SoC03 Ukweli usemwe! Kijana usipojifunza kutafuta pesa umasikini ni rafiki yako

Stories of Change - 2023 Competition

mwesigwa jr

Member
Feb 24, 2015
7
2
Tunatumia pesa kila siku na tunahitajika kutafuta pesa kila siku usiruhusu siku ipite bila kutengeneza pesa,na njia pekee ya kutengeneza pesa nikujifunza kutengeneza pesa.naumia sana nikimuona kijana mwenzangu wasasa pamoja na fursa zote hizi zilizopo bado anashindwa kujipatia kipato chochote.

Ukweli ni kwamba wakati wewe kijana bado unalalamika kuwa ajira hakuna na unamiliki smartphone ambayo unatumia sanasana kuwatukana watu mitandaoni kuna wengine wanatumia smartphone hizo hizo kuendesha maisha yao. Hilo hilo bando unalolitumia kuangalia porn(picha za utupu) kunawenzako wanadownload movies kisha wanatengeneza magroup ya telegram na whats app wanauzia watu,na kipato kinaingia .

Wakati wewe unacheka na udaku na kujibinua makalio tiktok kuna wenzako mtandaoni humo humo wanajifunza ujuzi mpya mfano graphics design,socialmedia management ,urembo na mengine mengi kisha wanaya practise mwishowe yanawaingizia kipato.wakati, wewe unalalamika mitaji hakuna kunawenzako wanatumia platform hizo hizo unazotumia na simu hizo hizo kama yako wanatengeneza content za makampuni au kutangaza bidhaa za watu na wanaingiza hela ya kutosha bila ya kuwa na fedha ya mtaji. Kiukweli nikuambie acha ujinga. Acha kujiona unafahamu kila kitu tafuta maarifa ya kutengeneza pesa utengeneza hela.

Internet imeleta fursa nyingi,imezalisha ajira mpya nyingi chache tuu naweza zitaja social media management,digital marketing,content creation,influencers na nyingine nyingi usiachwe nyuma nyuma jifunze.nikweli unasubiri ajira toka serikalini ila nakuhakikishia ukiijua siri Hutatamani tena.Wajibika juu ya maisha yako hakuna mtu atakuja kukuwajibikia kila mtu anayake yana mkabiri furaha yangu itakuwa kukuona wewe unafanikiwa cousin yangu.

Unahitajika kuwa smart kichwani kuzinusa fursa,swali unalopaswa kujiuliza mara kwa mara ni nawezaje kutoa pesa mifukoni mwa watu wanaonizunguka kuliko kuwaza ni msanii gani ana gari kali.Kaa na kampani ya watu wenye chachu ya kutamani kufanikiwa utajikuta unapata deni la kutaka kufanikiwa ila ukizidi kuambatana na watu uliowazidi kila kila kitu cousin watakuvuta ufanane nao.tambua katika ulimwengu wasasa vitu vidogo vidogo unavyo vidharau ndivyo vyenye pesa.

kuliko kulala tafuta hata shilingi elfu tano nunua karanga zifunge kwenye vifuko kaingie ubia na wakina mangi mtaani kwenu wakuuzie mgawane faida siutaki kuonekana unauza, hutakosa mia ndugu yangu .kukosa pesa kutakuletea msongo wa mawazo utajikuta unatusumbua kukutibia,jichanganye kwa watu uzidi kujinoa,mimi na kwambia sababu nakupenda chukua ushauri wangu ipo siku utanikumbuka na ukinikumbuka iwe ni kheri ausio cousin yangu.

Kaa vizuri leo jitafakari ikiwezekana chukua notebook orodhesha ujuzi wowote unao hisi unaujua kisha chagua kati ya hizo upi unaujua vizuri jinoe zaidi. Nakuambia kuna mtu mahali anauhitaji na ujuzi huo unachokosea wewe unashindwa kujiweka sokoni hivyo hawakuoni, tumia kurasa zako za mitandao kuwa cv ya kuuelezea ujuzi wako.sasa kama mfano ni mwanasheria na kurasa zako haziuelezei huo uwanasheria sisi tutajuaje?.tupe vyuma hivyo cousin tukutafute shauri yako.

Najua utaniuliza wateja nitapata wapi?,sikia ngoja nikuambie cousin kwenye hiyo whats app yako siuna namba za watu zaidi ya ishirini sasa unataka soko gani jingine?. Siri kubwa ya mtu kuwa mteja wako nikukuamini sasa hao watu wote unaowasiliana nao whats app kia siku wanakujua hivyo wanakuamini niswala la wewe kuwaonesha ni nini wanaweza nunua kutoka kwako ukiwafanyia hao watu wachache kitu kizuri na kwa uaminifu watakuwa mabalozi wazuri wa biashara yako kwa watu wao wengine yangu ni hayo cousin.

KATAFUTE HELA ACHA KULAUMU WATU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom