Ukweli mchungu ni kuwa JKT inazalisha mafisadi na watu wanaochukia nchi yao badala ya wazalendo

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2022
1,689
3,259
Hii habari ya JKT Tanzania Nyerere aliiga China kwa Mao. Mao alivuruga kila kitu, watu wakatolewa mashuleni, kwamba haina maana na kupelekwa "JKT." Kigezo cha kuingia chuo kikuu kikawa si ufaulu shuleni bali bidii ya mtu na utii huko JKT.

Watu walioenda kule JKT walikutana na mambo ya ajabu sana. Ufisadi wa wakubwa wao, dhuluma, kukosa maadili, uonevu, mazingira ya hovyo ya kazi, kifupi walikutana na mateso yaliyowafanya waiangalie nchi yao kwa jicho la tofauti kabisa.

Kuna jamaa JKT ya huko alipangiwa kufanya kazi zahanati, alishangaa mkubwa mmoja daily kuja kuchukua dawa zilizokuwa tamu kama pipi! Yenye anazila kama pipi, yaani anafanya ufisadi wa hali ya chini kabisa. Alipojaribu kumgomea na kazi yake ya zahanati iliisha. Kule walichofundishwa hasa ni ubinafsi na survival of the fittest, si uzalendo na maslahi ya wote. Unafundishwa upambane uishi kistarehe kama wakubwa wako.

Jamaa huyo anasema jambo pekee zuri alitoka nalo "JKT" ni nidhamu ya kazi. Anadai kuwa hata baada ya miaka mingi, bado anaona si sawa kukaa kwa saa kadhaa bila kujishughulisha na kazi ya kuzalisha.

Hata hapa ushahidi umetuonyesha jinsi watu waliopita JKT walivyofisadi nchi hii. Jinsi walivyotanguliza maslahi yao badala ya yale ya nchi. JKT wanaweza kuwa na mambo mazuri wanafundisha, ila tusidanganyane kuwa wanafundisha uzalendo, ni kinyume chake.

Nadhani tunahitaji namna mpya ya kufundisha watu uzalendo. Namna ambayo imefanya kazi kwenye nchi zingine.
 
Sahihi kabisa, mimi nilichotoka nacho JKT ni kuichukia nchi hii kwa mateso niliyopata kule, uonevu, wizi, kutishana, kuoneana na ufidhuli mwingine mwingi kupita kiasi. Toka hapo nikaichukia na kumchukia Nyerere mpaka leo.

Leo JKT yamekuwa makambi ya kubaka watoto wa kike! makambi ya kutesana na si kufundisha lolote la maana
 
Back
Top Bottom