mireille
JF-Expert Member
- Mar 4, 2020
- 321
- 424
JINA LA SIMULIZI.......................LISA
WHATSAPP.....................0628924768
SPONSORED BY.. SIMULIZI ZA DULLY
SURA YA .......................................1&2
SURA YA 1
“Paah!” Kofi kali lilitua usoni kwa Lisa Jones Masawe. Kofi hilo halikutoka kwa mwingine zaidi ya mama yake, aliyejulikana zaidi kama Mama Masawe.
“Umeniangusha sana. Dada yako amekuwa na wakati mgumu kwa zaidi ya miaka 20, sasa amerejea na anataka kuolewa. Bila aibu unapanga kumpokonya mwanaume wake. Huna aibu kabisa!” Mama Masawe alimuwakia mwanae Lisa.
Akiwa amejifunika sehemu ya uso wake iliyokuwa inauma, Lisa alimtazama mama yake bila kuamini. “Mama, Ethan ni mpenzi wangu tangu nikiwa shule. Kila mtu anajua hilo. Mnawezaje kuwa watu wasioelewa kiasi hiki?” Maneno yaliyokosa chembe ya heshima kwa mama yake yalimtoka Lisa kwa jazba.
Ndo kwanza Lisa alikuwa anafika nyumbani baada ya safari ya masomo nchini Marekani. Alimkuta dada yake mkubwa aliyepotea kwa muda mrefu, Lina Jones Masawe, akiwa amerudi. Wakati huo alikuwa ameketi na mpenzi wake Ethan kwenye kochi. Walioketi upande wa pili wa kochi walikuwa wazazi wa Ethan, Zackaria Lowe na Sonya Mushi ambao walionekana kuwa na mazungumzo ya kupendeza.
Kwa kweli, Ethan alikuwa mpenzi wa Lisa. Wamekuwa pamoja kama majirani lakini walipokuwa shule ya sekondari ambapo walisoma kidato kimoja, urafiki wamapenzi ukachanua kati yao na walikuwa wameahidiana kuoana. Baada ya kuhitimu chuo kikuu, Ethan alijiunga na baishara ya familia yao kama msimamizi wa kampuni ya Lowe Enterprises. Lisa naye alifanya kazi muda mfupi tu kwenye kampuni yao ya familia, Kibo Building Desing Group kabla ya kwenda kuongeza elimu ya juu ya uinjinia katika ujenzi kwenye chuo kikuu cha New South Wales nchini Marekani. Kwa muda wa miaka miwili walikuwa wakiwasiliana kwa simu tu.
Sasa baada ya Lina kurudi, Lisa anashangaa imekuaje tena Ethan amgeuke na kumchukua dada yake? Hakuweza kujizuia kumwendea Lina ili kumuuliza. Hata hivyo aliishia kupigwa kofi kali la uso na mama yake hapo hapo!
"Mama, tafadhali acha kumpiga Lisa ." Kwa sura ya wasiwasi, Lina alisema. “Ni kosa langu. Sikupaswa kurudi.”
Ethan alimshika mabega haraka. “Hapana Lina, ni kosa langu. Siku zote nilikuwa namchukulia Lisa kama dada yangu mdogo na rafiki yangu. Huenda kuna kitu amechanganya kati ya mapenzi na urafiki.”
Kuna kitu kilionekana kulipuka kichwani mwa Lisa . Maumivu ndani ya moyo wake yalikuwa makali sana hivi kwamba alishindwa kupumua.
“Eti Dada? Yaani leo hii mimi nimekuwa dada yako?” Macho yalimtoka Lisa sawia na maneno yake. “Kwa nini uliniahidi utanioa ikiwa ulinichukulia kama dada yako?
Kwa nini kila mara ulinikumbatia kwa nguvu na kunibusu na kunaimbia maneno matamu matamu ikiwa tu ulinichukulia kama dada yako?”
“Lisa..” Lina alitaka kusema neno lakini akazimishwa na karipio kali la Lisa.
"Nyamaza!" Alijikuta maneno hayo hayavumiliki na yalikuwa yakimjaza karaha.
“Wewe ndio unapaswa kufunga mdomo wako. Hivi ndivyo unavyotakiwa kuongea na dada yako?” Mama Masawe aliimfokea Lisa. "Je, huwezi kumheshimu dada yako? Ukizingatia kwamba amepitia miaka ishirini ya maisha magumu akiwa nje ya familia hii?"
