Ukweli mtupu usiopingika kuhusu maisha

Mundele Makusu

JF-Expert Member
Sep 28, 2021
884
1,307
Katika maisha ya leo ukijionea huruma, utakuja kutia huruma.

Ukikosa nidhamu, utakuwa kuadabishwa na walimwengu

Ukijidanganya utakutana na ukweli muda ukiwa umepita.
Tujifunze na kutia maanani yafuatayo:

1.Thamani yako ndo inaamua mkate unaoingiza. Ikiwa chini, lazima ipande kubadili matokeo. Hakuna namna.

2.Hakuna anayejali unachofanya, watu wanajali unachoweza kuwafanyia.

3.Hakuna mtu alitajirika kwa kuwa mlaji. Pesa na mafanikio ziko kwenye kuzalisha chako. Anza kuzalisha.

4.Pesa ngumu ni ya kufanya kazi kila siku kwa siku 30, na kulipwa mara moja. Vipi ukizalisha kitu na ukakiuza siku zote za maisha yako?

5.Vita nyingi utapigana peke yako. Ndio una ndugu na marafiki, lakini ukweli ni kwamba kuna mambo mengi ya muhimu kwao kuliko wewe. Usishangae kushindwa kusaidika na uwezo ukiwapo.

6.Waliofanikiwa sio kwamba ni wajanja kivile, ni wazuri tu wa kuhakikisha mipango inaenda.

7.Kutoboa kunakuja kutokana na kufanya mambo mengi magumu ambayo wengi hawawezi kuyafanya. Komaa.

8.Ukitumia nusu tu ya muda unaofikiria zaidi kufanya kazi, utakuwa mbali kuliko watu wengi.

9.Zaidi ya 90% ya muda mwingi unaosoma, kuweka mipango na kutafakari unakuwa una-procrastinate tu. Fanya kazi achana na mipango.

10.Una hazina kubwa 3: Muda, energy na attention. Zitumie vyema kukua. Usizipoteze.

11.Kama unashindwa kupost biashara au hustle zako mtandaoni, una madhara makubwa sana ya mifumo ya jamii. Amka. Umefungwa.

12.Hupati kile unachotaka, unapata kile unachokuwa. Work on yourself.

13.Kazi kadri inavyozidi kuwa ya kutumia nguvu nyingi, ndivyo inazidi kuwa na ujira kidogo. Kazi kweli.

14.Kuna machaguo 2. Kulalamikia mchezo au kujifunza sheria za gemu.

15.Kwanini watu wengi waliotusua ni watu wa kawaida? Kadri unavyozidi kudhani umeelimika na kuwa smart ndivyo unavyojitenga kupoteza gemu ya mtaa.

16.Vipi kama ungefanya yote uliyosema utafanya, leo ungekuwa na matokeo mara 10 zaidi.

17.Umewahi kusikia kitu kinaitwa “leverage” – Pesa iko kwenye kutumia vyema hii kitu. Pesa inatakiwa ije kwa “X” na sio kwa “+”.

18.Usipoteze muda wa kujifunza kitu kama hujui unaenda kukitumia wapi. Ni kupoteza muda. Jifunze kitu unachokitumia moja kwa moja.

19.Bila kujali unafanya mishe gani kwenye maisha yako. Kuuza ndio ujuzi wa lazima popote pale ulipo. Jifunze.

20.Kwanini huwa unawaza kushindwa mara nyingi zaidi kuliko kufanikiwa, ndio maana unafeli. Vipi ungewaza kufanikiwa mara nyingi zaidi kuliko kufeli, ungekuwa wapi?
 
Ukiwa mwanaume inatosha kuwa somo tosha, kama huwezi kukaza na kupambana, utaishiwa kuwa J LOKOLE TU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom