Ungefanya jambo la maana km ungemrekodi mwenye duka hilo kwa siri na kupiga picha duka hill kisha ungerusha hewani ili mamlaka zifuatilie kwa kutumia vidhibiti hivyo....vingenevyo unaonekana km unapiga tu majungu.Wakuu,
Natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA, jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya mzigo, nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.
Ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana, duka hili lipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya Uhuru kwa jambo hili walilonifanyia kama mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sababu.
TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app