Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Ukwepaji kodi Kariakoo yamenikuta

Mkuu huwa sina muda wa kudai kupunguziwa.! Lakini swali la msingi kwanini hiyo kasumba tuwe nayo sisi tu..!?
Kwanini wengine hawakwepi hiyo kodi?


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani huko kwingine kodi ni % ngapi? Kwa muono wangu naona 18% kwenye bidhaa ni kubwa sana, kiwanda chenyewe unakuta hakiweki margin 18% ila serikali inataka 18%...
Ni sawa tu na kodi za kuagiza magari ni kuumizana tu, kwanini wasiweke mfumo rafiki kwa wote ili kodi isigeuke kuwa adhabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Natanguliza malalamiko yangu tena kwa TRA, jana yamenikuta baada ya kujifanya mzalendo na kutaka risiti yenye thamani halisi ya mzigo, nimenyang'anywa mzigo na mwenye duka na maneno kibao ya kashfa na kejeli. Nikiambiwa najifanya mzalendo niende nitakako.

Ukweli nimedhalilishwa sana! Nimefedheheshwa sana! Na nimeumizwa sana, duka hili lipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni duka la pili baada ya ghorofa la Bakhresa! Upande wa kushoto ukitoka barabara ya Uhuru kwa jambo hili walilonifanyia kama mbwai basi iwe mbwai nimetengeneza uadui usio na sababu.

TRA timizeni wajibu wenu fanyeni uchunguzi mchukue hatua kila mtu anatakiwa kulipa kodi nimetoa dukuduku langu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kariakoo Usipende Kudai Risiti Iandikwe Unavyotaka Wewe Subiri Uandikiwe Wanavyojua Dhen Chukua Mzgo sepa Hii itakusaidia Kwenye warrant yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi ni mfanyabiashara pia nipo keko fenicha apo na efd ndio natumia.
Unanishangaza zaidi kama wewe ni mfanyabiashaea halafu hujui kutunza risiti zisifutike au kutunza risiti hata zikifutika usipate shida. Utakuja kuulizwa risiti za miaka minne iliopita utakosa jibu.
Nunua scanner, scan risiti zako save as soft copy kwenye files maalum. Ungekuwa unnafanya VAT returns ungenielewa.
 
Kuna watu hata wakinunua diamond karanga watadai risit

Kupima mkojo na uchochezi wapi na wapi??
 
Mfanyabiashara anae-comply VAT haimbabaishi tena inamsaidia. Ndio maana makampuni makubwa yanapenda kufanyakazi na waliojisajili kulipa VAT.
Kama unaingiza/unanunua mzigo kihalali kwa wholesaler lazima ulipe VAT. Mfano umenunua mzigo wa 10m hapo VAT ni 1.8m. Sasa kama hujasajiliwa VAT hio 1.8m inaenda TRA (imepotea).

Lakini kama umesajiliwa VAT kila ukiuza unachaji watu VAT huipeleki moja kwa moja TRA, unatoa kwenye hii 1.8m kila mwezi mpaka iishe.

Mimi nina miezi 5 sasa hivi tangu nisajiliwe VAT sijawahi kupeleka kwasababu nimelipa VAT kabla wakati naleta mzigo,sasa hivi bado nawadai TRA hela so VAT imo kwenye risiti na naingiza mzigo every three months hivyo najikuta bado natakiwa nirudishe VAT yangu ninayolipa nikiingiza mzigo.

Lakini kama huingizi mzigo kihalali VAT lazima uione chungu.
NB:Sio kila,mwenye EFD analipa VAT wengine hawalipi VAT, wanalazimishwa kutumia EFD ili TRA wajue mapato yao halisi. Sasa naona kila mtu anashadadia EFD inakata kodi,sijui inaongeza bei.

Im NOT Tax expert nawweza kukosea niko tayari kusahihishwa.
 
