Ukweli kuhusu Maisha

Kuwite94

Member
Oct 10, 2016
16
117
Mwenye degree asiye na ajira kuna wakati huwa anaona bora angeishia form four na angefanya shughuli nyingine...

Na aliyeishia darasa la saba kutokana na hali ya maisha aliyonayo kuna wakati anaona alipaswa kufika chuo kikuu ili awe na maisha mazuri...HUO NDIYO UTAMU WA MAISHA...

Uzuri ni kwamba maisha huwa hayana formula maalum...aliyesoma maskini, wakati asiyesoma ni tajiri, na kuna asiyesoma maskini wakati aliyesoma ni tajiri...

Mwenye pesa anaumizwa na mapenzi mpaka anatamani kuwa Single na asiye na pesa anaachwa kwa sababu hana kipato cha kumudu gharama za mwenzi wake...

Unawaza kuacha shule ili ufanye biashara kwa sababu watu wengi wanafanikiwa na muda huo huo kuna mwenzako anawaza kuacha biashara kwa sababu biashara hailipi ili arudi shule akimaliza akaajiriwe...

Ingelikuwa maisha yana jibu moja wala tusingeona utamu wake...HUAMINI...? chukua hii wakati wewe unaumiza kichwa ufanye nini ili ufanikiwe kuna mwenzako anatamani angefikia walau hata robo tu ya maisha yako...

Ishi kwa amani...ishi kwa upendo, ishi kwa furaha...maisha ndiyo haya haya...hakuna formula zaidi ya kuishi maisha yako...

Hard work pays...Ni kweli wakati mwingine kwenye maisha kufanikiwa huwa ni bahati, ila ni kwa wale tu ambao wanazielekeza bahati kuja upande wao...

Kuna anayejituma sana lakini miaka nenda rudi hafanikiwi na yupo mvivu na uvivu wake anatusua...kuna anayeweka bidii kubwa kwenye kazi/biashara na bado hafikii malengo...(Utamu wa Maisha)

Usiumize sana kichwa kuishi maisha ya wengine kwenye maisha yako....bali unatakiwa kutumia muda wako mwingi kuishi maisha yako kwenye maisha yako...

Dunia inakuruhusu kupanga na kubonyeza kitufe unachoona ni sahihi na huku ikiwa imeficha "button" ya matokeo...kazi yako kubwa ni kuumiza kichwa kipi ni kitufe sahihi unachopaswa kubonyeza ili kikuonyeshe "button" ya matokeo unayoyahitaji MAISHA pamoja na machaguo yote hayo.
 
Hiyo ya kwanza kabisa hapo juu ni kweli kabisa na ndio iliyopo zaidi kwasasa

Kuna jamaa alikuwa analalamika kuhusu maisha na akasema ni bora angeishia form four akaenda kusomea ufundi

Unakuta vijana walioishia Form Four wamenunua viwanja, wamefyetua matofali hata ya kuchoma, wana bajaji kadhaa mjini na mifugo

Wameoa na wana watoto na tena wanawasomesha vizuri tu

Wengine ni wauza chips tu

Sasa wewe na Degree au Masters yako endelea kusubiri kuajiriwa, utakuja kujenga na kuoa ukiwa na miaka 40 au zaidi
 
Maisha ni kama mpira wa soka, mnaweza kuweka juhudi, mkacheza vizuri na Bado mkafungwa, hapo unajua bahati haikua upande wenu.

Natamani na kutambua mchango wa juhudi binafsi, jitihada na bidii lakini haimaanishi Kila anaejituma sana au aliyesoma anafanikiwa.

Kuna wenye Hali mbaya kote Kwa waliosoma na wasiosoma, Hali kadhalika wenye maisha mazuri Kwa waliosoma na wasiosoma.
 
Life is like a box of chocolate you don't know what you will pick in the box –jack ma–
 
Hiyo ya kwanza kabisa hapo juu ni kweli kabisa na ndio iliyopo zaidi kwasasa

Kuna jamaa alikuwa analalamika kuhusu maisha na akasema ni bora angeishia form four akaenda kusomea ufundi

Unakuta vijana walioishia Form Four wamenunua viwanja, wamefyetua matofali hata ya kuchoma, wana bajaji kadhaa mjini na mifugo

Wameoa na wana watoto na tena wanawasomesha vizuri tu

Wengine ni wauza chips tu

Sasa wewe na Degree au Masters yako endelea kusubiri kuajiriwa, utakuja kujenga na kuoa ukiwa na miaka 40 au zaidi
Kwani kuoa au kujenga ukiwa na miaka 40 ni kosa la jinai?

Kila mtu anatembea kwenye 'timeline' yake. Hapa bongo sasa hivi ni saa sita na madikika adhuhuri, lkn kuna nchi nyingine sasa hivi ni usiku, hii haimaanishi Tanzania inachelewa, la hasha! Kila nchi inatembea kwenye timeline yake.

Acheni kukariri. Kuna mtu ameoa na miaka 25 ila hadi sasa hana mtoto/watoto, kuna mtu ameoa na miaka 40 ila ana mapacha 3. Kuna mtu amejenga na miaka 25 akafa baada ya mwaka 1, na kuna mtu amejenga na miaka 40 na anaishi kwenye nyumba yake mpaka sasa.

Tusipangiane maisha.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Naona unajifariji sawa
 
Sasa wewe na Degree au Masters yako endelea kusubiri kuajiriwa, utakuja kujenga na kuoa ukiwa na miaka 40 au zaidi
Maisha hayana formula ndugu.
2012 niliwaza nikipata Bachelor na Masters Kuna kitu (nilikua nakivizia kazini) nitakipata.
Baada ya ku graduate masters December, kufika March kile kitu NILIKIPATA.

Kwangu vyeti vimelipa na vimenifungulia fursa zaidi.

Usidharau DEGREE na MASTERS.

#YNWA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom