Ukweli ndio huu wadada... Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli ndio huu wadada... Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Money Stunna, Oct 22, 2012.

 1. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,092
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Najua wengine watapinga lakin huu ndio ukweli,naandika hivi kwa sababu nimeona wake za watu wengi wakidanganywa na kujipendekeza kwa wanaume wengine kwa sababu ya vitu vidogo dogo kama vocha,pesa za salun,nguo etc
  Mim nashauri msichana kabla ujaolewa angalia kwanza mtu wa kuolewa naye,kama ni mwanaume suruali au mtafutaji ili asije kukupeleka pabaya.
  wasichana waliotokea familia ya chini ni bora muolewe na mtu kutokea familia ya kuanzia wastani,ili muweze kujikimu kwa mambo madogodogo,hasara ya msichana kutokea familia ya chini kuolewa na kijana duni inaweza kupelekea msichana kuja kushawishika na mambo madogo ambayo yako nje ya uwezo wake,simaanishi vijana wa hali ya chini wasipate mke ila wajitaid waondokane na hali duni ndio wafikirie kuoa.
  Wadada wengi wanaotokea familia duni wakioa mtu duni wanaish maisha duni na mara nyingi mwanaume anakuwa na hasira sana ata inapotokea mke ametumia pesa sh3000 bila kumwambia mme wake atapokea kipigo.
  nashauri wadada kuepuka hivo ni bora ukaolewa na mwanaume mtafutaji na mwenye kujikimu ili muishi maisha bora yasiyo na shida ndogo ndogo kamwe kipofu awezi kumuongoza kipofu mwenzake
   
 2. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,663
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  If marriage is all or at large about money then u r very correct
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kweli mimi kwa kilaza sirushi mguu
  mtu kareseat form form mara mia
  hana maisha ya kueleweka
  hapana hapana
  hajui ata kuuza nyanya
  no big no
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 41,986
  Likes Received: 9,828
  Trophy Points: 280
  Hata utafute pesa kama ni wakutoka ata toka tuu!

  Kama mtu wa kusubiri kuletewa lazima uwaze kusaliti ndoa, lakini kama ni mchakalikaji huwezi kuwaza!

  Ni bora unge washauri nao wajishughulishe kutafuta hizo pesa hili wote wawe watafutaji si mmoja kuwa goalkeeper!

  Mungu kagawa huwezo kwa kila mtu hivyo kila binadamu ana uwezo wa kutafuta!

  Na wanaume tuna hitaji wanawake wachakalikaji sio wakusubiri alitewe! Leta na mimi ni lete na mapenzi ni kusaidiana!

  Hepuka kuwa mzigo ndio mwanzo wa kunyanya sika!
   
 5. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Unadumaza watu wewe..
  Mwanamke kuwa mtafutaji yeye kama yeye ndo mpango mzima!

  Utasubiri kuolewa na mwanamme mtafutaji ilhalli na familia yake inategemea mgao huo huo.....and probably wanandugu almost wote!!

  Utakesha!!!
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  ndege wanaofanana waruke pamoja
   
 7. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hata akili ya kushona lapa za watu hana.......khaaa!!
  Mwogope kama ukoma!!
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 41,986
  Likes Received: 9,828
  Trophy Points: 280
  Sasa mtu ana subiri aletewe tujiulize amekatika mikono?
  Huku kusubiri kuletewa kuna waliza wengi na kunyanyasika!

  Na unakuta yeye ana subiri aletewe na kwao wanamsubili alete. Huu ni ugonjwa mbaya sana!

   
 9. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,092
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  kuna mtu apa atajisikia fahari kuona dada yake anaolewa na mwanaume asiye na mbele wala nyuma?
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kuna wanaume hawapo responsible kabisa
  hawezi hata kukupa ushauri zaidi ya kukwambia vua chupi
   
 11. Risa

  Risa Senior Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He!!! wanaume wenyewe mgogoro kuwapata ati!!!! wakianza kuchambua si ndo watakosa kabisa????????????? halafu mimi sikubaliani na wewe kwa asilimia zote. Nachojua na nachoamini mimi siyo maisha duni yanayomfanya mtu kuwa na tabia hizo bali inakuwa ni tabia zake hata angepewa pesa kiasi gani kwa vyovyote vile angefanya. Kwani wangapi tunawaona kila kukicha wana maisha mazuri lakini bado wanakukuruka na vidumu pembeni??????
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  aisee usije jipeleka kwa mwanaume kwa kumuonea huruma kwamba ipo siku ataamka...mwanamme mvivu ni mvivu tu..kama maisha yamemshinda mwenyewe wewe ndo ujipeleke? mtu aoneshe juhudi hata kama anapata kidogo
  ndo yale yale nilianza na mume wangu hana kitu nimemsaidia kapata hanithamini...si hajatoa jasho?
  mimi kwa kweli mwanaume lazzy nooooooo
  akauze hata nyanya soko kuu tule dagaa huko simlishi kiti moto au kuku kwa hela yangu atakula hivo vitu siku akipata hela ya kuvinunua
   
 13. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Na ikitokea shida utasikia........sii uuze kitanda! haangalii hata rate ya maisha!
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  au mkope kakako basi kooote kwao anakuwa keshaharibu
  useless man!
   
 15. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Hapo kwenye blue;
  Kuna watu watakwambia "MUNGU KAKUCHAGUA ILI AMBADILISHE"
   
 16. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,092
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  kuna wanaume wenzangu muda wote wanakunywa kahawa na kupiga story,wolokoso nyingi,wanabishana siasa na majungu inapotokea binti ukaolewa kwa mwanaume kama uyu inakuwa imekula kwako,mjitaid muolewe na watu wenye kuwajibika,watafutaji kwa maendeleo ya familia
   
 17. K

  KEEN PERSON New Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila kusema ukweli alilosema lina ukweli hata kama kimaneno tutapinga,kiuhalisia yupo sahihi.
   
 18. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ndo hapo unakuta mtoto kaptura ya shule imechanika anaambiwa subiri baba yako aje kutoka safari!
  (Hapo mama kabana hela apeleke kwao......uchuroo tu)
   
 19. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,139
  Likes Received: 915
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha, nina work mates mdada hapa nimemuonesha kamkope kaka ako amecheka sana as ana tabia ya kumkopesha mume wake as anajifanya amemkopea kwa kaka ake,, tulimbananaisha kwa nini anamkopesha mume wake asimpe bure tu, akadai atakuwa mzembe as hela anayompa anapata kwenye mgao wa kodi wa nyumba zao za urithi so mume hatakiwi kuingilia wala kujua kama kuna hela anapataga kila mwaka za urithi.. Sema watoto ndo wanahusika as zinawahusu but mume hazimuhusu...
   
 20. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Wewe kama ni mzazi......basi dekeza sana binti zako ukitegea waje kuolewa na wanaume wenye hali nzuri!
  Na siku mwanaume akiukata ndo utakapo uona utamu wa kubakiwa na historia!

  BTW,mmesahau ndoa inacomprise vitu gani!
  Mwaume anaweza akawa well off lakini ndoa isijengeke hata robo!
   
Loading...