Kwa mshtuko, Lisa alilegea kidogo. Ilibidi kuwe na kikomo cha uvumilivu hata hivyo. Kwa nini aache mapenzi yake yapotee? Yeye pia ni binadamu, ana moyo unaouma.
Wakati huo, baba wa familia hiyo, Jones Masawe alisimama na kumwambia Lisa kwa ukali pia. “Umemaliza? Ethan ameshasema yeye si mchumba wako. Bado tunahitaji kujadili sherehe ya uchumba ya Lina sasa. Kama hutaweza kunyamaza bora uondoke. Usituletee zogo hapa."
Lisa alitetemeka na kumtazama Ethan ambaye hamkujali kabisa. Kisha akamtazama Lina ambaye alikuwa amemng'ang'ania. Ghafla, alihisi kama moyo wake unaganda kwa hasira. Watu hawa ndio alikuwa anawajali sana, lakini kila mmoja wao alikuwa akiegemea upande wa Lina kwa wakati huo. Machozi yalionekana kumtoka. Baada ya kufuta machozi, Lisa aligeuka na kuondoka na mkoba wake bila kuangalia nyuma. Bila kujua pa kwenda, alisimama na kumpigia simu rafiki yake wa karibu, Pamela Masanja.
"Pamela, ni mimi Lisa, nimerudi. Njoo tunywe pombe, leo nataka tulewe mpaka tukeshe." Sauti yake ilisikika kuwa ya kishindo katikati ya kwikwi zake.
Pamela alikubali mara moja. “Hakika. Nitakuwepo baada ya muda mfupi.
SURA YA 2
Pamela alipofika kwenye baa maarufu ya Mambo Garden, Lisa alikuwa tayari amemaliza chupa nzima ya mvinyo mwekundu peke yake!
“Umekuja kwa wakati muafaka shosti. Nitakuagizia chochote unachotaka. Huruhusiwi kuondoka hadi umalize vinywaji.” Lisa alimiminia Pamela glasi ya 9mvinyo.
"Nini tatizo?" Pamela alimuuliza kwa wasiwasi. Ilikuwa ni nadra sana kwa Pamela kumkuta Lisa akiwa anakunywa pombe kiasi hicho. Aliingiwa na wasiwasi sana kuhusu Lisa. Isitoshe hakujua kama alikuwa na furaha ama matatizo kwani ni miaka miwili walikuwa hawajaonana kwenda masomoni Marekani, japo walikuwa wakiwasiliana kwa simu na mitandao ya kijamii. Sasa baada ya kurejea tena nyumbani ni kitu gani kilikuwa kimemkuta?
“Ethan yuko wapi, kakufanyia nini?” Pamela alihisi huenda ni mpenzi wake, Ethan ndiye aliyemzingua, bila kujua kwamba alikuwa anatchoma msumari wa moto kwenye jeraha bichi la Lisa.
Alipotaja tu jina la Ethan, Lisa alihisi kana kwamba kuna kisu kikali kinakwaruza moyo wake. "Ameniacha, na sasa yupo na Lina na wanapanga sherehe za uchumba."
Pamela alicheka kwa hudhuni. Hakuamini kabisa alichosikia. "Hii ni kweli au naota?"
Lisa alimweleza kwa ufupi kilichotokea jioni hiyo wakati anafika nyumbani kwao. Pamela alihisi hali ya kutokuamini. Ethan na Lisa walikuwa marafiki wa karibu tangu utotoni na walikuwa wameanzisha uhusiano wa kimapenzi tangu shule ya sekondari. Hata hivyo, katika miaka miwili hivi, Lisa alikuwa anasoma nje ya nchi huku Ethan akiwa na shughuli nyingi za kazi. Hiyo ndiyo sababu iliyowachelewesha kuchumbiana rasmi. Lakini, wazazi wao wote wa pande zote mbili waliufahamu fika uhusiano wao. Pia walitoa baraka zao kwa wanandoa hao watarajiwa. Kila mtu katika mzunguko wao wa ndugu jamaa na marafiki alijua kwamba Ethan na Lisa wangefunga ndoa mapema au baadaye.
Sasa, ikawaje kwamba Ethan alikuwa amemtosa Lisa na kuangukia kwa Lina? Hilo lilimchanganya Pamela na kumfanya Lisa aonekane kama kituko cha mwaka.
