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya Mzigo nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na Kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.
ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana.. duka hili lipo mtaa wa livingstone kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya uhuru.
kwa jambo hili walilonifanyia kama Mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sabbu.
TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi
nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kitu ambacho serikali haikijui na wananchi hatufahamu ila wafanyabiashara wanafahamu.

Ipo hivi:

Wafanyabiashara wengi kariakoo hufuata mzigo China. Wakishafikisha mzigo hutakiwa kulipia ile VAT. Sasa unakuta wengi wao wananunua ile mizigo kwa hela za kichina. Wanapokuwa wameleta mizigo hapa bongo ukimuambia alipe tena kodi inakuwa ngumu kukokotoa tozo la VAT.

Wengi wao ukiwasikiliza wanataka watoza kodi wa Tz wafanye utaratibu wa kukata kodi from source (yaani waende viwandani wakajue gharama halisi ya bidhaa husika ili wajue VAT inatozwa kiasi gani). China wanafanya hivyo.

Na mizgo mingine wanauziana wao kwa wao hapo kariakoo. Pia faida yao hapo kariakoo ni ndogo sana tena sana, yaani margin profit ni ndogo, hivyo wanategemea kuuza mzigo mkubwa ili kupata faida.
 
Siku mtu aninyime risiti ndo tutajuana majina ya kati na ya mwisho....nitadeal nae mpaka anione mchawi
 
Yakiwa machafu je utadaije matengenezo ya gari yako kama huna risiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bongo hiiwatu wanadai fidia ya matengenezo yagari kama mafuta yalikuwa machafu? Kama ingekuwa hivyo naamini TANESCO wangeshafilisika kwa jinsi umeme wao unavyounguza appliances za raia
 
Nimebahatika kutoka nje kidogo ya Nchi yetu na kuona watu wao walivyo makini kutoa risiti kwenye kila huduma wanayotoa.
nimeenda kampala Ugana kwenye kila duka liwe dogo au kubwa baada ya manunuzi watakupa risiti.
nimeingia kwenye migahawa midogo ya chakula kwenye jiji la kampala unapolipa chakula chako unapewa risiti..hata ule (katogo) bado utapewa risiti.
nimeenda Malawi kila bidhaa unayoipata toka dukani unapewa risiti..
nimekwenda kula kwenye mgahawa bado nikapewa risiti.
je watu wao ni wapumbavu ama wajinga? Kwanini kwetu Watanzania iwe shida kutoa risiti?
mimi binafsi kodi inanisaidia sana tu..
bado natumia hosptali za umma ambazo ninaweza kumuona daktari kwa bei nafuu sana.!
bado mwanangu anasoma kwenye shule za serikali ambako pamoja na upungufu uliopo bado mwanangu anapata elimu..
bado ninasafiri kwenye barabara za umma ambazo pamoja na mapungufu yake naamini kodi yangu inahisika.
hivyo mtu akiniuliza kodi yangu inanisaidiaje hayo ni kwa uchache ninayoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongea tuu kwakua wewe ni msukuma ila hujui tuu. Mnataka mpunguziwe vitu kwa bei chee na risiti, ukiambiwa uongeze asilimia 18 ya bei mnalia hadi machozi. Siku yyte ukifanya manunuzi ukitajiwa bei waambie nnaongeza 18% ya bidhaa au ya huduma uliyopata. Hamna mfanyabishara ambaye hapendi kulipa kodi hapa duniani ila ni mfumo wa ulipaji unamnyonya mfanyabishara anaambulia faida kidogo ambayo haikidhi.
 
Back
Top Bottom