Yakiwa machafu je utadaije matengenezo ya gari yako kama huna risiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wenzio akili ya kufikiri imeishia hapo unajua watu wanaongea hivyo wamezoea kununua vya barabarani, mie siwezi nunua kitu changu cha thamani halafu aniandikie utumbo wake je huko kimeibiwa watajua vip kama mie ndiye mwenyewe siku hizi vitu vingi grantee mkuu tv miaka 2 sasa poteza risiti kama watakuelewa mpaka box lake unatakiwa kwenda nalo kama tv imepata shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimebahatika kutoka nje kidogo ya Nchi yetu na kuona watu wao walivyo makini kutoa risiti kwenye kila huduma wanayotoa.
nimeenda kampala Ugana kwenye kila duka liwe dogo au kubwa baada ya manunuzi watakupa risiti.
nimeingia kwenye migahawa midogo ya chakula kwenye jiji la kampala unapolipa chakula chako unapewa risiti..hata ule (katogo) bado utapewa risiti.
nimeenda Malawi kila bidhaa unayoipata toka dukani unapewa risiti..
nimekwenda kula kwenye mgahawa bado nikapewa risiti.
je watu wao ni wapumbavu ama wajinga? Kwanini kwetu Watanzania iwe shida kutoa risiti?
mimi binafsi kodi inanisaidia sana tu..
bado natumia hosptali za umma ambazo ninaweza kumuona daktari kwa bei nafuu sana.!
bado mwanangu anasoma kwenye shule za serikali ambako pamoja na upungufu uliopo bado mwanangu anapata elimu..
bado ninasafiri kwenye barabara za umma ambazo pamoja na mapungufu yake naamini kodi yangu inahisika.
hivyo mtu akiniuliza kodi yangu inanisaidiaje hayo ni kwa uchache ninayoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu vumilia hayo majibu. Nchi ina wapumbavu wengi sana. Kilichonifanya niseme mimi hii nchi basi ni pale majirani walipokuwa wanahoji mbona leo hatujakatiwa umeme.
 
Natoka kidogo nje ya mada,

Wataalamu wa Sheria mtusaidie,

Nijuavyo kwa MNUNUAJI kudai risiti ni HAKI,
Kwa MUUZAJI kutoa risiti ni WAJIBU.

Sasa huwezi kumuadhibu MTU asipodai HAKI,
Lakini asipotimiza WAJIBU unaweza kumuadhibu,

Naelewa umuhimu wa wateja kudai risiti , jambo la msingi ni kuwaelimisha wananchi na kuwasihi sana wawe wanadai RISITI,

Lakini naamini KISHERIA hakuna MTU anaweza kushtakiwa kwa kutodai HAKI yake.
 
Bado rist za efd zinamapungufufu mf. Jina la mbunuzi na aina ya bidhaa hazipo kwa rist so muuzaji bado anawez kumkana mnunuzi,hiki ni tatizo kubwa!!
 
Mkuu Kariakoo Usipende Kudai Risiti Iandikwe Unavyotaka Wewe Subiri Uandikiwe Wanavyojua Dhen Chukua Mzgo sepa Hii itakusaidia Kwenye warrant yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pilot.
inaeezekana upo sahihi lakini busara yangu inaniambia yanipasa kupiga kelele ili wanao husika wachukue hatua.!
sidhani kama kariakoo ni kubwa kiasi cha kuishinda serikali hii. Tunajua kuwa kariakoo ndio kitovu cha biashara cha Nchi yetu hivyo uozo ukianzia hapa unaenea kila mahali..
Tafadhari TRA hata kama mkipiga kambi hapo kwa mwezi mmoja bado mtaokoa pesa nyingi mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pilot.
inaeezekana upo sahihi lakini busara yangu inaniambia yanipasa kupiga kelele ili wanao husika wachukue hatua.!
sidhani kama kariakoo ni kubwa kiasi cha kuishinda serikali hii. Tunajua kuwa kariakoo ndio kitovu cha biashara cha Nchi yetu hivyo uozo ukianzia hapa unaenea kila mahali..
Tafadhari TRA hata kama mkipiga kambi hapo kwa mwezi mmoja bado mtaokoa pesa nyingi mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao TRA wenyewe wapigaji tu...huwa wanatisha watu pale ili waongwe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelekezo yanatosha watu Wa intelijensia wanaelewa ,wafanye kazi yao maduka mengi ya Kariakoo hawatoi risiti ,wakitoa hazilingani na thamani ya malipo uliyotoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado rist za efd zinamapungufufu mf. Jina la mbunuzi na aina ya bidhaa hazipo kwa rist so muuzaji bado anawez kumkana mnunuzi,hiki ni tatizo kubwa!!
Risiti halali ya EFD ina sehemu ya kujaza jina na TIN ya mnunuzi. Iangalie vizuri, ni kiasi cha kumwambia muuzaji aandike jina lako.
 
Back
Top Bottom