“Baba yako na mama yako wamerukwa na akili?” Pamela alishindwa kuelewa. “Huu ni upuuzi. Wewe na Lina wote mna umuhimu kwa wazazi wenu.”
Lisa alishika glasi ya mvinyo na kuongea kabla hajaigida mdomoni mwake. "Labda wanahisi kwamba Lina ameteseka sana huko alikokuwa. Kwa kuwa sasa amerudi, wanataka tu kumpa kilicho bora zaidi.”
Pamela bado alikuwa katika hali ya kutoamini. "Lakini wewe ni binti yao pia!"
Lisa alilazimisha tabasamu. “Hah. Sasa Lina amerudi, wanachojali ni Lina tu. Lisa lipigida funda jingine la mvinyo na kuendelea kuongea, “tangu mwanzo wao ndio walitaka kunioza kwa Ethan. Sasa kwa kuwa ninalichukulia suala hilo kwa uzito, wananiita sijakomaa. Pia, Ethan aliahidi kuwa nami milele, lakini amebadili mawazo yake hivyohivyo. Ninamchukia…” Maneno ya Lisa yalikuwa na ladha ya uchungu.
Mwishoni mwa sentensi yake, Lisa alianza kulia. Akiwa ameshika glasi alichukua mikupuo kadhaa ya mvinyo na kuruhusu machozi ya uchungu kumwagika machoni mwake. Wakati huo, alianza kuhisi kizunguzungu kidogo.
“Usinywe pombe kupita kiasi. Una kichwa chepesi sana. Utajisikia vibaya ikiwa utakunywa kupita kiasi.” Pamela alimpa angalizo. Alinyakua glasi ya mvinyo ya Lisa ili kugeuza mawazo yake kutoka kwayo. Baada ya hapo, alitazama macho yake kuzunguka baa. Kamwe hakutarajia kuona mtu aliyemjua. “Haya, tazama hapo!”
Pamela alimsukuma Lisa na kumuonyesha mtu aliyekuwa amekaa pembeni. Licha ya mwanga hafifu kwenye kona hiyo, mtu huyo alionekana vizuri. Alivaa suti ambayo haikufaa kwa mazingira hayo. Alivaa suti maridadi ya kibiashara. Mwanamume huyo alikuwa amefumba macho yake na alikuwa ameegemea kochi, akitoa nuru ya uzuri wakati mwangaza wa taa iliyozunguka ulipomwangazia mara kwa mara. Alionekana kuvutia sana hivi kwamba uso wake ulikuwa mzuri kama masanamu yale yanayovalishwa nguo kwenye maduka ili kuzitangaza kwa wateja. Baada ya kumtazama, Lisa alikwepesha macho yake kutoka kwake. "Hata awe ni mzuri kiasi gani, siko katika hali ya kufurahia kitu chochote kinachopendeza macho sasa hivi."
"Najaribu kukuambia kuwa mtu huyo ni mjomba wa Ethan." Pamela alimwambia.
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. "Una uhakika?" Ethan hapo awali aliwahi kumwambia Lisa kuwa alikuwa na mjomba wake tajiri sana. Hata hivyo, mjomba wake huyo alikuwa anafanya baishara zake nje ya nchi, kwa hiyo Lisa hakuwahi kumwona.
“Ndio, nina uhakika kuwa ni yeye. Kaka yangu alinionyesha tulipohudhuria hafla ya chakula siku moja. Nikasikia ni kijana mdogo tu na ana pesa sana. Hata baba yake Ethan hamfikii kwa utajiri alionao. Siku chache zilizopita, nilisikia kwamba alikuwa amerudi Bongo.
Macho ya Lisa yakaangaza. Mara moja akapata wazo lililomjia kichwani. “Naam! Unafikiri nini kitatokea nikiolewa na mjomba wa Ethan?”
“Pff…” Kwa mshtuko, Pamela akapaliwa mvinyo mdomoni mwake. “Sema hivyo tena?”
Lisa alimtazama kwa makini tena kijana yule aliyevuti kisha akafafanua hoja yake kwa Pamela. “Kwa kuwa siwezi kuwa binti-mkwe wa familia ya Lowe, nitakuwa shangaziya Ethan tu kwa kuolewa ha mjomba wake ili nipate nafasi ya kuwakomesha Ethan na Lina wake!”
