Yamkini uko sahihi, !
sijajua umeweza tembelea maeneo mangapi ya Nchi hii na sijui wewe uko wapi katika Nchi hii.
lakini mimi binafsi shughuli zangu zinanifanya nisafiri sana ndani ya Nvhi yetu kwa bahati iliyo njema hakuna mkoa ambao sijafika toka mtwara mpaka Kagera na kote natumia Gari binafsi.
na nimeweza safiri pia Nchi jirani kwa kutumia usafiri huohuo wa gari binafsi kote huko nimeenda nikiendesha mwenyewe.! Mtu akisema Nchi yetu haina maendeleo huwa namtazama kwa jicho la ajabu sana tena sana tu.
ndio maana nikasema kama ni siasa sitakuwa na uwezo wa kupingana nawe.
sabbu kila mwanasiasa hutetea tumbo lake..(wachumia tumbo) penye ukweli ataweka uongo mradi tu apate uashawishi wa ugali wake na wanawe.
Kama huna uzalendo sioni tofauti yako na wale wanaojitoa muhanga na kuua wananchi wenzao katika Nchi zao kwa itikadi wanazoamini wao ni sahihi..
nini tofauti yako na wafuasi wa Boko haramu,au alshabab ama hao wengine wafananao na hao?!
nilidhani urithi wetu ni Taifa letu ambalo vizazi vyetu watajivunia baada ya sisi kutimiza wajibu wetu na kuondoka!
lakini ukikutana na mtu kama wewe na akapandikiza hulka yako kwa watoto wetu yaani wasiwe na moyo wa kulipa kodi wala Uzalendo kwa Taifa lao halafu unategemea wataitwa kwa Utaifa upi?
Wamarekani ? Au.. Taifa gani ambalo wala haliishi katika mioyo yao.
ukizaa mtoto kisha akawa mwanajeshi na umemrithisha akili kama ya kwako.
unategemea ikitokea vita atapambana kwa ajili ya Taifa hili?
sina budi kukwambia yakupasa uone "AIBU"
TANZANIA ITABAKI KUWEPO KWA AJILI YETU NA VIZAZI VYETU NI LAZIMA TULIPE KODI ILI WAJE WAWE NA TAIFA BORA.
Sent using
Jamii Forums mobile app