Pamela alipigwa na butwaa kwa muda, kisha baada ya kufikiria kwa undani hoja ya Lisa, aliona imekaa poa! Akamwonyesha Lisa dole gumba mara moja. “Yeye ni mzuri, mzuri sana kwa kweli. Niko upande wako! Muonekano wa mjomba wake Ethan ni mkamilifu. Hata Ethan si mzuri ukimlinganisha naye. Utajiri na uwezo wake pia unazidi ule wa familia ya Lowe. Utakuwa umejiheshimisha sana ukiolewa na huyu kijana” Pamela alizidi kuchombeza. “Lakini je, utawezaje?”
Lisa alizidi kuchangamshwa na maneno ya uchochezi ya Pamela, akili yake ikapagawa namna ya kumpata huyo mtu.
"Ninahitaji kukukumbusha kwamba unapaswa kupata mume bora, msomi, mwenye pesa, au nafasi yako katika kampuni ya ‘Kibo Group’ itakuwa duni kuliko ya Lina. Kwa hiyo nadhani huyu mjomba wa Ethan anakufaa!” Pamela alitia maneno yake.
Lisa aliduwaa kwa sekunde. Alichokisema Pamela kilionekana kumwingia akilini. Ikiwa Lina angeolewa na Ethan na kuungwa mkono na familia ya Lowe basi nafasi ya Lisa ya kuwa mrithi wa kampuni ya familia yao Kibo Group ingekuwa hatarini. Kwa hiyo ujanja hapo ulikuwa ni kumpindua ili yeye aolewe na mtu maarufu zaidi kuliko Ethan ili heshima irudi kwake.
“Sawa, nitauteka moyo wake sasa hivi kama jambazi vile!” Lisa alijipa moyo wakati akimpokonya Pamela mkoba kisha akatoa lipstick na foundation. Alijipodoa kidogo na uso wake ulionekana kung'aa.
Pamela akaangaza macho. "Uh, una uhakika unaweza kukabiliana naye sasa hivi?"
“Unanionaje kwanza, mimi ni binti mrembo na yeye ni mwanaume tu, sivyo? Haha!” Lisa alijigamba kisha akafagia nywele zake kwenye bega moja na kumimina nusu ya mvinyo kwenye glasi. Akiwa na sura ya kuvutia na ya kupendeza, alitembea kuelekea kwa kijana huyo kwa maringo na madaha. Kadiri alivyozidi kumkaribia mwanaume huyo, ndivyo uso wake wa kupendeza ulivyozidi kuwa wazi. Macho yake safi yakionekana kuwa na huzuni kidogo na muundo mzuri wa sura yake vyote vilionekana kuvutia.
“Hi! Samahani kwa kukusumbua, lakini unaweza kuniambia muda sasa?" Lisa aligonga kidole chake begani kwa yule mtu mara mbili.
Mwanaume huyo alipofumbua macho yake yaliyolewa chini ya mwanga hafifu, neno ‘malaya’ lilimjia kichwani. Alimwona Lisa kama malaya tu anayejiuza.
Ubongo wa Lisa uliganda kwa sekunde chache. Baada ya kupata fahamu zake, alitabasamu na kusema, “Nafikiri kukutana kwetu kwa mara ya kwanza hapa ni mwanzo wa furaha yetu.”
Akiwa na uso uliobeba dalili za kukereka, yule mwanamume alisema kwa upole, “Mimi si daktari, sitoi matibabu kwa vichaa.”
"Nini?" Lisa aliuliza.
“Wewe ni kichaa, sivyo?” Midomo ya kupendeza ya mwanaume huyo ilivutia sana, lakini, maneno yaliyotoka kinywani mwake yalikuwa machafu sana.
“Mh!” Lisa akaguna. Wakati huo, Lisa alibidi atoe kioo ili ajiangalie tena kwa makini kama kweli sura yake haikutosha kumvutia yule jamaa. Lisa hakuona kasoro yoyote kwenye sura yake. Hata hivyo, hakukata tamaa. Haikuwezekana kufahamu mawazo ya wanaume vinginevyo Ethan asingemsaliti.
“Kweli mimi ni mgonjwa wa kichaa na kichaa changu ni cha mapenzi.” Lisa alitulia haraka na kutoa tabasamu la aibu. "Na kichaa changu cha mapenzi kilinipanda nilipokuona wewe kwa mara ya kwanza hapa."
Kijana yule mtanashati alipoinua uso wake, mara Lisa alichukua fursa hiyo kusema, "Wanasema mtu hawezi kujizuia kujisikia furaha anapokutana na mwanamume anayeweza kumfanya aonekane kama kichaa. Huyo ndiye mpenzi wa maisha yake, na hivi ndivyo ninavyohisi kwa sasa."
“Sawa, nimezisikia tenzi zako tamu za mapenzi, nimeburudika. Unaweza kuondoka sasa?” Mwanaume huyo alikwepesha macho yake mbali naye kwa namna ya kukatisha tamaa. Yale yote aliyoyasema Lisa yalionekana ni usumbufu tu kwake.
Lisa aliumia sana. Alikuwa mrembo wa kuvutia kwenye macho ya wanaume wengi. Kila siku alikabiliana na usumbufu mwingi wa wanaume waliokuwa wakimtaka kwa gharama yoyote ile. Kwenye mitandao ya kijamii wanaume walipagawa kila alipochapisha picha zake. Lakini kwa wakati huo ilikuwa tofauti. Kijana yule alikuwa anajisikia kwelikweli. Lisa alitamani kugeuka na kuondoka, lakini alipoifikiria nafasi ya kuwa shangazi wa Ethan, hata hivyo, akapata ujasiri wa kuendelea kumshawishi tena.
"Mpenzi mzuri, unaweza kunitajia namba yako ya WhatsApp?" Kimya!
“Kijana mzuri, unaweza kunipa namba yako?” Kimya!
“Handsome boy, unaweza kuniambia jina lako?” Kimya!
"Baby boy, unaonekana kupendeza na kuvutia sana kiasi kwamba mwanamke lazima apagawe anapokuangalia tu..."
Hapo walau akaambulia mguno tu wa yule jamaa. Kwa kukerwa na sauti ya Lisa aliyeonekana kukosa haya kabisa, mwanamume yule alifumbua macho yake na kuuliza kwa sauti ya kuudhika, “Unataka nini?”
“Nataka unioe, nataka niwe mke wako!” Lisa alifunguka moja kwa moja.
Mdomo wa mwanamume yule ukatetemeka kwa mshangao! Kwa muda akasalia kimya akimtazama Lisa kana kwamba ni kinyago. “Kweli wewe sikichaatu, bali mwendawazimu kabisa. Sijawahi kuona mwanamke akitafuta mwanamume wa kumuoa baa, tena asiye mfahamu.”
Huku akitabasamu, Lisa aliongeza, “Kusema kweli nina mpango wa kuwa mkeo. Japo nilichokisema kitaonyesha kuwa nimekosa aibu, au mimi ni mhuni ama malaya, vyovyote vile. Lakini nimesema ukweli wangu. Nina umri wa miaka 24 mwaka huu, na nilihitimu kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales Marekani. Mimi ni mwanamke mwenye uwezo wa kufanya vizuri nyumbani na kazini. Zaidi ya hayo, nitamtunza mume wangu. Nina uwezo wa kujitafutia pesa pia. Mimi ni mzima wa afya na sijawahi kufanya tabia yoyote mbaya. Zaidi ya yote, mimi si mpenzi kigeugeu.” Lisa aliitumia nafasi yake kujinadi vyema.
Yule mwanamume alikosa la kusema. Akayapapasa macho yake, kisha akamtazama kwa mshangao, bado mdomo wake uligoma kutoa neno lolote.
Lisa aliinua mkono wake. "Naweza kuapa kuwa kuanzia sasa na kuendelea, nitakutendea mema tu na kukuahidi kutekeleza kila kitu nilichosema..."
"Nyamaza. Hatimaye mwanamume yule alishoshwa na maneno yake, akasimama.
Lisa alipoinua macho ndipo akagundua kuwa kweli mwanamume yule alikuwa mrefu. Alikuwa karibu futi sita na inchi mbili juu, na zaidi ya hayo, alikuwa na umbo pana la kiume haswa.
"Ikiwa unataka kuolewa na mimi, kesho saa nne kamili asubuhi ufike na cheti chako cha kuzaliwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala." Mwanaume yule alimtazama akiwa kasimama, mkono mmoja ukiwa unasisitiza maneno yake huku mkono mwingine ukiwa mfukoni.
Lisa alipigwa na butwaa, hakuamini kabisa alichokisikia licha ya kuwa ndicho alichokuwa akikitaka, akajikuta anauliza kwa kigugumizi, “u..uu..uko seriuos?”
"Ukipenda uje ukipenda uache, ni juu yako." Yule mwanamume alimjibu kijeuri na kwa mkato kisha akageuka na kuondoka zake.
Wakati huohuo, gari aina ya Bentley Mulsanne lilisogea taratibu kuelekea lango la baa hiyo. Mlango wa gari hilo ulipofunguliwa, mwanamume aliyetoka kwenye baa ile akaingia ndani kwa madaha na kukaa kwenye kiti cha nyuma. Alifungua vifungo viwili vya shati lake juu ya kifua chake kupata hewa huku akiegemea kiti cha ngozi kwa uvivu.
“Si nilikuambia nataka nionekane wa hadhi ya chini safari hii, mbona umeniijia na gari la gharama hivi?” Mwanamume yule alimuuliza dereva wake.
Hans, ambaye alikuwa ni msaidizi wa kazi wa jamaa huyo mtanashati alijibu kwa upole. "Samahani mkuu, lakini Sam amesema hili ndilo gari la gharama ndogo zaidi kwa sasa katika familia ya Harrison."
“Kesho ukanunue Harrier, sitaki kuvutia umakini wa watu.” Yule mwanamume alikunja uso kidogo. "Nani mwingine anajua kuwa nipo Dar?"
"Ukiachana na Sam Harrison, hakuna mwingine isipokuwa Bibi Kimaro pekee." Hans alijibu.
Mwanamume huyo akamfikiria tena yule msichana aliyetoka kuongea naye ndani ya baa, na akamkabidhi Hans kazi ya kupepeleza wasifu wake. "Tafuta mtu huyu ni nani. Nataka kujua habari zake kabla ya mapambazuko.” Hans akakabidhiwa picha za Lisa alizopigwa kistadi na huyo jamaa wakati akiongea naye kwenye baa.
•••
Mpango wa Lisa ulienda haraka sana kiasi kwamba alijishuku kuwa alikuwa amelewa kupita kiasi. Japo alitaka sana kufakiwa jambo lake, hakutarajia kama yule mwanamume angekubali kirahisi vile. Lisa alihisi kama utani vile.
Wazo hilo lilibaki akilini mwake hadi Pamela alipokuja kumshtua kwa kumgonga begani, akamwambia kwa huruma, “Usikasirike sana. Si rahisi kuunasa moyo wa mwanamume handsome, tajiri na maaruf kama huyu. Endelea kujaribu hivyo hivyo—”
“Hapana, amekubali!” Lisa alionyesha wasiwasi huku akionekana kuduwaa. “Kaniambia tukutane kwenye lango la ofisi ya mkuu wa wilaya kesho saa nne asubuhi, ndiyo nipo nawaza, hivi kweli anamaanisha ama ananichora tu?”
“Wee!” Pamela alikaa kimya kwa muda kabla ya kuangua kicheko. “Hongera kwa kuwa shangaziwa Ethan!”
Lisa akauliza, “wewe unaamini kuwa kasema ukweli?”
Pamela aliubana kwa nguvu uso laini wa Lisa . "Kwa nini isiwe hivyo? Kwa mwonekano wako safi na wa asili, hakuna mwanamume anayeweza kukukatalia. Ikiwa ningekuwa mwanaume, ningekupenda mara ya kwanza tu kukuona. Twende tukanywe kusherehekea ndoa yenu.”
Lisa alijiuliza sana Pamela alikuwa amekunywa pombe kiasi gani baada ya kumuacha kwa muda ule mfupi. Alipotazama matupu mezani, alielewa kilichokuwa kwenye akili yake.
Hata hivyo, Lisa alianza kujisikia kulewa sana baada ya kunywa pombe kupita kiasi. Alihisi kichwa kuwa kizito.
ITAENDELEA....
Kwa leo tuishie hapa niseme tu tukutane katika sura ya 3 kujua nini kitafuata Je, mwanaume huyo mtanashati atatokea kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kama ambavyo amlimwambia Lisa?, pia ndioa ya Lina na Etham itakuwaje, basi sehemu inayofuata itakupa majibu zaidi.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app